Thursday, December 3, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

Ilipoishia Jumanne

“RAMONA amekuwa mtu mbaya kwa sababu ya mapenzi. Kwa sababu ya kumtaka mwanamume asiye wake. Nilipomuuliza kuhusu kifo chako aliamua kunipiga risasi. Sikutegemea kama rafiki yangu kipenzi atakuja kuniua kisa mwanamume wangu. Namchukia sana Ramona tena sana,” aliongea Biyanah kwa machozi.

Maneno hayo yalikuwa yamemuumiza sana Roika, aliona hana sababu ya kuyaweka akilini kwake kwa sababu, kwa muda huo hakuwa na lengo la kumuweka Biyanah wala Ramona moyoni mwake.

SASA ENDELEA

 

 

Roika aliogopa sana kwa kitendo cha wanawake hao kuingia kwenye mgogoro kisa yeye. Hakuwa na majibu rahisi kwa Biyanah, ambaye kiukweli hakuwa akimpenda. Alishindwa kuwa na uhuru wa kuzungumza, maana tayari mke wake alishakuwa ametambulika ndani ya moyo wake.

Alimtazama Biyanah kwa dakika moja ya ukimya. Alikiinamisha kichwa chake chini na kukiinua na kisha akasema.

“Biyanah, haina haja ya kumchukia Ramona kisa mimi. Urafiki wenu ni mkubwa kuliko unavyofikiri. Ya nini kuuana kisa mwanamume? Ni vibaya kufikia hatua kama hiyo.”

“Roika ni nani umemshuhudia akimpiga risasi mwenzake?” Biyanah aliuliza.

“Hata kama, lakini haipendezi nyie kufikia hatua ya kupigana risasi kisa mimi. Namfahamu Ramona na pia nakufahamu wewe. Ramona asingetaka kukuua ikiwa wewe hukutaka kumuua yeye. Nyie wote mnamakosa na inabidi mtubu dhambi hii.”

“Roika hupaswi kumtetea Ramona. Ramona ameniambia wewe umekwisha kufa na leo na kuona, hivi mtu kama huyo nimfananishe na kiumbe gani? hapana Roika haiwezekani. Achana na Ramona si mtu mzuri.”

“Yote kwa yote Biyanah mimi nataka ugomvi wa wewe na Ramona uishe. Nataka muanze maisha mapya.”

“Hapana Roika mimi kupatana na Ramona itakuwa ngumu, haiwezi akanichukulia mpenzi wangu halafu pia atake kuniua.”

“Nataka msameheane ili tuyatazame maisha mema yanayokuja.”

“Nitamsamehe endapo atakaa mbali na wewe,” aliongea Biyanah huku akitazama pembeni.

“ Nitafurahi endapo wewe na yeye mtaendeleza urafiki wenu.”

Biyanah hakuonyesha dalili yoyote ya kukubali kile Roika alichokuwa akikizungumza. Alimtazama Roika kwa sekunde kadhaa,  akamshika mkono na kisha akamuuliza.

“Roika bado unanisaliti?”

“Kwa nini unaniuliza hivyo Biyanah?”

“Nataka kujua unanipenda mimi au unampenda Ramona?”

Swali la Biyanah lilikuwa gumu kichwani kwa Roika, hakujua ajibu nini, maana tayari moyo wake ulishakuwa umehama kwa wanawake wote wawili. Ingawa alikuwa akimpenda Ramona kuliko Biyanah. Biyanah hakujua kama tayari Roika amekwisha pendana na mtoto wa Rais wa nchi hiyo aliyekuwa hapo hapo Hospitalini.

“Biyanah swali lako siwezi kulijibu saa hii nitakujibu wakati mwingine.” Aliongea Roika.

“Sawa, lakini niambie kama unanipenda.”

“Ndio nakupenda .”

“ Roika usichezee hisia zangu, upendo wangu kwako ni vigumu kuuelezea. Nakupenda sana Roika, nimeacha biashara zangu zote nimekuja Pakistani kuja kulifuata penzi lako tazama navyogangaika. Yote kwa sababu siwezi kuishi bila wewe.”

Wakati Biyanah akiongea hayo, Dk Sufian alikuja pale kitandani na kumwambia Roika.

“Mr Roika inatosha, mwache mgonjwa apumzike utakuja wakati mwingine.”

“Dk sitaki kupumzika mwache mpenzi wangu akae hapa,” aliongea Biyanah huku akitokwa na machozi.

“Unahitaji kupumzika jeraha bado halijaanza hata kukauka. Mr Roika naomba umpishe mgonjwa. Tafadhari sana.” aliongea daktari.

Biyanah alianza kulia akihitaji Roika aendelee kuwepo karibu yake. Lakini hiyo ilikuwa ni mbinu ya Dk Sufian ya kutaka Roika atoke pale na aende kwa Ramona maana muda ulikuwa unazidi kwenda na hali ya Ramona ikizidi kuwa mbaya.

Roika alitoka mle chumbani alikolazwa Biyanah na kwenda chumba cha Ramona huku akiwa amemuacha Biyanah kwenye kilio kikubwa. Kabla haujafikia mlango wa chumba cha Ramona, alikaa kwenye kiti kilichokuwa karibu na mlango. Mawazo yalikuwa ni mengi kichwani mwake. Maana ni kwa mara ya pili anakutana na mpenzi wake ambaye hadi kufikia muda huo alikuwa amekwisha kumuondoa kwenye himaya yake ya mapenzi. Kila alipoikumbuka sura ya Ramona, kumbukumbu  kupigwa risasi na mrembo huyo wa dunia, ilikuwa ikichukua nafasi. Toka mwanzo hakuwa amefikiria kuja kuonana tena na Ramona, lakini kutokana na daktari kumsihii kuonana naye ili kuokoa akili zake, ilimbidi akubali kwa shingo upande. Lakini ilikuwa ni ngumu kwake kuonana na mtu ambaye siku zote anajua kuwa Roika ni marehemu.

Baada ya kukaa pale kwenye kiti kwa muda mrefu. Alinuka na kuelekea kwenye mlango wa chumba alicholazwa Ramona. Alishusha pumzi na kuipandisha kwa uwoga wa hali ya juu, alifungua mlango na kuingia ndani. Kwa muda huo Ramona alikuwa amejikunyata juu ya kitanda, akiwa amegeukia upande mwingine. Taratibu Roika alipiga hatua kumsogelea. Hisia na mapenzi kwa Roika, vilimfanya Ramona kugeuka ili kumtazama mtu aliyekuwa karibu yake.

Macho yalimtoka alibaki ameganda kama sanamu. Akili yake ilianza kujichunguza kama ni kweli ilikuwa katika hali halisi au ilikuwa ikiota. Akili na macho yake yalimsibitishia kuwa ni kweli aliyekuwa akimuona mbele yake alikuwa  ni yule mwanaume aliyempiga risasi yeye mwenyewe. Hakika ilikuwa ni ngumu kwa yeye kuamini.

“Roika,” aliongea Ramona kwa sauti ya chini.

“Mimi hapa,” Roika aliitika huku akitoa tabasamu pana.

“Inawezekana vipi?” Ramona aliuliza.

“Amini ni mimi Roika.”

Kama mtu aliyechanganyikiwa Ramona alimkumbatia Roika na kumshika vilivyo. Alianza kulia kama mtoto mdogo.

Nini kitafuatia? Usikose kesho  

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -