Tuesday, November 24, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Ilipoishia jana

WAKIWA wamekaa, mmoja wao aliuchukua mkoba wa Ramona na kuufungua. Ndani yake alivikuta vitu vingi lakini kilichomshangaza aliiona waleti ya Roika.

SASA ENDELEA

Mmoja wao aliikumbuka ile waleti kuwa ilikuwa mikononi mwao. Lakini hakushtuka sana kwa sababu, alijua huenda Ramona alikuwa ameichukua kwa nia ya kuhifadhi waleti ya mpenzi wake aliyekuwa ameiaga dunia . Lakini alishtuka baada ya  kukiona kitambulisho cha Roika, kitambulisho cha umoja wa mataifa (UN) kilichokuwa ndani ya waleti hiyo.

Itakumbukwa kuwa pindi watu hao walipokuwa wamemnasa Roika ndani ya jumba lao la biashara, walimfanyia upekuzi na kufanikiwa kuiona waleti yake ambayo waliikagua na  kuviona vitu vingine, isipokuwa kitambulisho hicho.

Mmoja wao aliwauliza wenzake.

“Jamani hii waleti ilikuwa mikononi mwetu si ndivyo?”

“Ni kweli imekuwaje iwe mikononi mwa Ramona?”

“Si mbaya huenda alitaka tu kuihifadhi si unajua yule Mwafrika alikuwa mpenzi wake?”

“Sawa lakini unakumbuka hatukufanikiwa kukiona kitambulisho chochote cha yule bwana?”

“Ni kweli kwani vipi?”

“Kiangalieni hiki.”

Wote walikitazama kitambulisho kile ambacho siku ile hawakuwa wamefanikiwa kukiona. Jambo lile liliwashtua sana. Walijadiliana nini cha  kufanya, ambapo baadaye waliamua kuwa suala hilo walipeleke  kwa viongozi wao.

Hawakuwa na muda wa kupoteza, walitoka ndani ya hoteli hiyo wakaingia kwenye gari lao na kuondoka. Walirudi katika maskani yao, ambapo waliwaeleza viongozi wao kuhusu kukiona  kitambulisho cha Roika, kitambulisho kilichokuwa kwenye  waleti ambayo kwa muda huo ilikuwa imechukuliwa na Ramona.

Viongozi wa Swaba na viongozi wa mtandao wa biashara, walikaa meza moja ili kulijadili suala hilo. Waliona kwamba Ramona alikuwa anafahamu kuwa mtu waliyemua na kumchoma moto ni mtu wa umoja wa mataifa. Itakumbukwa kuwa kama siku ile wangefanikiwa kukiona kitambulisho hicho, Roika asingeuawa mara moja. Jambo ambalo lingefanyika ni kumkamata Roika na kumuweka kwenye mipango yao ya video, itakayoujulisha umoja huo kuwa imemshikilia mtu wao. Kitendo hicho, kingekuwa kimeudhalilisha umoja wa mataifa, umoja unaoendesha masuala yake ya ulinzi na upelelezi kwa siri kubwa. Na huenda hata Ramona angekuwa mashakani kwa sababu, yeye pia angeonekana ni mtu wa siri wa umoja huo.

Watu hao walilijadili suala hilo kwa mapana. Ilibidi wawajulishe wenzao waliokuwa mbali na Pakistani. Ambapo walitumia kufanya nao kikao kwa njia ya mtandao wa intaneti. Viongozi  wa vikundi na mitandao ya biashara haramu duniani kote, walilisikiliza suala hilo ambalo lilisimuliwa na Makx Viego kuhusu kukamatwa kwa mtu ambaye mwanzo hawakujua kuwa alikuwa ni mtu wa UN. Suala kuu lilibaki kwa Ramona maana mwenye kitambulisho hicho wanajua kuwa walishakuwa wamekwisha kumuua.

Walichokuwa wanakijua wao kuwa ndani ya umoja wa mataifa, Ramona ni mtu aliyechaguliwa tu kuwa mwakilishi wa wanawake wanaoishi katika mazingira magumu. Kwa sababu kawaida ya mrembo yoyote wa dunia, akishakwisha kushinda taji hilo, huwa anachaguliwa na UN kuwa mwakilishi wa masuala fulani ya kijamii. Hilo walikuwa wanalifahamu.

Wengi wao walianza kuamini kuwa huenda Ramona si mtu aliyechaguliwa kufanya shughuli hiyo tu bali ni mtu anayehusika na masuala ya ulinzi na upelelezi kama mfanyakazi hatari wa umoja huo. Kwani umoja wa mataifa unashughulika na masuala mengi ili kuilinda dunia. Kwani walijiuliza kwa nini Ramona awe anafahamiana na mtu kama Roika. Kwa sababu kitambulisho cha Roika kinaonyesha si mtu wa kawaida. Hivyo waliona kuwa Ramona alikuwa amejiunga katika mtandao wa wao wa biashara si kwa nia ya kufanikiwa kiutajiri, bali kwa masuala ya upelelezi, upelelezi  utakaokuja kuviangamiza vikundi na mitandao yao ya biashara.

Lakini baadhi yao walipinga wakisema kuwa Ramona ni mtu asie husika na kazi za siri ndani ya umoja huo. Walipinga kuwa Ramona si mtu anayewazunguka wala kuwapeleleza. Walisema wanaamini kuwa Ramona ni mwanamke makini na mfanyakazi wa kuaminiwa ndani ya mitandao yao. Wengine walisema kama Ramona angekuwa mtu mbaya kwao asingefanikiwa kusambaza zaidi ya silaha 50,000 duniani kote.

Kiongozi wa kikundi cha waasi cha Congo, bwana Mutika Suaka, alisema kuwa, anaamini  Ramona ni mwanamke mzuri kwake hawezi kumgeuka. Naye kiongozi wa kikundi cha Al Shabaab Munil Hamad, alisema haoni sababu ya kumshuku madam Ramona kuwa ni mtu mbaya kwao. Kiongozi mkubwa wa serikali ya Urusi, anayejihusisha na vikundi hivyo, alisema anaamini kuwa Ramona anaweza kuwa mtu hatari ndani ya kazi zao, hivyo inabidi wachukue hatua za haraka hata kama wanahisi Ramona ni mwanamke mzuri kwao.

Kutokana na ukubwa na heshima aliyokuwa nayo Ramona, ndani ya vikundi mbalimbali duniani kote, ilibidi kikao hicho kiahirishwe na kupangwa kufanyika wiki ijayo. Ambapo pia zitakuja kupigwa kura, kura zikazo amua kuwa Ramona auawe au aendelee kuwa mfanyakazi wao. Lakini kura hizo zitapigwa baada ya upelelezi mkubwa kufanyika ndani ya wiki hiyo.

Wakati huo huo kikundi cha Swaba kiliendelea kuitishia serikali ya Rais Galim Halim, kuwa siku si nyingi kinakwenda kumchinja Shazayi binti wa Rais, kwa kukitenganisha kichwa chake na kiwiliwili. Kitafanya hivyo, endapo serikali ya inchi hiyo itakuwa imeshindwa kutekeleza madai yao.

Lakini kwa kipindi hicho wapiganaji wa kikundi hicho waliendelea kumtafuta Shazayi ili wawe wamemtia mikononi mwao kiukweli si kama walivyoiongopea Serikali. Serikali pia ilitangaza dau nono endapo mtu yeyote atafanikisha kupatikana kwa binti wa rais.

Nini kitafuata usikose jumatatu

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -