Wednesday, November 25, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Ilipoishia Jumamosi

Ikionyesha kuwa polisi hao walikuwa wakihenya kila mahali kumtafuta mtoto wa rais

SASA ENDELEA

SURA nzuri ya Shazayi ilianza kubadilika na kuwa kama sura ya maiti, mtu aliyekufa dakika tano zilizopita. Lakini mapigo ya moyo wake bado yalionyesha kuwa yanashindana na mwili. Moyo wake ulikuwa unadunda kila baada ya sekunde kumi.

Dk. Sufian aliamini kuwa Shazayi hawezi kupona. Alianza kumuomba Mungu amsaidie kuilinda familia yake, pindi atakapokuwa kaburini, kwani kwa kesi kama hiyo, aliamini sheria itamuhukumu adhabu ya kifo. Hasa uzito wa hukumu hiyo, utajazwa na suala la kwamba Shazayi ni mtoto wa Rais. Kwani mahakama itamhoji kwanini alikubali kumtoa Shazayi damu, ikiwa anajua wazi kuwa kiwango cha damu atakachomtoa kitampelekea binti huyo kufa? Hakika alibaki yeye na Mungu wake wala hakuufikiria kabisa ukombozi kutoka kwa Roika.

Baada ya mwendo wa dakika 20 Roika akiwa ndani ya taksi, walikuwa wanaingia mtaa ulikokuwa na kizuizi cha polisi. Polisi walilisimamisha gari lao na kuwaamuru wote washuke. Roika na dereva walishuka. Askari walianza kulikagua gari lao. Baada ya kulikagua, waliwahoji maswali matano. Kwa wakati huo Roika alikuwa katika wakati mgumu, akimfikiria Shazayi. Aliamini kuwa kwa mtindo huo wa kuhojiwa na polisi, lazima atachelewa kufika hospitalini.

Baada ya polisi kuridhika nao, waliwaruhusu waende. Dereva aliwasha gari na kuliondoa pale taratibu, lakini alivyowaacha polisi mbali, aliongeza mwendo, akikimbiza gari  kupita kawaida.

Muda ambao Dk Sufian alikuwa akiamini kuwa Shazayi anakwenda kufa, ndio muda ambao Roika  alikuwa akiamini kuwa anakwenda kumkuta tayari Shazayi  amekwisha ondoka katika dunia hii. Dereva alijitahidi kupita barabara zisizokuwa na vizuizi ili aweze kuwakwepa polisi, lakini juhudi zake hazikuweza kufanikiwa. Bado polisi waliwasimamisha mara kwa mara.

Baada ya nusu saa, Roika hakuwa na haja tena ya kuingalia saa yake ya mkononi. Kwani tayari polisi walikuwa wamekwisha wasimamisha zaidi ya mara saba. Na kwa wakati huo ilikuwa tayari imekwisha kutimu saa 4:30. Hata dereva alijua kuwa tayari alikuwa amekwishazikosa zile dola 300 alizoahidiwa na Roika, endapo atakuwa amewahi kumfikisha hospitalini, kabla ya saa tano. Mwendo wa saa moja na dakika kadhaa ulikuwa umesalia kufika mji wa Alamayana. Roika alishakuwa amekataa tamaa ya kumuwahi Shazayi. Alibaki kulia pekee yake, asiamini safari yote aliyoifanya ya kwenda Tanzania kwa mama yake, kwa ajili ya kuichukua damu, ilikuwa safari isiyo na faida. Alibaki kumtegemea Mungu tu. Kwani alijiuliza hivi inawezekana vipi hadi kufikia muda huo Shazayi awe bado anaishi, aliona ni jambo lisilowezekana.

Tayari walikuwa wamekwishaingia mji wa Alamayana. Polisi wanaofanya dolia kwenye barabara ya kuelekea Nulhamik, Almita na daraja la Zuana, waliwasimamisha na kuanza kuwahoji maswali. Muda ulizidi kwenda, saa sita ilikuwa inakaribia. Dakika 15 zilikuwa zimebaki ili iweze kutimu 6:00. Saa sita ndio muda utaokaokuwa umezikamilisha zile siku tatu, ambazo daktari alikuwa amemwambia Roika kuwa ndio siku ambazo, Shazayi atakuwa amezimaliza kuishi duniani.

Roika alikuwa hana uhuru wa kujieleza sana mbele ya polisi, kwa sababu hakujua kama vyombo vya dola vilikuwa vinamsaka au vilipata fununu fulani kama alikuwa pamoja na mtoto wa Rais. Hivyo alijibu maswali yao kwa tahadhari na uwoga mkubwa. Mara nyingine alimwachia dereva awajibu polisi kile anachokijua yeye. Zaidi polisi walipomuhoji yeye, aliwajibu kuwa yeye ni mgeni hajui chochote kinachoendelea kwenye nchi yao. Baada ya polisi hao kuwahoji kwa muda wa dakika 17 waliwaruhusu waende.

Polisi wote walikuwa na maswali mengi, lakini swali lao kuu lilikuwa ni kuhusu kupotea kwa mtoto wa Rais.

Waliondoka lile eneo na kuelekea barabara ya Almita ambako huko kuna barabara ya kwenda Hospitali ya Mohamed Words. Baada ya dakika 10 walifika katika kizuizi cha polisi. Kizuizi hicho, ndio kile kizuizi cha wale polisi waliokuwa wamemsimamisha Shazayi siku ile, pindi alipokuwa anamuwahisha Roika hospitalini. Polisi hao walipowasimamisha, waliwataka kushuka. Roika na dereva wake walishuka na kuanza kujibu maswali. Lakini jeuri ya polisi hao, iliwafanya wakae pale kwa muda wa dakika 45. Na tayari kwa muda huo ilikuwa imekwisha timu saa 7: 15 usiku. Tayari Roika alikuwa amekwisha kata tamaa, akijua kuwa tayari kipenzi chake amekwisha iaga dunia. Ile ahadi aliyokuwa amemuahidi mama yake, kuwa angemletea mkwe wake, alianza kuijutia. Alijiuliza ni mwanamke gani mwingine ambaye atakuwa na hamu ya kumuoa endapo Shazayi akuwa amekwisha kufa. Alipomfikiria Ramona moyo wake ulishtuka, uliumia kupita kiasi. Nafsi yake ilimuomba Roika asimfikirie mwanamke huyo, kwani inateseka sana.

Baada ya dakika 45 kupita, polisi waliwaruhusu waende. Dereva alivyofika mbele kabisa, aliongeza mwendo wa gari. Lakini Roika alimwambia atembee taratibu, kwani tayari alikuwa amekwisha chelewa.

“Nisamehe kaka kwa kushindwa kukufikisha muda uliokuwa umeupanga,” aliongea dereva.

“Usijali si kosa lako,” alijibu Roika kwa unyonge mkubwa.

Ikiwa ni saa nane kasoro usiku Roika alikuwa anaingia Hospitali ya Mohamed Words.

Nini kitafuatia, usikose kesho            

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -