Tuesday, November 24, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU [20]

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Ilipoishia Jumamosi

Roika alikuwa amepanga tena kusafiri  kwa mara ya pili kumfuata mrembo wa dunia, Ramona Fika nchini Pakistani. Kwa akili ya kawaida ya binadamu isingeweza kufanya hivyo, ukizingatia nchi ya Pakistan haina amani ya kutosha. Roika hakujali Ramona amekwenda kufanya nini, alichojali yeye ni mapenzi. Siku ya nne hiyo, alishakuwa amemsahau mpenzi wake Biyanah mwanamke tajiri mtoto wa bilionea Branko Rumo bilionea wa wa tatu barani Afrika.

SASA ENDELEA

Hakuwa na muda wa kusubiri, moja kwa moja aliifuata simu ya mezani. Akachukua kitabu cha simu cha hoteli na kuzitafuta namba za uwanja wa ndege wa HIA, ambapo aliwapigia na kuomba akatiwe tiketi ya kuelekea Pakistani.

“Samahani hatuna ndege ya moja kwa moja inayoelekea Pakistan, bali tuna ndege ya kwenda Israeli, ukifika Israeli ndio utapata ndege ya kuelekea Pakistani,” aliongea mfanyakazi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Haiti.

“Sawa nitaomba tiketi ya kuelekea huko, je, ndege ya mapema inaondoka saa ngapi?” Roika aliuliza.

“Ndege ya mapema ni ile inayoondoka saa kumi jioni.”

“Sawa nitasafiri na hiyo hiyo.”

“Jina lako nani tafadhari?”

“Naitwa Roika Malino namba yangu ya pastipoti ni 332115 TZ.”

“Sawa Mr Roika, saa tisa na nusu uwepo uwanjani, tafadhali.”

“Bila shaka.”

Roika alikata simu baada ya kumaliza kuongea na mfanyakazi wa kike kutoka  uwanja wa ndege. Saa sita mchana alianza kupanga nguo zake na vitu alivyokuwa navyo tayari kwa safari ya kuelekea Israeli ambapo atapanda ndege ya kuelekea Pakistani. Baadaye kidogo aliletewa chakula na mhudumu wa hoteli. Ingawa hakuwa na hamu ya kula  alijitahidi kujilazimisha ili tumbo lipate nguvu ya kwenda kumsaka Ramona.

Alipomaliza kula, aliketi na kuchukua laptop yake ambapo aliingia kwenye barua pepe akatuma ujumbe kwenye benki, muda si  mrefu, benki ya Barclays walimpigia simu.

“Natumaini tunaongea na Mr Roika,” mfanyakazi wa benk aliongea.

“Ndio.”

“Naomba kukusaidia Mr Roika.”

“Nahitaji kutuma pesa kwenye akaunti nne tafadhali,” Roika alijibu.

“Sawa nitaomba unitajie neno lako la siri.”

“Twiga.”

“Sawa ninaomba namba za akaunti hizo unazotaka kutuma pesa.”

Roika alimtajia namba zote

“Kila akaunti unataka kiende kiasi gani cha pesa?”

“Dola 2000. Tafadhali.”

“Sawa Mr Roika tayari zimekwisha tumwa, kuna jingine nikusaidie?”

“Hapana, nashukuru.”

“Sawa asante kwa kuichagua Barclays nakutakia siku njema.”

“Asante, nawe pia.”

Roika alikuwa amemaliza kuwasiliana na benki ya Barclays ambayo ndio benki yake ya kuhifadhi pesa. Alikuwa amewataka kumtumia pesa katika akaunti nne. Akaunti nne hizo ni akaunti za vituo vyake vya kuwalea watoto yatima wazee na walemavu. Roika alikuwa anaweza kusahau yote lakini, si kuwasahau watu wa kwenye vituo vyake. Aliwajali sana kama anavyojijali yeye mwenyewe. Popote pale alipokuwa,  alihakikisha vituo vyake vinaendelea kuwatunza watu vizuri.

Akiwa amemaliza zoezi hilo la dakika 15, kengele ya mlango ililia, ikiashiria nje kuna mtu anamgongea. Alijua lazima atakuwa ni muhudumu. Alimwambia kwa sauti aingie, kwani mlango ulikuwa wazi.

Macho yake yaligongana na Sarah, mhudumu wa hoteli. Roika alipatwa na mshangao, akabaki kimya asijue nini cha kufanya wala cha kusema. Sarah alifunga mlango na kusogea pale Roika alipokuwa amekaa.

“Habari,” Sarah alimsalimia Roika kwa unyonge wa hali ya juu.

“Njema sijui wewe?” Roika alijibu.

“Si njema sana.”

“Kwanini?”

“Roika unafahamu ni kwa nini. Naomba usinifanyie hivyo. Nakupenda sana Roika, nahitaji uwe wangu.”

“Haitawezekana Sarah, mimi nina mke.”

“Roika najua unanidanganya wewe haujaoa bado, tafadhali usinikatalie.”

“Unajuaje kama sijaoa? Wewe hunijui na mimi sikujui. Mimi natokea Tanzania na wewe ni wa Haiti. Iweje usema nakudanganya? Tayari mimi nina mke na watoto wawili. Hivyo siwezi kumsaliti mke wangu nampenda sana, kwa hiyo Sarah utanisamehe.”

“Hapana Roika usiseme hivyo, mimi niko tayari kuwa mke wako wa pili. Amini siwezi kuishi bila wewe.”

“Nisikilize Sarah, wewe ni msichana mzuri, tena mrembo, hakuna mwanamume wa kukataa. Hata mimi naamini nisingekuwa na mke huenda ningekukubalia, lakini siwezi kumsaliti mke wangu na sijafikiria kuwa na mke wa pili. Usilie, wanaume wako wengi watakaokupenda.”

Sarah alilia sana pindi Roika alipokuwa anaongea hayo. Maumivu ya mapenzi yalikuwa ni makali sana. Baadaye kidogo alifungua vishikizo vya shati lake, akalivua na kubakia na sidiria. Roika alichanganyikiwa, akabaki kumkemea asifanye hivyo.

“Sarah unafanya nini? Hebu acha vaa shati.”

Lakini Sarah hakusikia hilo, ndio kwanza akavua na sketi, akavua sidiria na kubaki kama alivyozaliwa. Huku akilia akasogea mbele kidogo na kumwambia Roika:

“Kama umenikataa basi, tafadhali naomba penzi lako ili nifarijike.”

Roika alibaki ameduwaa, asijue cha kujieleza maana nguvu za kumkaripia Sarah zilikuwa zimemuisha. Ilikuwa kwa mwanamume yeyote angeliona umbo la Sarah, angeshindwa kufurukuta, lazima angekubali yaishe kwa kufanya kile alichokuwa amekitaka msichana huyo.

Sarah alisogea hadi kwenye kifua cha Roika, akamtazama Roika usoni, taratibu alianza kuupelekea mdomo wake, mdomo wenye lipstiki ya rangi ya zambarau karibu na mdomo wa Roika. Taratibu kabisa Sarah akambusu Roika, hisia kali za mahaba zilimpelekea Sarah kuanza kufungua vishikizo vya shati la Roika. Alipokifungua kishikizo cha tatu, Roika alimshika mkono ili asiendelee kufanya hivyo.

“Sarah subiri kwanza,” Roika aliongea.

“Nini tena?” kwa huzuni Sarah aliuliza.

Roika alilichukua shati na kumfunika Sarah, akamtazama kwa tabasamu zuri tabasamu lililomfanya Sarah kujisikia anakwenda kupona maumivu ya mapenzi. Akayashika mabega ya Sarah, na kumbusu. Sarah hakuamini, alibaki kumtazama Roika usoni kama mtu aliyekunywa kilevi kikali, nguvu zilimuishia kabisa.

“Nimetambua unanipenda, nami sina budi kukupenda,” aliongea Roika.

Sarah alishtuka.

“Kweli?” kwa furaha isiyo kifani Sarah aliuliza.

“Kweli Sarah, naomba ukae chini tuzungumze.”

Sarah alikaa kwenye sofa akiwa na shauku ya kumsikia Roika atasema nini. Baada ya sekunde kumi za ukimya, Roika alimwambia kuwa asiwe na wasiwasi, tayari ombi lake amelikubali.

Hakika furaha ilikuwa kubwa kwa Sarah, alimrukia Roika na kumkumbatia kama chizi. Baadaye Roika alifungua waini akamimina kinywaji kwenye glasi mbili glasi moja akampa Sarah.  Kwa furaha kubwa na kicheko Sarah aliipokea na kuomba kuigonganisha na glasi ya Roika. Waligonganisha glasi na kuendelea kupata kinywaji huku maongezi yao yakiendelea. Sarah alimwambia Roika kuwa anaacha kazi na kumfuata yeye nchini kwake. Roika alimwambia asiwe na wasiwasi, kwa kuwa amempenda watasafiri wote kulekea Tanzania. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa Sarah.

Waliendelea kuongea mengi wakitaniana na kucheka, furaha ilikuwa imetawala mle ndani, Sarah alishasahau kuwa yuko kazini. Mara kwa mara Roika alikuwa akiitazama saa yake ya mkononi pasipo Sarah kujua. Wakati huo ilikuwa ni saa nane kasoro. Muda huo ndio ilitakiwa Roika ainze safari ya kuelekea uwanja wa ndege, maana ni masaa mawili kutoka hoteli ya Lompi hadi huko. Kwa muda huo Roika alikuwa akiomba kimoyomoyo Sarah aondoke ili yeye apate muda wa kuondoka.

Baada ya dakika tano Sarah alimwambia Roika.

“Naomba niende kwanza ofisini kwetu. Nitarudi baada ya dakika 20, sawa mpenzi.”

“Sawa ila leo utalala kwangu,” alijibu Roika kwa tabasamu, tabasamu zuri lililozidi kumfinyanga Sarah.

“Sio leo tu mpenzi, kila siku kitanda changu ni kile pale,” Sarah alijibu.

Baadaye alivaa vizuri nguo zake za kazi ambazo ni shati la njano na sketi nyeusi, akamfuata Roika na kumbusu, akamuaga na kumwambia kuwa, atarudi muda si mrefu.

Sarah alipotoka, Roika alizitumia dakika tatu, kuhakikisha anamalizia kupanga kila kitu kwenye mabegi yake. Alivaa kofia yake nyeusi pamoja na mtandio. Akatoka  kulekea nje ya jengo la hoteli. Akiwa makini ili mhudumu atakaye kuwa ni Sarah asimuone. Alifanikiwa kwenda hadi mapokezi ambapo alipiga sahihi kwenye kitabu cha wageni.

“Asanteni kwa huduma zenu bora nitakaribia tena,” aliongea Roika.

“Asante sana karibu tena, na tunakutakia safari njema.”

“Thanks! See you.”

Roika alifanikiwa kutoka eneo la mapokezi ambapo alipewa gari la hoteli ambalo lilitakiwa kumpeleka hadi uwanja wa ndege. Aliondoka hoteli ya Lompi saa 8:15 mchana.

Saa tisa na nusu alikuwa anawasili uwanja wa ndege wa HIA (Haiti International Airport) moja kwa moja alielekea mapokezi, hakutaka kuonyesha kitambulisho chake cha UN, bali aliamua kutoa pesa ili kupewa tiketi hiyo. Baada ya kupewa tiketi, alielekea sehemu ya ukaguzi ambapo alikaguliwa. Saa 10:00 alikuwa ndani ya ndege, ndege iliruka na kuanza safari ya kuelekea Israeli.

Huku hoteli ya Lompi Sarah akiwa mwenye furaha kubwa, furaha  ambayo ni ngumu kuielezea, alikuwa anarudi chumbani kwa Roika, akiwa amependeza sana. Hakubonyeza kengele ya kubisha hodi, moja kwa moja alipitiliza ndani.

“Roika!,” Sarah aliita baada ya kuona ukimya umetawala.

“Roika mpenzi uko wapi, ahaa umejificha nitakuona tu.”

Baada ya kuona sebuleni hamuoni Roika, alielekea hadi chumbani, ambako pia nako hakumuona Roika zaidi aliona bahasha na pesa zikiwa juu ya kitanda. Mwili ulianza kutetemeka, furaha yake ilianza kushuka kama theluji akaisogelea bahasha na kuifungua. Hakukuta maelezo mengi zaidi ya maneno matatu.

“A’M REALLY SORRY” (samahani sana).

Alipiga kelele kama mtu aliyepagawa na pepo, akaichana ile bahasha, na kuzichana chana pesa ovyo. Alilia sana na kuzunguka mle chumbani kama mtu aliyeng’atwa na mbwa mwenye kichaa. Jasho lilimtoka ovyo. uzuri wake ulipotea ghafla. Akaelekea subuleni, kwa hasira akachukua chupa na kuipasua. Akiwa mwenye hasira kali alijichoma tumboni, damu nyingi zilimtoka, dakika mbili baadaye, msichana mzuri Sarah alipoteza maisha.

Baada ya msaa matatu, taarifa ilitolewa kwa uongozi wa hoteli na wahudumu wengine kuwa Sarah amefariki dunia. Mwili wake haukotolewa wala kuguswa hadi pale polisi walipofika eneo la tukio, ndani ya chumba alichokuwa anaishi Mr Roika Malino. Polisi walianza upepelezi juu ya kifo cha msichana huyo. Taarifa ya Bwana Roika Malino kuhusika na kifo cha Sarah ilitangazwa kwenye vyombo vya habari.

Ndege ya Haiti Airways ilikuwa inatua uwanja wa kimataifa wa jijini la Yerusalemu nchini Israeli. Akili ya Roika ilikuwa mbali, ikimfikiria Ramona. Hakika alikuwa ni mtu aliyekuwa amejitoa ufahamu, hakutaka kujiuliza mara mbili mbili juu ya safari yake ya kumfuata mrembo Ramona nchini Pakistani.

Masaa mawili baadaye alikuwa tena ndani ya ndege, akiondoka Israeli kuelekea Pakistani.

Nini kitafuatia? usikose kesho   

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -