Wednesday, October 21, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

Ilipoishia Jumamosi

 “Roika mpenzi wangu, mimi ni mwanamke ambaye ninazijua hisia zako. Lile unalowaza kunitendea, ndilo ambalo na mimi naliwaza kukutendea wewe. Umeshasahau kuwa Mungu ametuleta watu tunaofanana? Nilijua kuwa huwezi kuniletea chakula kwa wakati huu, wala kuniletea nguo, wala dhahabu, bali nilijua utaniletea maua ambayo ni ishara ya upendo wetu wenye thamani.”

SASA ENDELEA

Maneno ya Shazayi yalizidi kumshangaza sana Roika, alimwona ni mwanamke ambaye ni tofauti na wanawake wote hapa duniani. Kila neno alilokuwa analizungumza binti huyo wa Rais, lilikuwa ni neno lenye hekima na elimu ya kutosha. Maneno ambayo yalizidi kuufanya moyo wa Roika kugeuka rangi na kuwa rangi yenye sura ya Shazayi.

Taratibu Roika aliyatoa maua kutoka nyuma yake na kumpa Shazayi. Shazayi aliyapokea na kuyapeleka puani. Aliipenda harufu yake iliyompa hisia kali za mapenzi.

“Asante mume wangu,” alijibu Shazayi huku akiyabusu maua.

“Nisamehe kwa kuchelewa,” Roika aliongea.

“Nausamehe moyo wangu uliokuwa na hofu juu yako.”

Roika alimtazama Shazayi kwa dakika mbili za ukimya, Shazayi naye alibaki kumtazama Roika akijua kuwa kuna neno anataka kusema.

“Roika mpenzi wangu, macho yako yanakitu cha kusema hebu niambie wafikiria nini juu yangu?”

“I love Shazayi,” (Nakupenda Shazayi)

“Really ?” (Kweli? )

“Hakika.”

“Asante sana Roika, siamimi kama ndoto nilizokuwa naziota sasa zimetimia.”

“Amini hivyo Shazayi. Lakini shukrani zangu ziende kwa mama yangu mzazi aliyekufanya wewe ulejee katika uzima.”

“Una maana gani Roika?”

“Mama yangu ndio aliyejitolea damu kwa ajili yako.”

“Kweli Roika?”

Shazayi alishangaa kusikia hivyo, akili na moyo wake vikatulia kumsikiliza Roika, huku vikiwa na maswali mengi.

“Ni kweli kabisa, sikuona mtu mwingine wa kukupa uhai, zaidi ya mama yangu aliyekuwa damu yenye kundi moja na lako.”

“Roika hakika inanishangaza, kwani mama yako naye yuko hapa Pakistani?”

“Hapana nimemuacha Tanzania.”

“Aliwezaje kufika kwa muda mfupi na kunisaidia?”

“Mimi nilisafiri kurudi nyumbani kwa hiyo damu ameitoa akiwa kule kule.”

“Mmmh! Roika mpenzi uliweza kusafiri na ile hali uliyokuwa nayo?”

“Mungu wako alinisaidia.”

“Asante sana Roika nakupenda sana. Ninahamu kubwa ya kumuona mama yako ambaye sasa ni mama yangu.”

“Yeye ndiye anahamu ya kumuona mwanamke shujaa aliyeyaokoa maisha ya mwanaye.”

Roika aliposema hivyo Shazayi alicheka huku akitokwa na machozi. akamkumbatia Roika na kumwambia.

“Naisubiri kwa hamu siku ambayo wazazi wetu watakuwa pembeni wakiifurahia ndoa yetu.”

Shazayi aliposema hivyo, Roika aliacha kutabasamu. Akainama chini akionyesha kuwa mwenye huzuniko kubwa.

“Roika mbona kauli yangu imekunyima raha, nini tatizo?”

“Shazayi baba yako sidhani kama atakuwa tayari mwanaye uolewe na mtu kutoka Afrika.”

“Roika mpenzi, hutakiwa kuhofu kuhusu baba yangu, bali unatakiwa uwe na hofu ya kunipoteza kwa sababu, hata baba apinge vipi uhusiano wetu, kamwe hawezi kuubadilisha moyo wangu. Lazima itafika kipindi itamlazimu akubali kile binti yake anachotaka. Lakini naamini wazazi wangu hawezi kupinga uhusiano wetu.”

“Kweli?”

“Amini hivyo.”

Baada ya maongezi hayo, wote walikumbatiana. Hakika walipendeza sana kuwa pamoja. Muda mfupi baadae, Dk Sufian aliingia. Alipofika karibu yao alimsogelea Shazayi.

“Vipi madam unaendeleaje?” aliuliza daktari.

“Naendelea vizuri sana, nakushukuru kwa msaada wako hakika umeonyesha kunijali,” alijibu Shazayi.

“Usijali madam hii ni kazi yangu.”

“Lakini ni  lini nitatoka hapa?” Shazayi aliuliza.

“Umebakiza siku mbili. Lakini kuna taarifa sio nzuri.”

“Heee! Tarifa gani tena Dk?”

“Sio taarifa ya kiafya bali ni ya kiserikali. Kikundi cha kigaidi cha Swaba kimeidanganya serikali kwamba kinakushikilia wewe. Hivyo serikali pamoja na baba yako, wanahangaika wakitafuta njia ya kukukomboa na wanaweza kuwapa kikundi hicho vitu wanavyohitaji ili wakupate wewe.”

“Hata mimi taarifa hiyo imenishangaza nimeisikia leo kupitia redio Ala Suni,” aliongea Roika.

“Sio redio hiyo tu vyombo vyote vya habari  duniani kote vinatangaza taarifa hiyo.”

“Mungu wangu, baba yangu na serikali yake wanaweza kuingia katika hasara,” aliongea Shazayi kwa hofu kubwa.

“Nitaomba mlijadili hilo ila haitawezekana kwa wewe madam kutoka hapa hospitali kabla ya kesho kutwa. Ni lazima upone kabisa,” aliongea Dk Sufian.

Baada ya kusema hivyo, Dk Sufian alitoka pale chumbani na kwenda chumba walicholazwa Ramona na Biyanah. Akiwaacha Roika na Shazayi, wakiitafakari ile taarifa ya vyombo vya habari. Aliwatazama Ramona na Biyanah Baada ya kuridhishwa na Maendeleo yao, aliwatenganisha na kuwaweka kila mmoja chumba chake.

Ikiwa ni saa sita usiku, Ramona alifumbua macho. Alishangaa kujiona akiwa hospitalini. Haraka aliinua kichwa chake na kumtazama Dk Sufian aliyekuwa pembeni yake. alipotaka kunyanyuka, daktari alimzuia.

“Subiri kwanza bado hali yako si nzuri,” aliongea Dk Sufian.

“Nimefika saa ngapi hapa?” aliuliza Ramona kwa ukali fulani.

“Una masaa matatu tokea ufike.”

“Nahisi mara ya mwisho nilimuona Roika, nadhani nilikuwa naota au mzimu wake ulinitokea. Ama sivyo nilichanganyikiwa. Nieleze Dk nina akili sawa sawa?” aliongea Ramona kama mtu anayekwenda kuwa kichaa.

“Hapana wewe si kichaa inawezekana ulimuona kweli.”

“Kama kweli nilimuona, nioneshe yuko wapi Roika wangu. Nioneshe upesi,” aliongea Ramona kwa ukali huku akitokwa na machozi.

Nini kitafuatia? Usikose kesho.    

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -