Saturday, October 31, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

Ilipoishia Jumamosi

LAKINI kwa kipindi hicho wapiganaji wa kikundi hicho waliendelea kumtafuta Shazayi ili wawe wamemtia mikononi mwao kiukweli si kama walivyoiongopea Serikali. Serikali pia ilitangaza dau nono endapo mtu yeyote atafanikisha kupatikana kwa binti wa Rais.

SASA ENDELEA

HOSPITALINI

Ramona aliingiwa na wasiwasi baada ya kuona Roika hajafuata kile alichokitaka. Ingawa Roika alikuwa ameongea maneno mazuri na matamu, yanayoonyesha kuwa wao bado ni wapenzi, lakini hakutaka kushiriki kitendo cha kugusanisha ndimi. Hali hiyo ilimfanya Ramona aanze kuona kuwa, Roika hakuwa amemsamehe kwa kitendo alichokuwa amekifanya cha kujaribu kumuua.

Kwa huruma nyingi na sura iliyokuwa ikimfanya Roika siku zote amtukuze Ramona kimapenzi, ilimtazama Roika na kisha Ramona akasema.

“Roika kama hujanisamehe ninakuruhusu uniue sasa hivi.”

“Ramona hujanikosea, kilichotokea katika jumba lako la biashara ni kama ajali tu wala usifikirie kuwa mimi nililiweka suala hilo katika makosa yako. Hapana; naomba uwe huru. Najua moyo na nafsi yako vinafurahi kuniona hai kwa sababu havikuwa vimekusudia kuniua,” aliongea Roika akiwa karibu na uso wa Ramona.

“Nashukuru kwa usemacho, lakini nikuulize je, bado wanipenda,” aliuliza Ramona huku matone ya machozi yakidondoka.

Swali hilo lilikuwa gumu sana kwa Roika. Wakati akifikiria kulijibu, mwili wake ulikuwa ukitetemeka. Mapigo ya moyo wake yalikuwa yakimuenda mbio. Hakika aliogopa sana. Kwani ilikuwa ni rahisi kumjibu swali kama hilo Biyanah kuliko kumjibu Ramona.

“Ramona unajua kama nakupenda,” alijibu Roika.

“Roika mimi ninakujua toka nilipokuweka kwenye himaya ya mapenzi yangu. Nimekuwa nikiifahamu tabia yako. Leo nashtuka maana naona kabisa nafsi yako iko mbali nami.”

“Hapana Ramona moyo wangu uko pamoja nawe.”

“Au kwa sababu ya biashara haramu ninayofanya ndio unataka kuniacha. Niko tayari kuacha kila kitu kibaya ili upendo wetu uendelee kudumu milele na milele.”

Wakati Ramona akiongea hayo, moyo wa Roika ulikuwa kwenye mateso yasiyo na mfano, maana upendo wa Shazayi ulikuwa ukipigana na upendo wa Ramona ndani ya nafsi yake. Hakupenda kumuumiza Ramona hata kama moyo wake kwa muda huo ulikuwa ukimilikiwa na Shazayi binti Galim.

Wakati maongezi hayo yakiendelea Dk Sufian alikuja pale kitandani na kumsihi Roika aende akapumzike. Maana kwa muda huo ilikuwa ni saa 11: 30 alfajiri. Ramona alipopinga suala hilo daktari alimwambia kuwa akili zao wote zinahitaji kumpumzika. Lakini Dk Sufian alisema hivyo kwa kuwa, alijua mateso anayoyapata Roika juu ya wanawake watatu. Hivyo alihitaji kumuondoa maana alifahamu ni jinsi gani anaumia.

Roika alirudi chumba alicholazwa malikia mpya wa moyo wake, Shazayi binti wa Rais, Rais ambaye anahangaika yeye pamoja na serikali yake kumuokoa mtoto wake huyo  dhidi ya kikundi cha Swaba.

Alipofika pale, alimkuta Shazayi akiwa usingizini. Alimtazama sana kwa muda mrefu. Alizitazama kope za macho yake, zenye mvuto usio na mfano. Alishuka kuishangaa pua yake ndefu kidogo iliyozidi kuupendezesha uso wa binti huyo wa kiarabu.

Hakika moyo wake ulimuuliza swali ambalo akili yake ilimsuta. Kweli anaweza akamuacha mwanamke kama Shazayi? Mwanamke ambaye licha ya uzuri aliokuwa nao, alikubali kufa ili yeye apone. Akili yake ilimuuliza atapata wapi tena bahati ya kuwa na mwanamke kama huyo.

Siku hiyo ilikuwa ni siku ya maswali kwa Roika, alijiuliza ni njia ipi iliyo njema atakayotumiaa kumuacha Ramona. Nafsi yake ilipata tabu kwa suala hilo, kwa sababu, sehemu fulani ya moyo wake, ilikuwa bado inamapenzi na mrembo huyo wa dunia.

Mawazo yalizidi kuichanganya akili yake. Usingizi ukampitia akakilaza kichwa chake pembeni ya Shazayi aliyekuwa usingizini. Saa 12:30 Roika alishtuka, alipotazama kitandani hakumuona Shazayi. Aligeuka kulia kwake na kumuona akiwa amesimama dirishani. Alishangaa kuona afya yake  ikiwa imeimarika.

Alimfuata pale karibu na dirisha. Shazayi aligeuka kumtazama Roika huku akitabasamu, tabasamu zuri lenye nguvu ya kimapenzi. Roika naye alionyesha tabasamu zuri. Alimfuata Shazayi na kumkumbatia kwa nyuma.

“Za asubuhi mume wangu,” aliongea Shazayi aliyeonekana kuwa mwenye furaha isiyopimika.

“Nzuri mke wangu, siamini kama umesimama kutoka kitandani na umepata nguvu ya kutembea. Hakika Mungu ni wa ajabu,” alijibu Roika akimtazama Shazayi usoni.

“Damu ya mama yako inanguvu Roika.”

“Mmh! Kweli?”

“Hakika.”

“Nashukuru kukuona tena mbele yangu ukiwa mwenye afya njema,” aliongea Roika.

“Hata mimi nahisi furaha itokayo ndani ya moyo wangu, sasa kilichobaki ni mimi na wewe kwenda kwa baba yangu.”

“Mh! Ni kweli lakini inahitaji kujitoa.”

“Roika mpenzi wangu, usiogope baba yangu ni kama watu wengine hawezi kupinga maamuzi yangu. Amini ndoa yetu ilishapangwa na Mungu. Mwanadamu kama baba yangu hawezi kushindana na maamuzi yatokayo mbinguni.”

“Sawa kwa kuwa nakupenda nitamfanya baba yako afurahie kunipata mume bora wa mtoto wake.”

Wakati hayo yakiendelea hospitali ya Mohamed Words, nyumbani kwa Rais ndani ya ikulu, mama mzazi wa Shazayi alikuwa kwenye hali mbaya ya kiafya, hii ilitokana na tishio kutoka kwa kikundi cha kigaidi cha Swaba cha kwamba siku si nyingi kinakwenda kumchinja binti yake. Viongozi wa dini wakiwemo mashehe, walikuwa ikulu wakimuombea dua mke wa Rais aweze kupona lakini ukweli tiba yake haikuwa kitu chochote, zaidi ya kumuona mwanaye akiwa mbele yake. Huzuni kubwa ilitawala kwenye familia ya Rais. Amani ilitoweka, Rais Galim Halim alishindwa kufanya mambo mengine ya kiserikali kwa sababu ya binti yake.

Nini kitafuatia usikose kesho

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -