Wednesday, October 28, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

Ilipoishia jana

Akiwa anapanda ngazi mpiganaji mmoja wa kikundi cha Swaba alimwita na kumwomba waongee. Mpiganaji huyo ndiye yule aliyekuwa ametumwa akauchome moto mwili wa Roika.

SASA ENDELEA

Siku ile baada ya Ramona kumpiga risasi Roika, kiongozi wa kikundi cha Swaba, Zahil Bin Shaq, alikuwa amemwagiza mpiganaji wake aende akauchome moto mwili wa Roika. Lakini hakufanikiwa kwa sababu mwili wa Roika ulichukuliwa na mtoto wa Rais, Shazayi binti Galim.

Ilikuwa wakati anataka kuuchoma moto mwili huo, aligundua kuwa alikuwa amekisahau kiberiti na pia hakuwa na silaha yoyote. Hivyo aliamua kurudi  haraka kwenye jumba lao ili akakichukue na aliporudi hakuuona mwili wa Roika.

Ilibidi arudi bila kutekeleza agizo la kiongozi wake. Aliamua kufanya siri, hakutaka kumweleza Zahil Bin Shaq kuwa mwili wa Roika umechukuliwa. Aliogopa kusema jambo hilo, akihofia kupewa adhabu kali kutokana na uzembe aliokuwa ameufanya. Suala la kuwa mwili wa Roika umechukuliwa na mtu asiyejulikana, ilibaki kuwa siri yake.

Mpiganaji huyo aliamua kumwita Ramona na kumweleza siri hiyo kwa kuwa siku zote alikuwa akimuona mrembo huyo akiwa hana furaha kutokana na kumuua mpenzi wake.

“Samahani madamu tunaweza kuongea wawili kwa dakika chache?” Aliuliza mpiganaji huyo pindi Ramona alipokuwa akipanda ngazi kuelekea juu.

“Samahani sina muda kwa sasa labda kesho,” alijibu Ramona.

“Ni jambo muhimu madam ni vema lisingoje kesho.”

Ramona aliposikia hivyo, alimtazama mpiganaji huyo kwa dakika mbili za ukimya na kisha akamjibu.

“Sawa utanikuta chumbani kwangu, nifuate baada ya dakika tano,” alijibu Ramona.

Baada ya dakika saba, mpiganaji huyo alimfuata Ramona chumbani kwake.

“Karibu uketi,” aliongea Ramona.

“Asante madam,” alijibu mpiganaji huyo huku akikivuta kiti.

Baada ya kukaa, alimtazama Ramona na kisha akamwambia.

“Mimi ndiye niliyetumwa nikauchome moto mwili wa Mr Roika.”

Ramona alishtuka, alibaki ameduwaa kwa sekunde kadhaa. Baadaye alimjibu kwa shauku na umakini mkubwa.

“Uliuchomea wapi, twende ukanioneshe  nataka kuyachukua majivu tafadhali.”

“Sikufanikiwa kuuchoma,” mpiganaji alijibu.

“Hukufanikiwa?”

“Ndio!”

“Una maana gani kusema hukufanikiwa?”

“Nilipofika eneo la kuuchomea, niligundua nimesahau kiberiti. Ikabidi nirudi hapa maskani yetu kuja kukichukua. Na niliporudia eneo lile, mwili wa Mr Roika sikuuona.”

“Whaaat! Haukuuona?” Ramona alipatwa na mshangao mkubwa.

“Ndio sikuuona. Inaonyesha kuna mtu aliubeba.”

“Kuna mtu aliubeba?”

“Ndio.”

“Ni nani aliyeubeba?”

“Kwa kweli sifahamu.”

“Uko makini kunieleza jambo hili kweli?” Ramona aliuliza.

“Hakika madamu, nachokuambia ndio ukweli uliopata kutokea siku ile. Kwa siku zote hizi ilibaki kuwa siri yangu. Hata kiongozi Zahil, sijamwambia, maana nikimwambia, katu hatanielewa.”

Hakika taarifa hiyo ilikuwa imemshtua mrembo Ramona. Hakuamini kwa urahisi kile alichokuwa ameambiwa na mpiganaji huyo. Akili yake ilisimama kwa muda.

“Nani sasa kauchukua au kuna mtu alikuona wakati unataka kutekeleza zoezi hilo?”

“Yaani mi mwenyewe sikuamini. Kwa kuwa eneo lile hakuna mtu anayeishi. Na hakuna mtu aliyekuwa akinifuatilia, wewe mwenyewe madamu unajua, jinsi mitaa ya maskani yetu ilivyo tulivu. Na kule nilikokwenda hakuna nyumba ya mtu yeyote. Nilikuwa mimi peke yangu.”

“Ni kweli eneo letu ni tulivu na watu wanaogopa kupita mara kwa mara na huko ulikowenda hakuna watu. Sasa ni nani aliuchukua?”

“Madamu inaonyesha mtu aliyeuchukua mwili wa Roika ni mtu jasiri sana na huenda anazijua siri zetu.”

“Hakika sifahamu ni mtu wa aina gani aliyeweza kupita maeneo yetu na kwenda hadi kule mbele na kurudi,” aliongea Ramona akiwa mwenye kutafakari sana.

“Hadi leo mimi huwa sielewi ule mwili ni nani alikuwa ameuchukua.”

“Sawa hamna shida, nashukuru kwa kunifahamisha. Ngoja nifanye upelelezi wangu ili nijue ni nani aliubeba.”

“Sawa madamu siku njema,” alijibu mpiganaji huyo akafungua mlango na kutoka mle chumbani.

Kichwa cha Ramona kilitawaliwa na kutafakari jambo hilo. Aliendelea kujiuliza, ni mtu gani alikuwa ameubeba mwili wa Roika. Baada ya kujiuliza sana swali hilo, alimkumbuka rafiki yake Biyanah ambaye sasa ni maadui wakubwa.

“Mh inaweza kuwa Biyanah aliuchukua, sasa alipajuaje huku na alifika vipi? Maana nakumbuka yeye ndiye aliyekuwa akinifuata mara kwa mara kunihoji kuhusu mahali alipo Roika,” Ramona aliongea peke yake akimfikiria Biyanah.

“Naona hakuna mwingine isipokuwa ni Biyanah, Biyanah ndiye atakayekuwa ameuchukua mwili wa Roika na si mtu mwingine. Huenda nilipokuwa nakuja huku alikuwa akinifuatilia nyuma. Ndio ni kweli, lazima atakuwa ni Biyanah tu. Sasa tukikutana itakuwaje, maana atakuwa ameshanijua mimi kuwa ndiye niliyemuua wa Roika.”

Ramona aliamini kuwa mtu aliyeuchukua mwili wa Roika alikuwa ni Biyanah. Alijua kuwa huenda wakati anaelekea kwenye jumba lao la biashara, Biyanah alikuwa akimfuatilia. Sasa alijua kuwa, Biyanah anajua kuwa yeye ndiye aliyemuua Roika. Ramona hakuwa na njia nyingine ya kukabiliana na rafiki yake, zaidi ya kujihami na kujilinda. Alijua hata akimueleza kila kitu kilichopata kutokea, Biyanah hawezi kumwelewa.

Hivyo alijua kuwa kwa vyovyote vile, Biyanah atakuwa anamtafuta ili amuue. Ramona alishakuwa amesahau kuwa baada ya yeye kumpiga risasi Roika, aliporudi hotelini alikutana na Biyanah aliyekuwa akimhoji kuhusu mahali alipo Roika. Kwa kuwa hakuwa na mtu mwingine wa kumfikiria zaidi ya Biyanah, aliamini rafiki yake huyo ndiye aliyeuchukua mwili wa Roika.

Aliamua kuingia chumba cha silaha na kuchukua bastola aina ya Short Vizic. Akapandisha gauni lake na kuichomeka kwenye paja lake la kulia.  Aliamini kuwa akikutana na Biyanah lazima kuwe na vita.

Nini kitafuatia, usikose Jumatatu.   

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -