Monday, January 18, 2021

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU [22]

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

Ilipoishia Jumanne

Akiwa anautafakari ujumbe huo, alikutana na picha aliyokuwa ametumiwa na rafiki yake Ramona. Picha hiyo ilimuonyesha Ramona akiwa yuko sehemu ya michezo ya farasi na mwanaume. Biyanah alipomtazama mwanaume huyo alishtuka.

SASA ENDELEA

BIYANAH hakuyaamini macho yake kwa kile anachokiona, japo ubongo wake ulishatambua mara moja, lakini hali ya kukubali kuwa mwanaume aliyopo kwenye picha ya Ramona ni Roika haikupatikana mara moja. Alitoa macho kuitazama ile picha kadiri alivyoweza ili kuielewa, lakini bado alihitaji nafasi nyingine ya kuamini. Baadaye bila kujilazimisha aliamini mwanaume wa kwenye ile picha ni mpenzi wake Roika ambaye kwa muda huo anajua yuko nchini Mexico kikazi.

Mapigo ya moyo wake yalianza kwenda isivyo kawaida, huku akijiuliza inakuwaje rafiki yake Ramona yuko na mpenzi wake. Kwani yeye anafahamu  kuwa Roika na Ramona ni watu wasiofahamiana.

Hakuwa kabisa na wazo la kuwahusisha watu hao wawili, kufahamiana kwa vyovyote vile. Yaani kifupi, haikumuingia akilini, maana kutumiwa picha na rafiki yake ilimaanisha kuwa siku mbili zilizopita au muda huo, Ramona yuko na Roika. Kwa kuwa mara nyingi Ramona alikuwa akipenda kumtumia rafiki yake picha pindi anapokuwa kwenye starehe fulani au matembezini, basi moja kwa moja Biyanah alielewa kuwa rafiki yake yuko na mpenzi wake.

“Watu hawa wanafahamiana, mbona hainiingii akilini, toka lini na wapi, mbona Roika hakuwa kuniambia kuwa anafahamina na Ramona na hata Ramona mwenyewe hakuwahi kuniambia kuwa, anafahamiana na Roika? Lakini hata hivyo! asingeweza kuniambia kuwa anafahamina na Roika kwa kuwa anajua mimi Roika simjui. Ehee Mungu niambie nini maana ya jambo hili?” alijisemea Biyanah.

Aliendelea kuwa katika sintofahamu huku akiendelea kuongea peke yake kama mtu anayekwenda kuwa chizi.

“Labda wanafahamiana, na kama ni marafiki basi, urafiki wao si wa muda mrefu,”alijisemea.

Biyanah alianza kufikiria labda rafiki yake amemtumia picha hizo kwa lengo la kumuumiza kiutani, ili aumie kuona yuko na mpenzi wake. Lakini swali kwake lilikuwa ni je Ramona anajua kuwa Roika ni mpenzi wake, jibu liliokuwa kichwani kwake lilikuwa ni hapana kwa sababu, hakuwahi kumtambulisha Roika kuwa ni mpenzi wake, kwani toka aanzishe uhusiano wake wa kimapenzi na Roika, hakupata muda wa kutosha kumtambulisha kwa marafiki, ndugu na jamaa zake akiwemo rafiki yake kipenzi Ramona.

Kifupi Biyanah, mwanamke tajiri, hakuwa na jibu la maswali hayo juu ya picha ile aliyotumiwa na rafiki yake. Hazikupita dakika tano, picha zingine mbili ziliingia kwenye akaunti yake ya Twitter, akiwa ametumiwa tena na rafiki yake Ramona, zikimuonyesha Ramona akiwa na Roika hotelini, wakipata chakula, huku nyingine ikiwaonyesha wakiwa bustanini.

Kabla moyo wake haujamuuma, alipoozwa na maneno yaliyoandikwa chini ya zile picha yaliyokuwa na ujumbe uliosema, ‘nikiwa na rafiki yangu, tukibadirishana mawazo.’

Hapo sasa Biyanah alijua kuwa Roika na Ramona ni marafiki. Maumivu ya mapenzi yalianza kupungua kidogo. Japo upande mkubwa wenye mapenzi kwa Roika, ulizidi kutawaliwa na mashaka na wasiwasi. Kwani alijua, urafiki wao huo, unaweza kubadirika ghafla na kuwa uhusiano wa kimapenzi. Kwa kuwa alijua kuwa rafiki yake Ramona, ana uzuri ulioitikisa dunia, basi alijua fika kuwa, huenda uzuri huo unaweza pia ukamtikisa na mpenzi wake, hivyo aliona  anahitaji kuvaa ujasiri na nguvu za kumlinda mpenzi wake mbele ya rafiki yake.

Ilibidi ampigie simu rafiki yake Ramona, ambaye anajua kwa muda huo yuko nje ya nchi kwa masuala yake ya biashara na urembo, ili kumuuliza maswali, kuhusu ukaribu wake na mwanaume anayeitwa Roika Malino.

PAKISTANI

Si Roika pekee aliyestaajabu uzuri wa mwanamke huyo, hata watu wengine walibaki kummezea mate wakimtazama kila hatua aliyopiga, hadi alipojitupa ndani ya maji na kuanza kuogelea.

Moyo, nafsi, akili na macho, vilivyokuwa vinamtambua Ramona kwa undani zaidi, vilimgundua vizuri mwanamke yule  kuwa ndiye Ramona Fika. Moyo ulimuuma Roika kwa maumivu ya ghafla, ule wasiwasi wa kuwa hatamuona Ramona katika hoteli ile ulishamtoka muda mfupi uliopita baada ya Ramona kutoka ndani ya bwawa la kuogelea.

Ramona aliendelea kuwa kivutio kwa watu, licha ya eneo hilo kujawa na wanawake wengi wazuri, tena wa kiarabu, pamoja na wazungu, lakini yeye aliendelea kuoneka ni mwanamke wa kipekee sana.

Baada ya Ramona kutoka ndani ya bwawa la kuogelea, alielekea kwenye kitanda cha mapumziko na kujilaza ili kupata mwanga wa jua, huku akiendelea kupata juisi ya matunda. Roika akiwa kama mtumwa asie na mfano, alinuka pale kwenye meza, meza iliyokuwa umbali wa hatua kumi kutoka pale alipojilaza Ramona. Alibaki anamtazama Ramona Kwa huzuni kubwa, akitamani Ramona ainuke ili amuone lakini alizidi kuogopa vilivyo, kupita alivyokuwa anaogopa mwanzo.

Roika alikaa tena kwenye kiti akiendelea kujishauri njia gani aitumie kuonana na Ramona. Mwili ulitetemeka, akizidi kukumbwa na uoga usio wa kawaida.

Ukiwa umepita muda wa nusu saa, Ramona aliinuka pale kwenye kitanda, akasimama na kurudi ndani ya hoteli. Roika naye aliinuka haraka, ili kuwahi kuona Ramona ataingia chumba gani. Alipiga hatua za haraka kidogo, akimkaribia Ramona aliyekuwa tayari anaingia kwenye lifti ili kupanda vyumba vya juu. Uzuri wa lifti hiyo, ilikuwa ni ile lifti inayoonekana wazi wakati wa kushuka na kupanda, yaani lifti ya nje,, iliyowaonesha watu waliokuwemo ndani na sehemu watakayoishia, lifti iliyokuwa ya vioo pande zote.

Roika alisimama, akimuangalia Ramona aliye ndani ya lifti hiyo, pamoja na watu wawili wakipanda kuelekea juu. Baadae lifti ilisimama, Ramona alishuka na kuelekea chumbani kwake. Moja kwa moja Roika alijua kuwa Ramona ameshuka eneo la tatu la gholofa. Naye aliingia kwenye lifti hadi kwenye eneo hilo la tatu ambapo alishuka  na kutazama huku na kule. Pale sasa hakujua Ramona ameingia chumba gani, alibaki amesimama asijue pa kuelekea.

Hakuwa na ujanja wa kujua, ilibidi amsubirie muhudumu yoyote wa hoteli, atakayekuwa anapita eneo hilo, ili apate kumuuliza. Dakika mbili baadae, muhudumu mmoja akiwa anasukuma meza ya chakula, alikuwa anapita hilo eneo, Roika alimuita na baada ya salamu alimuuliza:

“Bila shaka unamfahamu, Ramona unaweza ukanionyesha chumba chake?”

“Ndio namfahamu, chumba chake ni kile pale mwishoni, hata hichi chakula nampelekea yeye,” alijibu muhudumu huyo.

“Hichi chakula ni chake?” kwa mshangao Roika aliuliza.

“Ndio Mr, vipi unashida naye, kwani wewe ni nani?”

“Naitwa Mr. Roika, mimi ni rafiki yake nimefika jana usiku.”

“Sawa chumba chake ni kile pale wewe nenda ukamgongee,” aliongea muhudumu.

“Sasa sikiliza, naomba uniachie hicho chakula nimpelekee mimi. Nataka kumfanyia saplaizi.”

“Haitawezekana Mr Roika.”

“Kwanini isiwezekane?”

“Kwanza kazi yangu hainuruhusu kufanya hivyo, pili mimi sifahamu kama wewe na yeye mnafahamiana, japo umeniambia ni mpenzi wako lakini siwezi kuliamini hilo mapema. Sasa kukupa chakula ambacho ndio usalama mkubwa kwa mteja wetu ni hatari sana. Je  wewe kama ni adui yake mimi nitajuaje?”

“Ningekuwa ni adui yake, ningepanga muda mwingine wa kumfanyia kitu kibaya, kwa sababu tayari umekwisha nionesha chumba chake. Hadi ukanijulisha chumba anachoishi, inamaana haukuwa na shaka nami”

Roika alizidi kumshawishi muhudumu huyo, ili ampe kile chakula akipeleke mwenyewe chumbani kwa Ramona. Ilikuwa ngumu kwa muhudumu huyo kukubali ombi hilo, akihofia usalama wa mteja wao, lakini baadae alimkubalia na kuahidi kumfuatilia Roika,  ili yasije kutokea matatizo  kwa mteja wao Ramona.

“Asante sana, usijali, hakuna kibaya chochote kitachomkuta mteja wenu. Niamini.

Roika aliipokea ile meza ya chukula, meza yenye magurudumu, iliyokuwa maalumu kwa kusafarisha chakula. Akaanza kuisukuma taratibu kuelekea chumbani kwa Ramona, akimuacha muhudumu huyo, akielekea sehemu yake ya kazi akiwa na chembe ndogo za mashaka.

Alifika hadi mlangoni, akasimama na kutazama huku na kule ili kuona kama kuna mtu alikuwa akipita eneo hilo. Akatega sikio vizuri kwenye mlango wa Ramona ili kusikia kama kuna mtu mwingine tofauti na Ramona  atakaye kuwa ndani akiongea naye, lakini hakusikia maongezi yoyote yale, ukimya ulikuwa mkubwa sana.

Akiwa mwenye uoga mkubwa, huku moyo ukimdunda kwa fujo, Roika  alijiandaa kugonga mlango. Alihema juu juu, jasho jembamba lilimtoka alishusha pumzi na kuipandisha. Moyo uliompenda Ramona, uliishawishi akili yake kuwa jasiri, akili ambayo baadae ilimtuma kugonga mlango, japo mkono wake,  haukuwa na nguvu ya kufanya hivyo.

Kwa ujasiri wa kiume Roika aligonga mlango, baada ya kugonga mara mbili, sauti nzuri ya Ramona ilimruhusu kuingia. Ramona akiwa amekaa kwenye meza akifanya kazi zake kwenye laptop

(kompyuta) alijua kuwa anayemgongea  lazima atakuwa ni mhudumu wa hoteli. Maana muda mfupi uliopita, alikuwa ameagiza chakula.

Akiwa ameugeuzia mgongo mlango wa kuingilia ndani, Ramona aliendelea kuwa makini na kazi zake, asimtazame mhudumu aliyemletea chakula. Wakati huo tayari Roika alikuwa amekwishaingia ndani. Na mara baada ya kuingia, alifunga mlango. Macho yake yalimtazama Ramona aliyekuwa makini na kazi zake, aliyekuwa anajua kuwa nyuma yake kuna muhudumu aliyemletea chakula.

Moyo wa Roika uliendelea kuwaka na kuzima kama taa ya king’ola, ukiashilia hatari fulani. Woga ulishakuwa sehemu ya pumzi yake kwa wakati huo. Alimtazama Ramona aliyekuwa amevaa kijigauni chepesi, kifupi cha rangi nyeupe. Kilichokuwa kinaonesha nusu nzima ya mwili wake, kuwa yu uchi. Hapo akili ya Roika ndio ilisimama zaidi.

Ramona akijua nyuma yake kuna muhudumu aliyemletea chakula, akauliza..

“Umeniletea kinywaji gani? maana nilisahau kukwambia uje na Pandora.”

Nini kitafuatia? usikose kesho

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -