Wednesday, August 12, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

Ilipoishia Jana

Baada ya kiongozi wa mtandao, Mexk Viego kuongea hayo, aliinama chini na kuiokota ile bastola, akampa Ramona aishike kwa mara ya pili. Ramona alishtuka, mapigo ya moyo wake yaliongezeka kasi zaidi ya mwanzo. Alimtazama kiongozi wake kwa sura ya huruma asitake kumuelewa amekusudia nini kumpa silaha aishike kwa mara nyingine.

SASA ENDELEA

“Ramona wewe ni mwanamke tunayekutegemea sana, wewe mwenyewe unalijua hilo. Kwa kuwa mpenzi wako amekwisha kuzijua siri zetu, hauna budi kumuondoa hapa duniani. Huo utakuwa usalama wako na usalama wetu pia. Achana na masuala ya mapenzi. Wanaume wako wengi hapa duniani, lakini kazi yako iko moja tu tunakuamini malikia wetu. Kuwa jasiri kumbuka kazi hii inavyokupa pesa nyingi. Je, uko tayari ndugu zako wakashindwa kuwa matajiri kwa sababu ya mwanamume. Ili sisi tuwe na imani na wewe badili moyo wako. Tukuamini kama tulivyokuamini mwanzo. Muondoshe mtu huyu duniani,” aliongea Mexk Viego, akiwa amemshika Ramona bega.

Nguvu fulani zilianza kumjia mrembo Ramona, alimtazama Roika kwa jicho la huruma hafifu. Akaishika bastola yake vizuri tayari kwa kuiruhusu risasi itoke. Roika akijua maisha yake yanakwenda kuishia pale, alikiinamisha kichwa chake chini asitake kumtazama Ramona. Alimuomba Mungu amsamehe. Pia akamuomba msamaha na mama yake mzazi kwa kushindwa kumpelekea mchumba, mwanamke ambaye angekuja kufanga naye ndoa. Kwa kuwa siku zote mama yake alikuwa akimlaumu mwanawe, akimwambia kuwa, atakuja kufa akiwa bado hajaoa, kutokana na ubishi wake wa kutotafuta mwanamke.

“Kweli mama uliniambia, nisamehe sana mwanao. Hata hivyo, juhudi hizo hizo za kukutafutia mkwe zimeniponza. Leo nakufa katika nchi ya watu pasipo kuwaaga wewe na mdogo wangu. Nisamehe mama’ngu,” alijisemea Roika kimoyomoyo.

Chozi lake likidondokea kwenye sakafu ya jumba la magaidi.

Ramona hakuwa na jinsi, tayari maneno ya kiongozi wake, Mexk Viego yalikuwa yamekwisha kumuingia. Alimtazama Roika, aliyekuwa anainua kichwa taratibu na kumwambia.

“I Love you Roika. I’m sorry (nakupenda Roika, nisamehe).

Aliposema hivyo, alifyatua risasi ya kwanza iliyokwenda kumtoboa Roika tumboni. Roika alianza kushuka taratibu chini huku akitokwa na machozi.

“Nakupenda sana Ramona,” aliongea Roika kwa sauti isiyokuwa na nguvu.

Kabla hajafika chini akiwa anadondokea  ubavu wa kushoto, Ramona alifyatua risasi ya pili iliyokwenda kumpata tena Roika tumboni. Roika alilala taratibu chini roho yake ikaanza kumtoka. Alianza kuona macho yake yanafifia. hayakuwa na nguvu tena ya kuuona uzuri wa Ramona, mrembo wa dunia kutoka Afrika aliyekuwa mzuri ajabu. Hatimaye akaona mbele giza. Asimuone tena Ramona.

Baada ya tukio hilo, watu wote mle ndani, wamlipigia Ramona makofi. Kiongozi Mexk Viego pamoja na Zahil Bin Shaq walitabasamu na kumshika Ramona bega.

“Nilishasema wewe ni mwanamke mwenye nguvu kuliko wanawake wengine. Hongera sana kama umeweza kumuua mtu umpendaye, inaonyesha ni jinsi gani unaithamini kazi yetu. Futa yote yaliyopita, anza maisha mapya.” Aliongea kiongozi wa Swaba Zahili Bin Shaq.

Baadaye Ramona alivutiwa kiti na kukaa. Kila mmoja mle ndani kwa wakati huo alijiona yu salama. Ule wasiwasi uliokuwepo mwanzo ulikuwa umetoweka ndani ya jengo hilo. Maana mtu aliyekuwa ameingia kwenye jengo lao, mtu aliyekuwa amefanikiwa kuzijua siri zao, tayari alikuwa amekwisha kufa.

Baada ya hapo, kiongozi Zahil alimfuata mpiganaji wake na kumwambia autoe mwili wa Roika aende akauchome moto.  Wakati mambo mengine ya mkutano yakiendelea, mpiganaji huyo aliubeba mwili wa Roika na kutokana nao nje.

Wakati huo moyo wa Ramona ulikuwa kwenye mateso makubwa, mateso ambayo hakuwahi  kuyahisi tokea azaliwe. Alijikaza vilivyo asionyeshe kuwa kumuua mpenzi wake ilikuwa imemuumiza sana.

Ikiwa ni saa moja joini, Shazayi mtoto wa Rais alikuwa bado ameegama kwenye usukani wa gari lake. Alishaanza kusinzia kutokana na kukaa pale kwa muda mrefu. Toka saa saba mchana hadi saa moja usiku hakika alikuwa amechoka. Alijikutana anaanza kulia, pindi alipolikumbuka tabasamu la Roika, mwanamume aliyeonana naye siku mbili tu na kumpenda ghalfa. Ingawa alijua kuna siri kubwa juu ya maisha ya Roika, kutokana na jinsi alivyomuona mrembo wa dunia Ramona Fika, alitaka kuachana na suala la kumfuatilia Ramona. Maana alikuwa amekaa pale kwa muda mrefu bila kufanikiwa kugundua kitu wala kuona Ramona akitoka.

Aliwasha gari akitaka kugeuza kurudi nyumbani kwake. Kwani ukimya wa mtaa ule ulizidi kumuogopesha sana.

Akiwa ananyonga ufunguo, kwa mbali alimuona mtu mmoja akitoka ndani ya jengo lile. Mtu huyo alikuwa ameubeba mwili wa binadamu, mwili ambao aliutua na kuupakia kwenye gari. Macho yalimtoka Shazayi, alibaki kumtazama mtu yule, asilijue lengo lake.

Nini kitafuatia usikose kesho               

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -