Tuesday, January 19, 2021

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

Ilipoishia jana

PAKISTANI

BIYANAH mwanamke bilionea alikuwa kwenye wakati mgumu usiolezeka. Maisha yake yalianza kumtofautisha yeye na utajiri aliokuwa nao. Kwani alikuwa analia kila siku. Hakujua hadi muda huo Roika alikuwa amekwenda wapi. Aliamua kuongea na uongozi wa hoteli ya Alashak  ambapo walikaa na kuulizana kuhusu mahali alipo kijana huyo.

SASA ENDELEA

Biyanah aliutaka uongozi wa hoteli utoe taarifa polisi kuhusu kupotea kwa mpenzi wake mara moja. Kwani ni wiki zaidi ya tatu alikuwa hajapata kumuona.

Muda haukupita uongozi wa hoteli ulipiga simu polisi na kutoa taarifa kuhusu kupotea kwa mteja wao. Taarifa hiyo pia ilisimuliwa na Biyanah kituo cha polisi. Lakini Biyanah hakutaka kuwaambia polisi kuhusu mtu anayemshuku kuwa amehusika na kupotea kwa Roika ambaye ni Ramona. Kwani alihitaji yeye mwenyewe aweze kumalizana na adui yake ambaye ni Ramona.

Sasa alipanga kumhoji Ramona kwa mara ya mwisho juu ya mahali alipo mpenzi wake. Roho yake iliyokuwa inatambua mapenzi kuliko urafiki wao wa zamani, ilikuwa inapanga kumfanyia Ramona kitu kibaya.  Kwani Biyanah aliamini muda wote kuwa, mtu ananayehusika na kupotea kwa mpenzi wake ni Ramona.

HOSPITALINI

Masaa yalizidi kusogea pindi binti wa Rais alipozidi kupata auheni. Roika hakutoka pembeni ya kitanda. Muda wote macho yake hayakuacha kumtazama  Shazayi.

Tayari mstari wa kijani ulikuwa umefika kwenye duara la kijani. Iliamanisha  kuwa muda wowote Shazayi ataweza kufumbua macho. Fuaraha ya Roika ilizidi kuwa kubwa pindi apozidi kuona hali zuri inayoendelea kuonekana kwa Shazayi.

Wakati huo serikali ya Pakistani iliendelea kuhangaika, ikifanya kila njia iweze kumtoa binti wa Raisi, katika mikono ya kikundi hatari cha kigaidi kikundi cha Swaba, kikundi kilichodai kuwa, kinahusika na kupotea kwa mtoto wa Rais. Hivyo kilihitaji pesa na umiliki wa eneo la Ramadan Kash ili kiweze kumuachia Shazayi.

Lakini ukweli ni kwamba, kikundi hicho hakikuwa kimemteka Shazayi kama madai yao yalivyosema. Polisi walikuwa wameacha kufanya upelelezi wao katika hospitali ya Mohamed Words, kwani kikundi kilichomteka binti huyo kilikuwa kimejitangaza.

Viongozi mbalimbali wa Pakistani wakiwamo mawaziri, walisema kuwa haitawezekana kuwapa pesa nyingi kiasi hicho na kuwapa eneo la Ramadan Kash kikundi hicho. Kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wameingia kwenye hasara kubwa, kiuchumi na kiulinzi na watakuwa wamekiinua kikundi hicho kwa kiwango kikubwa, kikundi kinachotishia amani ya nchi na dunia kwa ujumla. Hivyo viongozi hao, waliitaka serikali, pamoja na Rais wao kutumia njia nyingine ya kumtoa binti huyo kwenye mikono ya magaidi hao na si kuwapa kile walichokitaka.

Mama yake Shazayi mke wa Rais alimtaka mumewe, kuwapa vitu hivyo kwani watamkosa binti yao.

Kiongozi wa kikundi cha Swaba Zahil Bin Shaq alisema, kama hawatekeleza agizo hilo, kufikia mwezi ujao, watatoa mkanda wa video utakaonyesha jinsi binti huyo, anavyotenganishwa kichwa na kiwiliwili.

Roika akiwa hospitalini, alishangazwa na taarifa hiyo ya uongo ya kikundi hicho. Alimtazama Shazayi aliyekuwa amelala kisha akacheka.

Ikiwa ni siku ya tatu tokea Shazayi alipoongezewa damu, Roika alikuwa amekilaza kichwa chake kwenye mapaja yake. Mwili wake ulishtuka na kusisimka, baada ya kuguswa. Alipogeuka kuona ni nani alikuwa amemgusa, aliukuta mkono wa Shazayi ukiwa kichwani kwake. Haraka aliinua kichwa chake na kumtazama Shazayi usoni. Hakuyaamini macho yake baada ya kumuona Shazayi akiwa amefumbua macho.

Moyo wake ulimdunda zaidi ya ngoma, mwili wake ulitetemeka. Taratibu alianza kuusogeza uso wake kuelekea kwa Shazayi. Hakika ilikuwa ni siku ya muujiza. Shazayi alikuwa anamtazama Roika kwa tabasamu zuri ajabu. Macho yake mazuri mithili ya malaika mtoto, yalikuwa yakitokwa na machozi. Hakika Shazayi aliionekana ni mwanamke mzuri kama mtu aliyetokwa kuzaliwa upya.

Nini kitafuatia? Usikose Alhamisi

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -