Thursday, October 29, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU [24]

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

Ilipoishia jana

Aliamua kulelekea kwenye lifti ambapo aliingia na kubonyeza kitufe namba sifuri, akitaka kwenda chini kwanza kabla ya kuelekea ghorofa ya nne ambako kuna chumba chake. Alipofika chini ambako kuna watu wengi, mbele yake aliwaona watu wasiopungua watano, wakitoka nje na kuingia ndani ya hoteli, wakija kwenye lifti. Watu hao aliwaona ni wa tofauti kidogo, kutokana na umakini wao na mavazi yao. Licha ya kuwa Pakistani ni nchi ya Kiislamu, lakini uvaaji wa watu hao ulikuwa tofauti kidogo na wengine. Walikuwa wamevaa kanzu nyeupe ambazo ni za gharama kubwa. Huku wakiwa wamejifunga vichwa vyao na mitandio myeupe. Machoni walikuwa wamevaa miwani myeusi ndevu zao zilikuwa ndefu kidogo.

SASA ENDELEA

Roika alipishana na wale watu, akiwaacha wakipanda lifti wakati yeye anakwenda eneo la bustani. Alifika na kukaa bustanini. Muda haukupita, alijikuja mhudumu wa hoteli akiwa na vinywaji. Alichagua kinywaji na kuendelea kuituliza akili yake pale bustanini. Maumivu ya mapenzi aliyokuwa nayo yalizidi kumtesa kuzidi jana. Hakujua ni siku gani atakayokuwa anafunga ndoa na Ramona.

Alianza kujilaumu kwa kumfuata Ramona Pakistani. Ile hasira aliyomuona nayo Ramona kule ndani ilizidi kumweka katika mazingira magumu ya kumpata mrembo huyo. Baadaye aliwakumbuka wale watu aliopishana nao eneo la lifti. Bila kujiuliza alijua lazima wale watu watakuwa wameelekea chumbani kwa Ramona. Swali lililoanza kumsumbua kwa muda huo ni baada ya kujiuliza ni biashara gani anayofanya Ramona. Wale watu ni nani kwake?  Baadae pia  alikumbuka  kule nchini Mexico, ambako aliwaona watu waliovaa suti nyeusi wakiingia chumbani kwa Ramona, alianza kuhisi labda kuna biashara ya siri anayoifanya mrembo huyo.

Baada ya kulifikiria sana jambo hilo, aliamua kuachana nalo, kwa kuwa undani na uhakika wa maisha ya Ramona hakuufahamu vizuri. Yeye alichokiangalia ni mapenzi.

“Hata kama Ramona amekasirika mimi kuja hapa, siwezi kuacha kumwambia jambo lilonileta. Nitamwambia kwamba, Sikuyafuata maisha na biashara zake, bali nimeyafuata mapenzi,” alijisemea Roika.

Muda ulizidi kwenda wakati Roika akiumiza kichwa pale bustanini.  aliongea peke yake kama mtu aliyechanganyikiwa, hakuona umuhimu wa kuyafuatalia maisha ya Ramona, kwa kuwa hilo si alilolijiia Pakistani. Mengine yote yanayohusu maisha ya Ramona hayakuwa sehemu ya safari yake, alichofikiria yeye ni mapenzi yake kwa mrembo huyo wa dunia.

Yakiwa tayari yamepita masaa mawili, Roika aliamua kuondoka pale bustanini na kurudi ndani ya hoteli. Eneo hilo la wazi, ndani ya hoteli, lilikuwa na watu wengi wanaoingia huku na kule wanaopanda lifti na wanao shuka. Wakati akiisubiri lifti pamoja na watu wengine, alitazama juu na kuona lifti ikitoka gholofa za juu. Na ilipofika gholofa ya tatu, baadhi ya watu walishuka na wengine kupanda. Miongoni mwa watu waliopanda ni wale watu watano aliokuwa amepishana nao muda ule wakati yeye anatoka gholofa ya tatu alikokuwa chumbani kwa Ramona. Roika alitoa macho kuwatazama, akiamini kabisa watu hao walikuwa ni wageni wa Ramona.

Alipishana nao tena wakati yeye anaingia kwenye lifti na wenyewe wanashuka, ambapo walielekea eneo la maegesho ya magari. Wakati lifti ikipanda juu, yeye alikuwa anawaona kwa chini .

Baadhi ya watu aliokuwa nao kwenye lifti, walibonyeza vitufe namba mbili, namba tatu na tano, huku yeye akibonyeza kitufe namba nne, akiashilia kuwa anakwenda gholofa ya nne ambako ndiko kuna chumba chake. Hakuwa na nguvu ya kumfuata tena Ramona kwa siku hiyo, kwa kuwa aliogopa sana. Alipanga kumfuta kesho ili kumueleza nia yake ya kumfuata Pakistani.

Alishuka gholofa ya nne na kuingia chumbani kwake, ambapo aliwapigia simu wahudumu wa hoteli akiwaambia kuwa anahitaji chakula. Hazikupita dakika kumi muhudumu alimgongea mlango, alisimama kwenye kiti na kwenda  kufungua. Muhudumu aliyekuja kumletea chakula ndiye yule  aliyekuwa amemuonesha chumba cha Ramona. Aliyekuwa amemuomba ampelekee yeye chakula.

“Kaka kumbe uko huku?” aliuliza muhudumu huyo.

“Ndio karibu sana,” Roika alijibu.

Aliingia na chakula na kukiweka mezani akakipanga vizuri, baada ya hapo alimgeukia Roika na kumuuliza.

“Ulimfanyia saplaizi rafiki yako?”

“Ndio, alifurahi sana.”

“Kaka samahani, hivi ni kweli yule mrembo ni rafiki yako au mpenzi wako.”

“Kwani mwanzo nilikwambia ni nani yangu?”

“Rafiki yako.”

“Huo ndio ukweli.”

“Mhh! Hivi inawezekana kweli mtu ukawa na nguvu ya kumfanya mwanamke mzuri kama yule kuwa rafiki yako?”

“Kwanini isiwezekane?”

“Mimi siwezi.”

“Mimi nimeweza ndio maana hadi sasa ni rafiki yangu wala hakuna mapenzi kati yetu.”

“Kama umeweza hilo kaka, basi wewe ni watofauti sana. Hata hivyo urafiki wenu  sidhani kama utafika mbali. Mimi ninaamni hivyo,” aliongea muhudumu huyo aliyekuwa amemchangamsha kidogo Roika.

Maneno hayo ya muhudumu, yalimuumiza sana Roika, kwa kuwa ulikuwa  ni ukweli mtupu. Baadae muhudumu huyo alimuaga Roika na kutoka. Roika alielekea mezani kupata chakula ikiwa ni saa tisa kasoro alasiri.

Ramona alikuwa amechoka kwa kiasi fulani baada ya kumaliza kikao kirefu na wageni wake. Baada ya wageni kuondoka akili yake yote aliihamishia kwa Roika. Aliumia sana kwa kitendo chake cha kuonyesha hasira mbele ya rafiki yake. Japo ni kweli Roika alikuwa amefanya kosa, kosa la kuja bila taarifa au kumfuata pasipo idhini yake, lakini aliona haikuwa sababu ya yeye kumkasirikia na kumtolea maneno ya juu.

“Nisamehe Roika. Usalama wa kazi yangu ndio umenifanya niukasirikie ujio wako,” alijisemea Ramona.

Alipanga kumtafuta Roika haraka iwezekanavyo, ili wakae na kuzungumza, ikiwezekana amuombe msamaha kwa kumkasirikia. Kwa kuwa hakujua chumba anachoishi Roika, aliinua simu yake ya mkononi na kutaka kumpigia ili kumuuliza. Lakini alisita kufanya hivyo. Wakati akitafakari jambo hilo mlango wake uligongwa. Alimruhusu anaegonga kuingia. Muhudumu wa hoteli aliingia mle ndani. Muhudumu mwenyewe ni yule aliyekuwa ametoka kuongea na Roika muda mfupi uliopita. Alikuja chumbani kwake kwa nia ya kutoa vyombo vya chakula.

“Madamu mbona hujala chakula?” aliuliza muhudumu huyo.

“Sijisikii vizuri, ila niachie nyama na mayai hivyo vingine vitoe. Je unaweza pia ukaniletea na Pandora?” alijibu Ramona na kuuliza kwa unyonge sana.

“Sawa madamu usijali.”

“Halafu naomba nikuulize swali.”

“Uliza tu madamu.”

“Sijui unaweza ukamfahamu mteja wanu anayeitwa Roika Malino?”

“Roika Malino?”

“Ndio.”

Muhudumu alivuta kumbukumbu ya jina hilo, ambapo alimkumbuka mtu aliyetoka kuongea naye gholofa ya nne, ndio mtu anayeitwa Roika. Kwa kuwa siku ile aliyoomba kumpelekea chakula mteja wao Ramona, alikuwa amejitambulisha kwa jina hilo.

“Ndio ndio namfahamu,” alijibu muhudumu.

“Unaweza kuniambia atakuwa gholofa ya ngapi na chumba namba ngapi?”

“Yuko gholofa ya nne chumba namba tisa.”

“Sawa nashukuru kwa kunifahamisha.”

“Sawa madamu.”

Mudumu wa hoteli alitoka na kwenda kumletea Ramona kinywaji cha Pandora wine.

Ilipofika saa moja jioni, Ramona alitoka chumbani kwake. Akaelekea kwenye lifti, baada ya kuingia alibonyeza kitufe namba nne. Alishuka gholofa ya nne na kuelekea chumba namba tisa. Aliufikia mlango wa chumba cha Roika na kugonga. Roika akiwa mwenye mawazo, juu ya kiumbe anayempenda, alikuwa akitafakari ni njia gani nyingine aitumie kumfuata Ramona  ili kumueleza jambo moja tu kuwa anampenda. Akiwa kwenye uamuzi wake wa mwisho, alisikia mlango ukigongwa. Aliinuka kwenye kiti na kwenda kufungua.

Kabla macho yake hayajaona, pua yake ilishatambua kwanza, kuwa aliyekuwa amesimama mbele yake ni nani. Marashi ya siku zote aliyopenda kuyatumia mrembo huyo wa dunia, yalikuwa ni kitambulisho kikubwa kwenye hisia za Roika. Baadae macho yake yalifuata zamu yake, pale yalipomuona Ramona akiwa amesimama mlangoni, akimtazama kwa unyonge mkubwa.

Roika alipigwa na butwaa, akabaki kumtazama Ramona kwa sekunde 90 za ukimya, asiamini mtu ampendaye amekuja. Hakutegemea kama Ramona atamfuata yeye, wazo hilo hakuwa nalo kabisa. Kwa jinsi Ramona alivyokuwa amekasirika vile, ilikuwa ni ngumu kuamini kama ndio yule anayemuona pale mlangoni.

“Karibu Ramona karibu sana,” kwa uoga na aibu Roika aliongea.

Ramona hakujibu lolote lile, zaidi alipitiliza ndani, ambapo alielekea moja kwa moja mezani. Akaichukua chupa ya Alamosi na kumimina kinywaji kwenye glasi, akainywa yote na kisha  akamgeukia Roika. Macho yake mazuri, yalimtazama Roika aliyekuwa amesimama kama mtu aliyenyeshewa na mvua. Ukimya ulitawala kwa dakika mbili wakiwa wanatazamana. Baadae Ramona aliongea.

“Roika nisamehe sana, najua nimekuumiza. Sikupaswa kuwa na hasira kiasi kile hata kama umeniudhi. Ujio wako sikuutegemea kabisa ndio maana nikapandwa na hasira, hata hivyo ilitakiwa nikuelewe rafiki yangu.”

Kwa huzuni kubwa na moyo uliopinga siku zote kuitwa rafiki, Roika alimsogelea Ramona kwa uwoga mkubwa akihema kwa siri.

“Hupaswi kusema hivyo, kwa kuwa nilistahili hata kuadhibiwa. Kukufuata na kuja kwako bila taarifa, wala idhini yako, ni makosa. Hivyo mimi ndio ninapaswa kukuomba wewe msamaha. Nisamehe sana.”

“Roika tuache kwanza kuzungumzia ujio wako, tuzungumzie msamaha. Nina hakika utanisamehe nami nimekusamehe.”

“Asante Ramona.”

“Asante Roika.”

Ramona alimsogelea Roika na kumkumbatia. Kitendo hicho kilimfanya Roika kujihisi yuko dunia ya tatu, mwili wake ulitetemeka, akihisi nguvu za kuongea chochote kwa Ramona zikimjia haraka. Wakati kifua cha Roika kikiwa kimegusana na kifua cha Ramona, kifua chenye chuchu zilizosimama, Ramona alimwambia Roika.

“Wewe ni rafiki yangu pekee ambaye nimetokea kukupenda kati ya marafiki zangu wote. Ni rafiki wa tofauti sana.”

Maneno hayo, yalikuwa ni mwiba sana kwa Roika, aliyezidi kuumia vikali kupita kawaida. Maumivu yake yalikuwa ni zaidi ya yule mtu aliyepigwa risasi ya mbavu. Baadae, Ramona alijitoa kwa Roika, lakini alishangaa kuona Roika amekosa furaha, zaidi ya mara ya kwanza, huku yeye akiwa mwenye tabasamu. Alikunja ndita kidogo na kuuliza.

“Nini tena mbona hauna furaha au bado hauja nisamehe?”

Roika hakujibu chochote, alibaki kimya kwa sekunde kadhaa kitendo kichozidi kumshtua Ramona. Baadae kwa moyo wa ujasiri moyo uliomfanya kusafiri kutoka Mexico kwenda Haiti na baadae kutoka Haiti kuja Pakistani, ulimtuma kumwambia Ramona kile alichokuwa amekijia Pakistani.

“Ramona nakupenda sana, naomba uje kuwa mke wangu.”

Nini kitafutia? Usikose jumatatu    

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -