Friday, December 4, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

Ilipoishia jana

JIJINI CAIRO

Roika alikuwa amekwisha shuka jijini Cairo nchini Misri, akiwa anatokea Tanzania, alikokwenda kumuomba mama yake damu, damu itakayomuinua tena Shazayi binti wa Rais asipatwe na umauti.

SASA ENDELEA

Sasa alikuwa anakata tiketi ya ndege ya kuelekea nchini Pakistan. Hiyo ikiwa ni siku ya pili na masaa kadhaa, tokea alipoondoka Pakistan na kuelekea Tanzania na baadae kufika Misri.

Baada ya dakika 20, Roika alikuwa ndani ya ndege, iliyokuwa inalitafuta anga la Islamabad ndani ya Pakistan.

HOSPITALI YA MOHAMED WORDS

Wasiwasi na hofu aliyokuwa nayo daktari, daktari mkuu wa hospitali ya Mohamed Words, uliwafanya polisi kuwahoji wauguzi na madaktari wote na kuanza kuikagua hospitali hiyo. Sumu ambayo daktari alikuwa amewapa wauguzi wake, ilikuwa ni sumu kali ya kutosema jambo lolote linalomhusu Shazayi. Kabla polisi hawajaja hospitalini hapo, daktari alishakuwa amewaonya wauguzi wote, kuwa endapo watasema jambo lolote linalomhusu Shazayi na mtu aitwaye Roika, basi hospitali nzima itakutwa na hatia ya kusababisha kifo cha binti wa Rais, hivyo wauguzi na madaktari wote watanyongwa au kwenda jela.

Hivyo wauguzi na maktari wote waliapa kutosema lolote linalomuhusu madam Shazayi. Kwani nao walihofia kukutwa na hatia.

Baada ya polisi kuwahoji wauguzi na madkari na kutopata ukweli halisi wa mahali alipo Shazayi, walianza kuingia chumba baada ya chumba kumtafuta Shazayi. Hatua ya kwanza ilikuwa ni kwenda mochwari kumtafuta kwenye masanduku ya maiti ili kujua kama binti huyo wa Rais alikuwa amekwisha kufa na kufichwa huko.

Ingawa ilikuwa ni ngumu kuamini kuwa hospitali hiyo inahusika kwa namna moja au nyingine ya kupotea kwa mtoto wa Rais, lakini polisi waliona hawana sehemu nyingine ya kumtafutia Shazayi isipokuwa hospitalini hapo.

Daktari alijua kabisa kuwa lazima wataingia kwenye mikono ya polisi kwa kuwa Shazayi alimficha sehemu ambayo inaweza kugundulika mara moja. Alianza kumuomba Allah amtetee na kama atashindwa kumtetea, basi ailinde familia yake.

Askari waliendelea kukagua chumba baada ya chumba, wodi baada ya wodi. Lakini hawakumuona Shazayi.

Askari mmoja alielekea kwenye chumba kimoja kilichokuwa ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi ICU, chumba ambacho daktari, alikuwa amemficha Shazayi. Akafunua pazia na kuuona mwili wa mtu kwa mbali ukiwa juu ya kitanda, huku ukiwa na mashine ya kusaidia kupumua. Alipiga hatua kwenda kuusogelea, ili kujua kama mwili huo ni wa Shazayi. Akiwa anaukaribia, saa yake ya mkononi ilitoa mlio fulani na kuwaka taa nyekundu. Ishara hiyo ilimaanisha kuwa kuna jambo lingine la hatari au taarifa inatolewa kwa askari wote. Aliamua kuacha kuufuata ule mwili, mwili uliokuwa kweli wa Shazayi, binti Halim na kuamua kurudi kwa wenzake. Alipofika katikati ya hospitali aliwakuta wenzake, wakiwa wamekusanyika pamoja.

“Jamani kuna nini, mmekwisha kugundua mahali Shazayi alipo?” aliuliza askari huyo.

“Hapana, polisi wote tunajulishwa kuwa kuna mlipuko umetokea katika daraja la Zuana. Hivyo wote tunaombwa kufika huko mara moja.” Alijibu kiongozi wao.

“Sasa vipi kuhusu binti wa muheshimiwa?”

“Tuachane kwanza na hilo la binti, tutarudi wakati mwingine.”

Baada ya maongezi hayo, polisi wote waliingia kwenye magari yao na kuondoka hospitalini hapo. Haraka daktari alikimbia kuelekea kwenye chumba alichokuwa amemficha Shazayi. Alimkuta Shazayi akiendelea kuhema kwa tabu. Kwanza alipiga magoti na kusujudu mara tano. Akimshukuru Mungu kwa kuweza kumnusuru asishikwe na mikono ya serikali.

Siku hiyo hiyo vyombo vya habari vilianza kuripoti fununu za kupotea kwa mtoto wa Rais. Kamishina mkuu wa idara ya polisi, alistushwa na jambo hilo. Alishangazwa na taarifa hizo ngeni zilizokuwa zinakwenda kulichafua jeshi la polisi, jeshi lililopewa jukumu la kumlinda binti wa Rais.

Ule mlipuko uliokuwa umetokea muda ule wakati polisi wakiikagua hospitali ya Mohamed Words, ulikuwa ni wa mtu mmoja aliyejitoa muhanga katikati ya daraja, ambaye hakujulikana ni wa kikundi gani cha kigaidi. Hata hivyo mtu huyo hakuleta madhara makubwa, kwani watu watatu pekee ndio walipoteza maisha na 15 kujeruhiwa.

Kamishina wa polisi aliwaita haraka askari wa idara ya ulinzi wanaoshughulikia usalama wa binti wa Rais. Aliwahoji kwa ukali kuhusu uzembe walioufanya uliosabisha mtoto wa Rais kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Polisi wanaohusika na ulinzi na usalama, pamoja na msafara wa Shazayi, walikuwa matatani.

Taarifa hizo zilimfikia Rais wa nchi. mheshimiwa Galim Halim kuwa mwanawe hajaonekana kwa siku mbili na masaa kadhaa. Hakika alichanganyikiwa, mama yake na Shazayi mke wa Rais, alilia kilio kikubwa. Alimpa mumewe siku mbili za kumletea binti yake la sivyo anakwenda kujiua.

RAMONA

Ndege ya shirika la Qatar Airways ilikuwa inatua uwanja wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. Ramona alishuka akiwa pamoja na walinzi wake watano. Alikuwa na moyo ule ule moyo wa ajabu uliotaka kwenda kumwambia mama yake na Roika juu ya kilichompata mwanawe na kumuomba msamaha.

Nini kitafuatia? usikose kesho

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -