Sunday, November 29, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Ilipoishia Jumamosi

ALIAMUA kuingia chumba cha silaha na kuchukua bastola aina ya Short Vizic. Akapandisha gauni lake na kuichomeka kwenye paja lake la kulia. Alimini kuwa akikutana na Biyanah lazima kuwe na vita.

SASA ENDELEA…

Ramona hakuwa na mtu mwingine wa kumfikiria zaidi ya Biyanah. Akili yake yote ilishakuwa imemchunguza Biyanah vya kutosha. Majibu aliyokuwa nayo ni kwamba, Biyanah alikuwa akifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea siku ile pindi yeye alipopewa jukumu zito la kumuua Roika. Lakini alishakuwa amesahau siku ile baada ya yeye kurudi, akiwa mwenye kilio kikubwa, alikutana na Biyanah kule hotelini, aliyekuwa akitaka kujua mahali alipo Roika.

Hivyo si kweli kwamba Biyanah ndiye aliyeuchukua mwili wa Roika, kwani hakujua lolote lililopata kutokea. Biyanah hakuwa akifahamu kama Ramona ni mwanamke anayefanya kazi hatari. Licha ya urafiki wao wa muda mrefu, Biyanah hakujua kingine alichokuwa akikifanya Ramona zaidi ya biashara za urembo na uwakilishi wake wa makampuni ya biasharaa yeye kama mrembo wa dunia.

Ramona alitoka ndani ya jengo lao na kuingia kwenye gari. Alimwambia dereva wake aelekee hotelini. Akiwa ndani ya gari alikuwa akijisemea moyoni mwake.

“Nitamueleza Biyanah kuwa watu wangu wa biashara ndio waliomuua Roika. Sitamwambia kama mimi ndiye niliyemuua, akishindwa kunielewa, itabidi nimuue, endapo yeye atataka kuniua mimi,” alijesemea Ramona akiwa na sura nyingine, iliyotawaliwa na ujasiri mwingine.

Ramona alikuwa njiani kuelekea Nuruwan kunako hoteli ya Alashak. Wakati huo huo Roika naye alikuwa akitokea Alamayana kunako hospitali ya Mohamed Words akielekea hoteli ya Alashak. Ramona yeye alishakuwa ameingia mji wa Nuruwan na kwa muda huo alikuwa anakaribia mitaa ya hoteli. Roika yeye alikuwa nyuma kidogo bado hakuwa mbali tokea alipokiacha kizuizi cha mji wa Nuruwan.

Wakati huo huo Biyanah mwanamke bilionea, alikuwa hotelini, hoteli ile nyingine yenye utegemezi na hoteli ya Alashak. Mawazo yake yalikuwa ni makali na yenye kumuumiza. Mapenzi kwake yalishakuwa zaidi ya virusi, damu yake yote ilikuwa imetawaliwa na hisia zinazomhuhusu mwanaume Roika. Ilikuwa akikumbuka jinsi alivyolionja penzi la Roika kwa siku chache roho ilimuuma sana. Jambo lililomtesa zaidi ni kwamba, hakuwa amekutana na Roika kimwili. Aliona afadhari angepata mimba ya Roika, huenda ingempunguzia machungu. Lakini hakuwahi kulala kitanda kimoja na Roika toka walipoianzisha safari yao ya mapenzi ambayo ilikwenda kuvunjika siku chache baada ya Roika kutekwa kimapenzi na Ramona.

Hasira za Biyanah zilikuwa zikiwaka zaidi pindi alipokumbuka kuwa Ramona alishakuwa amekutana kimwili na Roika. Alimuona Ramona kuwa ni adui yake namba moja, kwa siku zote za maisha yake. Hadi muda huo, hakujua Roika yuko wapi na yuko katika hali gani. Hakujua Ramona amemficha wapi mpenzi wake.

Biyanah alishakuwa ametumia kila aina ya kilevi ili apunguze mawazo, lakini vilevi hivyo, havikuweza kushindana na damu yake, damu iliyokuwa imetawaliwa na chembe hai za mapenzi. Alitumia dawa za kulevya aina zote lakini bado aliendelea kulia akimlilia Roika wake.

Aliamua kuchukua bastola na kuiweka kwenye mkoba wake, alipanga kwenda kumuhoji Ramona kwa mara ya mwisho juu ya mahali alipo Roika. Endapo Ramona hatasema lolote, alipanga kumuondoa duniani.

Wakati Biyanah akiwa hotelini kwake, Ramona alikuwa akiingia hoteli ya Alashak. Moja kwa moja alipanda lifti kuelekea chumbani kwake gholofa ya tatu. Alipofika huko, mawazo juu ya Roika yaliendelea kumwandama. Alijiona mtu aliyekosea sana kukubali kumuua Roika.

“Roika sikujua wewe ndio furaha yangu. Furaha yangu zaidi ya kazi inayoniingizia utajiri. Sasa naona utajiri nilionao, hauwezi kukununua wewe, tayari uko kaburini na umeniacha na pesa zangu. Uko wapi urembo wangu wa dunia? nimeuvaa lakini bado nahangaika. Roika huko uliko tambua mpenzi wako ninahitaji msamaha wako, tayari mama yako amenisamehe na ninakupa pongezi zote kwa kuwa na familia bora,” alijisemea Ramona akitokwa na machozi mengi.

Baadaye alitoka chumbani kwake alipanda lifti kuelekea gholofa ya nne na kwenda chumbani kwa Roika. Majonzi na huzuni huwa vinazidi pindi anapokuwa anaingia kwenye chumba hicho. Chumba kilichotawaliwa na upweke wa hali ya juu.

Wakati Ramona yuko chumbani kwa Roika, Biyanah alishakuwa ametoka hotelini kwake na kwa muda huo alikuwa anashuka kwenye gari akiwa tayari amefika Alashak. Moja kwa moja alielekea mapokezi ambapo aliwauliza wahudumu wa hoteli kama wamepokea taarifa zozote kutoka idara ya polisi, zinazohusu kupotea kwa Roika.  Wahudumu hao walimwambia kuwa hakuna taarifa zozote.

Muhudumu mmoja alimuuliza Biyanah.

“Kwanini hukuwaambia polisi kuwa mrembo wa dunia Ramona anaweza kuwa anahusika na kupotea kwa Roika?”

“Najua Ramona hawezi kuwaambia chochote hata kama atakuwa amemficha Roika. Hivyo ni bora niendelee kumuuliza mimi naona ninaweza kujua kitu. Ukizingatia Ramona anaheshimika, polisi hawawezi kutumia nguvu kumhoji na hawatakuwa na ushahidi wa kutosha kuwa Ramona anahusikia na kupotea kwa Roika,” Biyanah alijibu.

“Lakini polisi wataanza upelelezi makini hapa hotelini kwake. Kwa kuwa kila kitu kinajieleza wazi kuwa Ramona anahusika na kupotea kwa Roika.”

“Nitajua cha kufanya hivyo niachieni kwanza mimi,” alijibu Biyanah.

Biyanah hakutaka kuwaelewa wahudumu, zaidi alitaka yeye kumalizana na Ramona. Kumbukumbu iliyozidisha hasira yake, ilikuwa ni ile ya kwamba Ramona alikutana kimwili na Roika na yeye hakuwahi kuuonja mwili wa Roika. Hiyo ndiyo iliyokuwa ikimtia hasira.

Nini kitafuatia usikose kesho

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -