Friday, November 27, 2020

Upendo Kushinda Ufahamu [17]

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Ilipoishia Jumanne

Kabla hawajazamia koridoni, tayari Roika alikuwa nyuma yao. Watu hao walipofika mlango wa chumba cha Ramona walisimama na kubisha hodi. Ramona aliyekuwa ndani alifungua mlango wote wanne waliingia ndani.

Roika Malino alishtuka sana, alibaki ameganda pale nje, asijue watu wale wamefuata nini chumbani kwa Ramona.

SASA ENDELEA

ALIBAKI amesimama pale koridoni akiutafakari ujio wa wale watu waliokuwa wameingia chumbani kwa Ramona.

Roika aliamua kupitiliza chumbani kwake, ambako alikaa na kuanza kukiumiza kichwa chake kwa swali lisilo na jibu. Watu wale wanne waliingia kwa Ramona kufanya nini. Ukizingatia alikuwa kwenye kifungo kikubwa cha jela ya mapenzi, basi alizidi kuumia kupita kawaida. Alikaa mle chumbani akiwa na shauku ya kutaka kujua Ramona na wale watu wanafanya nini au wanazungumza kitu gani.

Huzuni na maumivu ya moyo yalizidi kumtesa Roika. Alishindwa kuushinda wivu alionao kwa Ramona. Baadaye alijiuliza au wale watu wanafanya biashara na Ramona? Swali hilo lilimpa kidogo nafuu ya maumivu aliyokuwa anayahisi.

Baadaye aliamua kurudi kwenye ukumbi wa mpira, mahali alipokuwepo mara ya kwanza, kabla wale watu hawajafika. Ingawa yeye ni mtu anayependa sana kutazama soka lakini siku hiyo hakutamani kuangalia mpira, akili yote ilikuwa kwa wale watu waliokuja kwa Ramona. Pale nje ya magari yao walikuwa wamebaki watu watatu waliokuwa wamevaa suti nyeusi na miwani, wakiangaza huku na kule. Ilionyesha wako makini na kazi yao.

Baada ya nusu saa kupita, wale watu walitoka chumbani kwa Ramona na kurudi kwenye magari yao, mtu aliyeonekana kuwa ndio bosi wao, walikuwa wanamuweka katikati ili kumlinda maana ilionyesha ni mtu mkubwa tena mwenye fedha nyingi. Waliingia kwenye magari yao kwa sekunde kadhaa hawakuwasha magari. Wakati wanatoka, Roika alikuwa amewakazia macho akijaribu kuwapeleleza kwa hisia na kuona.

Magari hayo aina ya range. Yenye rangi nyeusi, yaliondoka pale hotelini na kueleka kule kusikojulikana. Roika aligeuza shingo na kuendelea kuangalia mpira, wakati huo tayari mechi kati ya Barcelona na Atletico Madrid ilikuwa inaelekea kumalizika. Hata hivyo bado aliendelea kusumbuka juu ya ujio wa wale watu. Baadae aliamua kuacha kufikiria jambo hilo baada ya kujiridhisha kuwa watu wale watakuwa ni wafanyakazi kwenye masuala ya kibiashara na Ramona.

Ikiwa ni saa mbili usiku, Roika alikuwa chumbani kwake, ikiwa ni mara baada ya kumaliza kutazama mechi, wakati huo alitamani kuonana na Ramona waliyekuwa wameonana mchana.

Akiwa amekaa sebureni kwake huku akitazama runinga, mlango wake uligongwa, aliinuka kwenda kuufungua akijua labda ni Ramona au muhudumu wa hoteli  aliyekuwa akimgongea.

Alipoufungua alikutana na muhudumu aliyeitwa Sarah, ambaye siku anafika pale hotelini alikuwa amemuuliza kuhusu uwepo wa mrembo wa dunia pale hotelini. Roika alishtuka kidogo baada ya kukumbuka kuwa msichana huyo alikuwa amemuahidi jambo. Alikumbuka siku ile alikuwa amemuahidi, kuwa watakaa na kuzungumza yao, akimaanisha watatoka kimapenzi. Ahadi  iliyokuwa ni ya uongo. Kutokana na Roika kuhitaji majibu mazuri, ilikuwa imemlazimu  kumdanganya binti huyo kwa ahadi ya kutoka kimapenzi, akijua baadae binti huyo hata fikiria suala hilo na kama atafikiria basi atataka pesa.

Muhudumu huyo alitokea kumpenda sana Roika, siku hiyo aliamua kumfuata Roika chumbani  ili kumuuliza kuhusu ahadi aliyokuwa amemuahidi.

Roika alipomuaona alionyesha tabasamu la kujnilazimisha, wakati huo Sarah alikuwa akitabasamu kwa furaha zote, huku akiyalegeza macho yake yaliyoonekana kama yanataka kuanguka. Ile hali ya uhudumu iliyomfundisha kuwa na heshima kwa wageni ilikuwa imemtoka.

“Habari Mr Roika,” Sarah alisalimia huku akionyesha mwili wake kuna kitu ulihitaji.

“Nzuri tu nikusaidie nini?” aliuliza Roika kana kwamba hakufahamu alikuwa amemuahidi nini msichana huyo.

“Naweza kuingia ndani kwako?” Sarah aliuliza.

Roika hakujibu chochote zaidi, alimpisha  aingie ndani, Sarah alipiga hatua kwa mwendo usiokuwa wa kawaida. Alipofika ndani, alikaa kwenye kiti na kuweka mguu wake mmoja juu ya mguu wake mwingine, wakati huo Roika alikuwa anatafuta maneno mengine ya uongo ya kumueleza, juu ya ahadi aliyokuwa amemuahidi. Alipomtazama, alikuta vifungo vya shati lake la kazi vikiwa vimefunguliwa sehemu ya kifua. Sidilia ya rangi nyeupe ilionekana huku matiti mazuri ya msichana huyo,  yaliokuwa yana uwezo mkubwa wa  kumtamanisha mtu, yalikuwa yamesimama.

“Roika unaniuliza unisaidie nini, wakati unajua ulichoniahidi?” Sarah aliuliza.

Roika hakujibu chochote, zaidi alielekea kwenye begi lake liliokuwa kabatini, ambapo alilifungua na kutoa kiasi cha pesa, ambacho ni dola 600, sawa na shilingi milioni moja za taifa la Tanzania. Alimtazama Sarah kwa sekunde kadhaa,  akanyosha mkono kumpa zile pesa. Sarah alimtazama Roika kwa huzuni yenye hasira, huku akiwa amekunja ndita.

“Sihitaji pesa,” Sarah aliongea.

Roika alipatwa na mshangao, macho yalimtoka asiamini kile muhudumu Sarah alichokuwa amemjibu.

“Sasa unahitaji nini?” Roika aliuliza.

“Pesa si muhimu kwangu, cha muhimu ni penzi lako.”

“Sikia Sarah, kwa sasa sina muda wa kufanya hivyo, naomba uondoke nitakutafuta wakati mwingine.”

“Roika usinifanyie mjinga, hadi nakataa pesa ujue nakupenda. Na uliniahidi tutakaa na kuzungumza yetu. Siwezi kutoka humu ndani hadi utimize ahadi yako ya mara ya kwanza si kunipa ahadi nyingine, na sihitaji pesa zako”

“Unataka kulala na mimi tu?” Roika aliuliza.

“Sio kulala na wewe tu bali nahitaji kupendwa na wewe.”

Wakiwa wanaendelea na maongezi hayo, maongezi ambayo Roika alikuwa akiyafanyaa kwa haraka, akihofia mrembo Ramona kuja chumbani kwake, kengere ya mlango ililia, ikiashilia nje kuwa kuna mtu alikuwa anamgongea. Roika alishtuka, moja kwa moja alijua kuwa anayegonga ni Ramona.

“Sawa naomba uje kesho saa tano usiku, saa hizi nina maongezi na mtu wangu wa kazi, tafadahri Sarah,” aliongea Roika ambaye alijishusha huku akihofia uwazi mdogo wa kwenye kifua cha muhudumu Sarah. Usije kuonekana mbele ya Romana.

Kwa shingo upande Sarah aliinuka kwenye kiti, akamsogelea Roika aliyezidi kuwa muoga, akataka kumbusu lakini Roika aligeuka kutazama pembeni.

“Sawa mi nakwenda ila tambua nakupenda na ninaamini hauta vunja ahadi yako.” Aliongea Sarah na kuelekea mlangoni.

Roika alienda kufungua mlango haraka, ili Sarah atoke, wakati huo pia kuna mtu mwingine alikuwa akimgongea. Alipofungua mlango macho yake yaligongana na macho ya mrembo Ramona. Sarah naye alishtuka baada ya kumuona mrembo wa dunia amesimama mlangoni, Ramona naye alionyesha kushtuka kidogo, kumuona muhudumu anatoka chumbani kwa Roika. Kilichomshtua si muhudumu huyo, kuingia chumbani kwa Roika la hasha, maana ni kazi yake, zaidi alipatwa na mshangao ambao hakuuonyesha wazi baada ya kuona vifungo vya shati la muhudumu huyo wa hoteli vikiwa vimefunguliwa.

Roika alikuwa katika wakati mgumu kupita kiasi akijishtukia sana pindi Ramona alipokuwa amesimama mlangoni na muhudumu Sarah akitoka mle chumbani.

“Karibu Ramona,” aliongea Roika akiwa amejikaza ili asishtukiwe kama alikuwa amejawa na wasiwasi.

“Asante sana,” alijibu Ramona huku akipiga hatua kuingia ndani akionyesha hana wasiwasi wowote.

Ramona alipishana na Sarah aliyekuwa anaonyesha uwoga wa kujishtukia.

Roika alifunga mlango wakati tayari Ramona yuko ndani na Sarah amekwisha ondoka.

“Habari Ramona karibu sana,” aliongea Roika.

“Asante sana Roika, naona leo ulikuwa makini sana na mambo mawili,” alijibu Ramona kwa tabasamu zuri na kwa utani mwingi.

“Mh! Mambo mawili kivipi?” kwa mshangao Roika aliuliza.

“Ulikuwa makini kutazama mpira, na pili ulikuwa makini na muhudumu wa hoteli.”

Licha ya Ramona kuongea kwa utani, lakini Roika alikasirika, maneno hayo yalikuwa, yameusurubu moyo wake. Moyo unaompenda Ramona kupita kiasi chake cha kupenda. Hata hivyo Ramona alijua kuwa maneno aliyoyazungumza, Roika alikuwa hajayapenda. Alitabasamu na kumpiga Roika begani.

“Nakutania Roika naona ulianza kukasirika.”

“Hapana mimi sijakasirika.”

“Lakini ni kweli leo ulikuwa makini sana kutazama mechi, hadi ukaniacha peke yangu chumbani.”

Roika aliposikia hivyo aliona huo ndio muda wa kufahamu wale watu waliokuja chumbani kwa Ramona walikuja kufanya nini, walikuwa na mipango gani na Ramona je ni watu wake wa biashara au kulikuwa na  jingine?

“Mbona wewe ulikuwa makini na wale wageni wako? hata haukukumbuka kuja kutazama mechi na mimi.”

“Uliwaona?”

“Iweje nisiwaone?”

“Wewe ulikuwa makini kutazama mpira, ulijuaje kama walikuja kwangu?” aliuliza Ramona swali lililokuwa limemuingiza Roika mtegoni.

“Wakati nakuja kuchukua simu yangu niliyoiacha chumbani, hao watu nao walikuwa mbele yangu, ndipo nikawaona wanaingia chumbani kwako.”

“Mh! Kweli?”

“Hakika, wala sikuwaona wakati mwingine zaidi ya huo.”

“Sawa Roika tuachane na hilo, wale ni watu wangu tunaofanya nao biashara. Ehee niambie kesho hatuwezi kutoka?”

“Inawezekana kwa nini isiwezekane,” alijibu Roika aliyeonyesha kutoridhika na majibu juu ya wale watu waliokuja chumbani kwa Ramona.

“Sawa Roika mimi leo sikeshi sana usiku huu nakwenda kulala. Kesho asubuhi nitajiandaa mapema nawe fanya hivyo,” aliongea Ramona huku akisimama pale kwenye sopha.

“Sawa mrembo,”  alijibu Roika kwa tabasamu.

Wakati Ramona anatoka mle chumbani Roika alitamani hata kumkumbatia, lakini nguvu hizo hakuwa nazo kwa kuwa Ramona ni mwanamke mwenye kiwango cha juu sana.

Asubuhi ya siku iliyofuata, Ramona alikuwa  amekwisha jiandaa, hakika alikuwa amependeza zaidi ya jana, kila siku uzuri wake ulizidi kubadilika badilika mithili ya rangi nzuri za kinyonga. Roika alipomtazama, alijihisi hana hadhi ya kuwa pembeni ya Ramona. Hakika alizidi kuwa zaidi ya mlevii katika kupenda.

Walitoka na kuelekea nje ya hoteli, Ramona aliwataka walinzi wake wabaki hotelini wakati yeye anatoka na Roika. Walimpinga wakitaka kuambatana naye wakihofia usalama wake. Lakini aliwalazimisha kubaki, baadae walimtii.

NCHINI TANZANIA

Biyanah mwanamke bilionea mtu aliyeanza kudhohofika mwili kutokana na mapenzi, alikuwa nyumbani kwake akiitazama picha ya mwanaume Roika huku machozi yakimtoka. Huzuni ilikuwa imetawala kwa mgonjwa huyo wa mapenzi. Ni siku ya tatu tokea Roika amwambie kuwa atakuwa amerudi nchini Tanzania lakini hadi wakati huo bado, Roika alikuwa hajarudi Tanzani na hakuna ujumbe wowote aliokuwa ametumiwa wala kupigiwa simu.

Moyo ulimuuma sana binti wa tajiri Branko Rumo, alilia kila wakati. Hakupenda kumpoteza Roika mtu aliyeahidi kuutumia hata utajiri wake kumpata.

Uamuzi aliokuwa ameufikia ni kuamua kumfuata Roika nchini Mexico, akijua kuwa Roika yuko huko kikazi.

Nini kitafuatia?Usikose kesho     

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -