Wednesday, October 28, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

Ilipoishia Jumanne

HARAKA na kwa uwezo wa hali ya juu, Ramona alifunua gauni lake, alichomoa bastola na kufyatua risasi. Biyanah alipotaka kufyatua ya kwake, tayari risasi iliyotoka kwenye bastola ya Ramona, ilishakwenda kumtoboa kwenye mbavu za kushoto. Alipiga kelele kwa maumivu, alirudishwa nyuma na kujigonga kwenye kochi na kudondoka chini.

Roika akiwa amekifika chumba chake, baada ya kushuka kwenye lifti, alisikia kishindo kutoka ndani. Alipofungua mlango, alimkuta Ramona akiwa ameshika bastola na pembeni yake alimkuta Biyanah akiwa anaugulia maumivu.

SASA ENDELEA

Ramona alipotazama mlangoni, macho yake hayakuweza kuamini kabisa, mtu  anayemuona. Moyo wake ulishtuka, kasi ya kupiga iliongezeka ghafla. Alibaki ametoa macho kama mtu aliyekufa kifo cha kushangaza.

Roika alibaki amesimama asielewe jambo lolote. Alibaki anamtazama Ramona aliyekuwa na bastola mkononi, huku akigeuka kumtazama Biyanah aliyekuwa chini akitokwa na damu.

Ramona alipatwa na mshtuko mkali wa kichwa. Viungo vya mwili wake vyote vilisimama kufanya kazi. Hatimaye alidondoka chini na kupoteza fahamu. Roika alimkimbilia, akamshika na kumuita jina lake mara mbili.

“Ramona! Ramona!”

Lakini Ramona hakuweza kuitika. Aliyainua tena mcho yake na kumtazama  Biyanah aliyekuwa akiendelea kugalagala kwa maumivu. Alimuacha Ramona na kwenda kumshika Biyanah na kukilaza kichwa chake kwenye kifua chake.  Alimshika sehemu ya mbavu, sehemu iliyokuwa ikitokwa na damu. Alimtazama Biyanah usoni aliyekuwa akitokwa na machozi.  Moyo wake ulihuzunika sana.

Biyanah naye alimtazama Roika usoni kwa huruma na majonzi na kwa sauti ya chini aliuliza.

“Roika wangu umekuja?”

“Ndio nimekuja, kaza moyo kwani uko kwenye mikono yangu,” alijibu Roika huku machozi yakimtoka.

Hakika Roika alichanganyikiwa. Ramona alikuwa  akihitaji msaada, pia Biyanah naye alikuwa akihitaji msaada. Lakini msaada aliokuwa akihitaji Biyanah, ulikuwa ni mkubwa zaidi, kwani muda wowote angepoteza maisha. Damu nyingi zilikuwa zikiendelea kumtoka kwenye mbavu zake za kulia. Roika alimtazama Biyanah na pia alimtazama Ramona. Hakuelewa afanye nini.

Haraka alichukua simu yake ya mkononi na kumpigia Dk Sufian.

“Haloo Dk Mr Roika hapa.”

“Ndio Mr Roika habari za mchana?”

“Si nzuri Dk, nina matatizo, nahitaji msaada wako wa hali na mali.”

“Kuna nini tena Mr Roika?”

“Dk kuna mwanamke anahitaji msaada, amepigwa risasi na mwingine yuko chini amepoteza fahamu, fanya upesi Dk tafadhari sana,” aliongea Roika kwa msisitizo.

“Ni wapi huko?” Dk Sufian aliuliza.

“Ni katika hoteli ya Alashak.”

“Alashak?”

“Ndio.”

“Mr Roika huko ni mbali sana, nitaweza kuwahi kufika kweli?”

“Vyovote itakavyokuwa Dk, kwa kuwa siwezi kuwatoa watu hawa nje ya hoteli. Naamini Mungu atakusaidia fanya upesi Dk.”

“Sawa ngoja nijaribu, ila chukua pamba na kitambaa kizito viweke sehemu ya kidonda na umfunge kwa shuka. Na huyo aliyezimia mlaze kitandani na uendelee kumpepea sawa?”

“Sawa Dk.”

Dk Sufian alitoka ndani ya hospitali ya Mohamed Words, aliingia kwenye gali yake, gari aina ya Lava 4. Aliondoka hospitalini hapo kuelekea mji mdogo wa Nuruwan kunako hoteli ya Alashak kwenda kumpa msaada Roika aliyekuwa na mtihani wa kuokoa maisha ya wanawake wawili.

Roika alifanya kama daktari alivyomwambia, alitumia njia ya kienyeji kuizuia damu isiendelee kutoka kwa Biyanah. Alirudi kwa Ramona akambeba na kumlaza kwenye kochi ambapo alimpepea kwa muda wa dakika tano na baadae alirudi tena kwa Biyanah.

Biyanah bado alikuwa macho, bado aliendelea kuugulia maumivu makali yaliomfanya kuhema kwa tabu. Lakini alijihisi raha na matumaini kuwa kwenye kifua cha Roika. Macho yake hayakuacha kumtazama Roika mwanaume anayempenda kuzidi kila kitu alichokuwa nacho. Ingawa alikuwa kwenye maumivu makali ya risasi, lakini aliendelea kutabasamu, maana sura ya Roika ilimpa furaha.

“Nakupenda sana Roika,” aliongea Biyanah kwa tabu huku mkono wake uliokuwa umetapakaa damu, ukimshika Roika kwenye shavu lake la kulia.

Roika hakujibu lolote, zaidi machozi pekee ndio yaliokuwa yamechukua nafasi ya maneno. Mara kwa mara alimtazama Biyanah na kuinua macho yake kumtazama Ramona. Roika hakujua ni nini kilikuwa kimetokea mle ndani, hakujua sababu iliyompelekea Ramona kumpiga risasi Biyanah. Pindi yeye alipokuwa anakuja, hakutegemea kuwaona wanawake hao wawili chumbani kwake. Kwani nia yake haikuwa kuonana na Ramona wala Biyanah. Hakupenda kabisa kukutana nao hususani Ramona aliyekuwa akijua kuwa Roika ni marehemu na Roika alilijua hilo, kuwa Ramona anajua kuwa yeye amekwisha kufa.

“Roika nitazame mimi,” aliongea Biyanah aliyekuwa anazidi kuishiwa nguvu.

Roika aliacha kumtazama Ramona, alishusha macho chini na kumtazama Biyanah aliyekuwa bado amemlaza kwenye kifua chake.

“Usimtazame mtu aliyenipiga risasi kwa ajili yako, bali nitazame mimi ambaye nimehangaika hizi siku zote kukutafuta. Maana nafsi yangu inaishi ndani yako,” aliongea Biyanah maneno yaliomuumiza sana Roika.

“Usijali Biyanah kila kitu kitakuwa sawa,” alijibu Roika maneno yasiokuwa na imani ndani yake.

“Roika niambie kama unanipenda.”

Roika alikaa kimya kwa muda wa dakika mbili asijue la kujibu. Kabla hajalijibu swali hilo, lenye mtihani ndani yake, Biyanah alifumba macho na kupoteza fahamu.

Wakati huo Dk Sufian alizidi kukanyaga mafuta akilitoa gari kwa kasi katika Barabara ya Alamayana na kuliingiza kwenye Barabara ya Nuruwan. Polisi hawakulisimamisha gari lake maana walilifahamu gari hilo kuwa ni la Dk. Sufian.

Nini kitafuatia? usikose kesho     

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -