Sunday, January 17, 2021

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

Ilipoishia jana

Hakika Roika alizidi kuchanganyikiwa, kwani tayari yeye alishakuwa na nguvu, lakini Shazayi hakuwa na nguvu na ilionekana kuwa muda si mrefu hali ya huzuni itakwenda kutokea.

Taratibu huku machozi yakimtoka, Roika aliusogeza mdomo wake karibu kabisa na mdomo wa Shazayi, akambusu. Shazayi alitabasamu na kisha akasema.

 “Thank you Roika.” (asante Roika).

Aliposema hivyo, alifumba macho.

SASA ENDELEA

Roika alianza kulia kilio kikubwa, japo hakuwa na nguvu ya kusimama pale kitandani, kutokana kuwa na kidonda kikubwa tumboni, aliinuka na kuishusha miguu yake chini. Akamsogelea Shazayi na kuanza kumuita, lakini Shazayi hakuitika.

Daktari akiwa amechanganyikiwa, alisogea pale na kuanza kumpima Shazayi. Wakati huo Roika aliendelea kumlaumu daktari kwa kukubali kumtoa damu Shazayi na kumuongezea yeye.

“Dk kwa nini ulikubali kumtoa damu? Ulishindwa kuwa na hata chembe ya woga kujua kuwa huyu ni mtoto wa Rais. Haya utasema nini kwa serikali yako, utamwambia nini Galim Halim?” aliuliza Roika akionekana ni mtu anayekwenda kuwa kichaa.

Daktari hakuwa na jibu, aliendelea kumhangaikia Shazayi. Maana hata yeye alizidi kuwa na hofu kubwa endapo binti huyo wa Rais atapoteza maisha.

“Kwa nini hukuniacha mimi nife?” aliendelea kuhoji Roika huku akilia sana.

Baadaye alikaa chini na kuendelea kulia. Hakuwa na cha kufanya alibaki kusubiri neno la mwisho la daktari huyo, ambaye mwanzo alikuwa akimpenda. Lakini kwa muda huo, alikuwa akimuona mzembe kutokana na kukubali kufanya kitendo cha hatari cha kumuokoa yeye na kumuua binti wa Rais.

Baadaye daktari alipata majibu. Akamgeukia Roika aliyekuwa na shauku ya kutaka kujua neno lolote isipokuwa  la Shazayi amekwisha kufa.

“Mr Roika Shazayi bado anaishi, lakini ili aendelea kuishi anahitaji nusu lita ya damu, damu kutoka kundi ‘O’, ana siku tatu za kuishi.”

“Naomba unitoe mimi damu na umpe Shazayi.”

“Haiwezekani.”

“Kwa nini isiwezekane?”

“Kwa sababu masaa mawili yaliyopita, yeye alikuwa akikuongezea wewe. Hivyo damu yako haifai kwa sasa kumpa, labda ipite wiki moja ndio utaweza kumuongezea. Pia damu ya kundi ‘O’ ni damu adimu sana hapa hospitali. Mimi nadhani zoezi hili ni gumu kulifanikisha. Ukizingatia wewe huna uwezo wa kutoka hapa hospitali, kutokana na hali yako kuwa si nzuri.”

“Nitakwenda mimi kuitafuta na kuileta hapa,” aliongea Roika kwa ujasiri.

Lakini daktari alijua Roika anasema tu, ukweli halisi asingeweza, kutokana na kwamba masaa manne yaliyopita alitoka kufanyiwa operesheni ya kutolewa risasi. Hivyo isingewezekana kabisa.

“Mr Roika, huwezi kwenda kokote. Kutokana na hali uliyokuwa nayo, kubali kushindwa, kubali kumpoteza Shazayi.”

“Niache nitakwenda,” aliongea Roika kwa ukali mkubwa.

Ikiwa ni saa kumi alfajiri, Roika alimwambia daktari amuitie teksi. Kutokana na Roika kuwa mbogo, daktari hakuwa na jinsi, alimpigia simu dereva taksi aje pale hospitalini. Roika aliinuka kwa tabu na kumwambia daktari.

“Kwa hali yoyote ile, popote ilipo damu, nitaileta, Shazayi lazima apone.”

Baada ya kusema hivyo, Roika alijikongoja hadi nje ya hospitali, akimuacha daktari katika sintofahamu. Alipofika nje alimwambia dereva amuwahishe uwanja wa ndege.

Lengo la Roika lilikuwa ni kusafiri hadi Tanzania kwenda kuifuata damu. lilikuwa ni jambo la kushangaza, japo daktari alimwambia kuwa Shazayi ana siku tatu za kuishi hapa duniani. Kwa kuwa damu ya kundi ‘O’ ilikuwa ni ngumu kupatikana, urahisi ambao Roika aliuona ni kusafiri kwenda nyumbani kwao. Ilikuwa ni baada ya kukumbuka kuwa mama yake mzazi, damu yake iko kwenye kundi ‘O’.

Aliamini kuwa ndani ya siku tatu anaweza kusafiri kwenda Tanzania na kurudi. Ingawa hali yake kiafya ilikuwa mbaya alijituma hivyo hivyo.

Si hofu tu ya kumpoteza mtoto wa Rais, lakini tayari alikwisha kujua kuwa Mungu amekwisha mpa mke, mke ambaye yeye hakumtarajia. Aliamini mapenzi ya Shazayi kwake ni mapenzi ya ajabu.

Kwa muda huo hakutaka kujiuliza, ilikuwaje amepona, lakini swali kuu kwake lilikuwa ni je, Shazayi ameingia vipi kwenye tukio lake. Lakini akili yake kwa muda huo ilikuwa ikifikiria ni jinsi gani atafaulu kumuokoa binti huyo wa Rais.

Lakini kwa mtu mwingine angemuona Roika hana akili kwa kitendo chake cha kusafiri na hali aliyokuwa nayo kutoka Pakistani kwenda Tanzania ili kwenda tu kuifuata damu. Lakini kuokoa maisha ya binti huyo wa Rais ilibidi iwe siri. Maana serikali ikijua yeye na daktari watakuwa matatani.

Nini kitafuatia? usikose kesho        

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -