Sunday, January 17, 2021

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

Ilipoishia jana

MACHO yalimtoka mama Roika pindi alipomuona mrembo wa dunia Ramona Fika pale sebuleni. Upesi kichwa chake kilifikiria kwa haraka mambo mengi aliyosimuliwa na mwanaye, kuhusu mrembo huyo na kilichompata Pakistani. Alijiuliza ni nini kilikuwa kimemleta pale nyumbani kwao. Alianza kujawa na woga kwa sababu alimfahamu Ramona kuwa ni mtu hatari. Macho ya Ramona yalimtazama mama Roika kwa woga mkubwa, lakini nafsi yake ilikuwa ikimwambia mara kwa mara kuwa liwalo na liwe. Dina aliyekuwa ameketi pale sebuleni, alishangazwa na tukio la wawili hao kuonana.

SASA ENDELEA

Kwa heshima Ramona alisimama kwenye kiti, akimsubiria mama Roika aliyekuwa amesimama baada ya kusita pindi alipopigwa na bumbuwazi. Taratibu mama Roika alipiga hatua huku akijipa roho ya ujasiri. Ramona naye alipiga hatua kumsogelea kabla hajamfikia. Kwa wakati huo kila mmoja alikuwa na busara yake aliyopanga kuionyesha kwa mwenzie.

“Shkamoo mama,” Ramona alisalimia kwa salamu ya kitanzania.

“Marhaba hujambo mwanangu,” alijibu mama Roika akionyesha mtu asiye na shaka. Ingawa moyoni mwake, alikuwa akijuliza ni nini kilikuwa kimemleta Ramona nyumbani kwake.

“Sijambo mama.”

“Karibu uketi.”

“Asante mama.”

Ramona alikaa kwa uwoga mkubwa. Baada ya kukaa, alianza kutokwa na machozi, machozi aliyoshindwa kuyazuia. Dina alishangazwa na kitendo cha mgeni kutokwa na machozi kwa kuwa hakuwa akielewa kitu. Lakini mama Roika alikuwa akijua ni nini kilichokuwa kikimliza mrembo huyo. Ingawa bado hakuwa amelijua lengo la mwanamke huyo kuja nyumbani kwake.  Wakati Ramona akifuta machozi, mama Roika alimtazama mwanaye Dina na kumwambia.

“Dina nenda chumbani kwako mimi ninamaongezi na mgeni.”

Dina alishangaa, alimtazama mama yake kwa mtazamao wa kuhoji. Baadae aliinuka kwenda chumbani kwake kwa shingo upande. Maana hata yeye alitaka kujua nini kimemleta mrembo huyo wa dunia nyumbani kwao. Lakini baadae mama Roika alijifikiria, akamuua kumuita tena Dina. Dina alipokuja mama yake alimuuliza.

“Si ulisema gari yako haina mafuta?”

“Ndio mama.”

“Chukua gari yangu uwende sokoni, ukanunue mchele si unajua ndani umekwisha?”

“Lakini mama na mimi nilitaka kufahamiana na mgeni, si nikirudi atakuwa amekwisha ondoka?” aliongea Dina akiwa amenuna.

“Usijali mwanangu, ukirudi utamuona, sawa, wala haondoki.”

Dina alitoka tena kwa shingo upande, akaelekea kabatini ambapo alichukua funguo za gari na kutoka mle ndani. Lakini Ramona alishangazwa na kitendo cha mama Roika kumtoa binti yake.

Baada ya Dina kuelekea nje, mama Roika alimgeukia Ramona aliyekuwa akitokwa na machozi

“Mwanangu mbona unalia kuna tatizo?”

Ramona hakulijibu swali hilo, zaidi alimfuata mama Roika na kukaa chini mbele yake, safari hii kilio chake kilikuwa ni kikubwa zaidi. Baadae alianza kujieleza akimsimulia jinsi alivyokutana na Roika , namna walivyoanza mahusiano yao na kile kilichompata mwanaye, ndani ya jumba lao la biashara. Wakati Ramona akimsimulia hayo, mama Roika alikuwa akitokwa na machozi mengi. Baadae alilia sana,.

Kwa kuwa mama Roika alishakuwa ameyafahamu yote hayo, kilio chake kilikuwa kimegawanyika mara mbili. Kwanza alilia kwa sababu, alikuwa amekumbushwa machungu ya matatizo, matatizo yaliompata mwanaye na pili alilia kama maigizo ili Ramona asijue chochote kilichokuwa kikiendelea. Kwani mama Roika alifahamu kuwa mwanaye ni mzima, ingawa kweli alikuwa amepatwa na mikasa hiyo.

Mama Roika hakuhitaji kumwambia Ramona kuwa Roika anaishi. Hivyo kwa upande mwingine alijidai analia ili Ramona asijue jambo lolote. Mama Roika alijidai kuwa, taarifa za kifo cha mtoto wake  alikuwa anazisikia kwa mara ya kwanza. Aliendelea kulia sana huku akiongea maneno yaliozidi kumuumiza Ramona.

“Mwanangu umeniulia mtoto wangu. Nitaishi vipi bila Roika wangu. Kwa nini lakini?”

“Mama nisamehe mama sikufiria kufanya hivyo, najutia dhambi yangu,” aliongea Ramona huku akiwa ameishika miguu ya mama Roika, akilia kupita kiasi.”

Kilio kikubwa kilikuwa kimetawala mle ndani, kila mmoja aliendelea kulia. Lakini kilio cha mama Roika kilikuwa ni kilio cha kuigiza kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa akifahamu kuwa mwanaye yuko wapi na anafanya nini kwa muda huo. Lakini kilio cha Ramona kilikuwa ni zaidi ya kilio cha kusaga meno. Maana yeye hadi kufikia muda huo, alikuwa akijua kuwa mpenzi wake yuko kaburini.

Nini kitafuatia? usikose kesho

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -