Tuesday, October 27, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

Ilipoishia jana

“Sasa Mr Roika, unafikiri kwa sasa Ramona anaweza kuchukua nafasi ya Shazayi?” Dk. Sufiani aliuliza.

SASA ENDELEA

 “Dk. jina la Shazayi ni jina kuu sana kwenye moyo wangu. Tayari limekwisha chukua nafasi ya Ramona. Unajua mwanzoni, nilikuwa najua kuwa hakuna mwanamke yoyote hapa duniani, atakayechukua nafasi ya Ramona. Niliamini Ramona ndiye mwanamke pekee atakayeendelea kuishi kwenye moyo wangu siku zote za maisha yangu. Lakini nahisi nilikuwa najidanganya. Kumbe alikuwepo mwanamke mwingine aliye na nguvu kuliko yeye,” alijibu Roika kwa hisia kali.

“Roika najua ni jinsi gani Shazayi alivyokubadilisha, lakini naomba nikuulize swali.”

“Uliza Dk.”

“Je, unampenda Shazayi kwa kuwa aliyaokoa maisha yako tu au upendo wako kwake ni zaidi ya hivyo?”

“Dk. naamini Shazayi nampenda si kwa sababu aliokoa maisha yangu. Bali moyo wangu umegeuka kimaamuzi na kuridhika kupita kiasi. Kitendo cha kuokoa maisha yangu kilikuwa ni ishara tu ya sisi kukutana. Na mi mwenyewe nilishangaa nguvu ya upendo aliyonayo Shazayi. Nilijikuta nampenda kupita kiasi kuliko ule mwanzo wa sisi kukutana.”

“Sawa Mr Roika, lakini je, upendo wako kwa Ramona umehama kwa sababu Ramona ni mtu anayefanya biashara haramu?”

“Hapana si kwa sababu ya biashara haramu, kama nimempenda, nimempenda tu, kwa sababu mara nyingi upendo huwa hauangalii tabia ya mtu, japo tabia au kazi mbaya anayofanya mpenzi wako, inaweza kukukatisha tamaa kwenye suala zima la kumuoa na pia kiasi fulani cha upendo kinapungua. Lakini Ramona nampenda hata kama ni mtu mbaya. Lakini Shazayi ni zaidi, kwa sababu nimegundua kuwa ni mwanamke ninayeweza kumuoa nikiwa huru ndani ya moyo wangu na pia kwenye maisha yangu ya kawaida.”

“Sawa Mr Roika, tuishie hapo. Lakini unakazi kubwa sana ya kuwaeleza  wanawake hawa juu ya upendo wako kwa Shazayi ili wakuelewe na wakuache huru. Hata hivyo, naamini utaweza.”

“Ni kweli Dk. namwomba Mungu anisaidie katika hili.”

Baada ya maongezi hayo, taratibu za kuwapeleka Ramona na Biyanah hospitalini, ilibidi zifanyike. Kwa sababu hali zao zilikuwa bado si nzuri bado walihitaji matibabu. Lakini ilibidi watolewe hotelini, pasipo polisi kujua, kwa sababu wangejua jambo hilo, lingeweza kufika mbali. Ilibidi waongee na baadhi ya viongozi wa hoteli waliokuwa zamu siku hiyo, ambapo waliwasimulia hali halisi iliyopata kutokea. Viongozi hao walikubali kuwasaidia na walifanya hivyo ili kuepuka hoteli yao kuchukuliwa hatua za kisheria na serikali.

Ilibidi watumie gari la wagonjwa (ambulance) ambalo ni maalum kwa ajili ya watu wanaopata matatizo katika hoteli. Ramona na Biyanah waliingizwa kwenye gari hilo na safari ya kuelekea hospitali ya Mohamed Words ilianza mara moja. Roika alipanda na kukaa nyuma ya gari hilo walikolazwa Ramona na Biyanah.

Huku hospitalini, Shazayi alianza kulia kwa kuwa ni muda mrefu ulikuwa umepita, Roika alikuwa hajarudi. Alijua huenda Roika wake, amepatwa na tatizo. Alibaki amelala pale kitandani, akitamani kuamka lakini bado mwili wake ulikuwa hauna nguvu. Mara kadhaa alipotaka kufanya hivyo, muuguzi alimkatalia, akimwambia kuwa bado hakuwa na nguvu ya kusimama.

Baada ya dakika 50, gari la wagonjwa lenye nembo ya hoteli ya Alashak, lilikuwa likiwasili hospitali ya Mohamed Words. Wakati hudo Dk Sufian bado alikuwa  nyuma akitumia usafiri wake binafsi aliokuwa amekwenda nao hotelini.  Waaguzi walikuja na vitanda vya wagonjwa na kuwapeleka chumba kimoja cha wagonjwa mahututi. Maelezo ya kuwapeleka Ramona na Biyanah chumba kimoja, waliyapata kwa njia ya simu kutoka kwa Dk Sufian. Aliyewaambia watumie chumba cha gholofa ya pili.

Baadae Dk Sufian aliwasili, ambapo yeye na Roika, walikuwa pamoja kushughulikia afya za Ramona na Biyanah, waliokuwa hawajitambui. Wakati Dk akiendelea kuwapa matibabu Ramona na Biyanah, Roika alimuomba Dk Sufian gari lake, akitaka kutoka nalo nje mara moja. Daktari alimpa ufunguo, ambapo aliondoka na gari hilo na kwenda nalo duka moja la maua, duka lililokuwa pembeni ya barabara ya Alamayana, barabara inayokatiza kwenda Ramat. Aliyanunua maua mekundu, yenya mchanganyiko na maua ya rangi ya kijani na kurudi nayo hospitalini. Wakati huo ilikuwa ni saa mbili kasoro usiku.

Shazayi akiwa analia, akiwa amegoma kula wala kunywa chochote, Roika alikuwa anaingia mle chumbani. Alipogeuka kulia kwake, alimuona Roika akiwa anatabasamu. Mapigo ya moyo wake yalimdunda, kifua chake kilishuka. Alibaki ametoa macho akimtazama Roika mwanaume aliyezidi kumvutia kila baada ya sekunde moja.

Roika akiwa ameyaficha  maua kwa kuiweka mikono yake nyuma, alipiga hatua kumsogelea Shazayi aliyekuwa ameganda kama sanamu. Akiutazama uzuri mpya wa Roika. Roika alipofika kitandani, alimtazama Shazayi kwa furaha kubwa na kisha akamuuliza.

“Hebu bashili nimekuletea zawadi gani?”

Kwa tabasamu ambalo lilimfanya Roika kuona sana aibu, Shazayi alijibu.

“Umeniletea maua mazuriiii.”

“Whaat!”

Roika alishangaa kuona Shazayi amebashili sahihi. Alijiuliza amejuaje kama amemletea maua.

“Nashangaa umejuaje au umeyaona wakati naingia?”

“Roika mpenzi wangu, mimi ni mwanamke ambaye ninazijua hisia zako. Lile unalowaza kunitendea, ndio ambalo na mimi naliwaza kukutendea wewe. Umeshasahau kuwa Mungu ametuleta watu tunaofanana? Nilijua kuwa huwezi kuniletea chakula kwa wakati huu, wala kuniletea nguo, wala dhahabu, bali nilijua utaniletea maua ambayo ni ishara ya upendo wetu wenye thamani.”

Nini kitafuatia? Usikose Jumatatu

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -