Wednesday, October 28, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

Ilipoishia Jana.

Watu wengi walitikisa vichwa wakiashiria kuwa Ramona ni mtu mbaya kwao.

SASA ENDELEA

Nusu nzima ya watu mle ndani waliunga mkono kuwa Ramona aliwaficha jambo hilo kwa makusudi yake maalumu, ikiwemo kujificha yeye asijulikane ni mtu wa aina gani. Viongozi mbalimbali waliokuwa wakichangia mkutano huo kwa njia ya intaneti, walisema kuwa wanahitaji jambo hilo lifikiriwe mara mbili. Wengine walimhoji Ramona kuwa kama alijua kuwa mpenzi wake ni mtu wa umoja wa mataifa, kwanini hakuwaambia.

Maongezi hayo yalimfanya Ramona kumwaga machozi. Aliona kama watu hao wamekosa imani na yeye ihali kuwa alishafanya kitendo kibaya ili kuwaridhisha. Aligonga meza, watu wote wakatulia, aliwatazama kwa sekunde kadhaa huku machozi yakimtoka.

“Sikiliza, hivi kwanini mnakosa imani na mimi? Wakati mimi nilifanya jambo baya la kumuua mpenzi wangu ili niwathibitishie kuwa nilikuwa pamoja nanyi. Hata kama sisi ni watu tofauti na jamii inayotuzunguka, lakini kila mmoja wetu anajua mapenzi nini, anajua jinsi mapenzi yanavyoweza kumkosesha binadamu raha. Kila mmoja hapa ana haki ya kupenda na ana mtu wake mahususi. Hata kama kazi yetu inatufanya tusijiingize kwenye mahusiano ya kimapenzi, lakini hiyo haimaanishi kuwa hatuwezi kupenda. Mimi nilimpenda Mr Roika kuliko mwanamume yeyote hapa duniani. Lakini nilikubali kumuua kwa sababu ninajua umuhimu wenu kwenye maisha yangu. Si kwamba niliwaogopa, la hasha ila nilitaka kuthibitisha kuwa mpo na mwanamke anayeaminika kwenye mtandao wetu ulimwenguni. Na pia sikutaka mengine zaidi yatokee juu yangu kwani nina familia ya mama na mdogo wangu wanaonipenda sana.”

Aliongea Ramona kwa machozi mengi, maneno yaliowafanya wote mle ndani kumuhurumia, hasa kiongozi wake Makx Viego. Alijifuta machozi na kisha akamalizia kwa kusema:

“Kama hamniamini tekelezeni yale mliopanga kufanya juu yangu. Maana Makx na Zahil wameshindwa kuyajua maumivu yangu baada ya kukubali kumuua mtu nimpendaye. Bado hawajaridhika nami.”

Kilio na maneno ya uchungu ya Ramona yaliwapelekea watu wengi kuinamisha vichwa chini hasa wale waliokuwa mbali na Pakistani. Kiongozi wa kikosi cha waasi cha Congo alisema kuwa hawezi kuendelea na kikao cha kumjadili Ramona, kwa kuwa haoni mashtaka ya maana dhidi mwanamke huyo. Alijizima kwenye video yake ya intaneti na kuwaachia kikao wengine. Kiongozi wa Al Shaabab Rajab Nuheek naye pia alijitoa akisema kuwa haoni sababu ya kupiga kura wala kumjadili mrembo huyo.

Baadaye kiongozi wa Swaba aliamuru kura zipigwe, kura za kumshuku au kumwamini Ramona. Lakini kiongozi wa mapinduzi nchini Yemen na muuzaji wa makombora ya Frit zic alisema kuwa, haina haja ya kupiga kura. Ila baadaye alitoa wazo na kusema kuwa Ramona kwa sasa anachotakiwa  kufanya, ni kutekeleza jambo kubwa kwa wafanyabiashara wenzake au kwa kikundi cha Swaba litakalowaaminisha kuwa yeye yupo pamoja nao na si mpelelezi wa umoja wa mataifa. Huo ndio utakuwa uaminifu mkubwa kwao na wataendelea kumthamini mrembo huyo wa dunia.

Watu wote mle ndani waliliunga mkono wazo la kiongozi huyo. Kwa kumpigia makofi na kugonga meza. Watu   wachache tu ndio waliolipinga. Kiongozi wa Swaba Zahil Bin Shaq alisimama na kusema:

“Madam Ramona tunakuamini lakini hatupaswi kuwa na hata chembe ndogo ya kutokukuamini, maana mashaka madogo kwetu ni adui mkubwa. Hivyo basi, unatakiwa ufanye kitu chochote cha kutuaminisha kuwa wewe upo pamoja nasi, upo pamoja na wafanyabiashara wetu  na upo na Swaba. Hapo utakuwa huru na utaendelea kuingiza pesa nyingi na kupata mafanikio makubwa. Na utaepuka sisi kukuundoa duniani.”

Zahil Bin Shaq aliposema hivyo, watu wote mle ndani walitikisa vichwa. Walibaki kusubiri Ramona atasema nini juu ya jambo hilo. Ukimya ukiwa umetawala watu wakiwa wanasubiri Ramona aongee, Ramona alisimama na kuuliza.

“Mnataka nifanye jambo gani?”

Viongozi wa Swaba na wale wa mtandao wa biashara waliongea maongezi yao ya chinichini na kisha wakamwachia Zahil Bin Shaq aendelee kuongea.

“Ramona unatakiwa uchague kati ya haya mawili, kutekeleza shambulio la bomu kwenye soko la Manita au kumuondoa waziri wa ulinzi Mr Hashemu Rashid.”

Ramona aliposikia hivyo moyo wake ulishtuka. Jasho jembamba lilimtoka alibaki anawatazama asijue cha kuwajibu. Alikaa muda mlefu bila kuwajibu kwa kuwa, ukiwa mmoja wa watu hao, ilikubidi uwe jasiri hata kama huna ujasiri. Kwa sekunde kumi, alikiinamisha kichwa chake chini ili kuupumzisha ubongo wake. Aliwatazama na kusema.

“Nipeni masaa kadhaa ya kulifikiria wazo hilo.”

Aliposema hivyo, wote walitikisa vichwa.  Kiongozi wa Swaba alisimama na kuahirisha kikao hicho hadi hapo baadaye.

Ramona aliingia kwenye chumba chake kilichopo ndani ya jumba hilo, huko alilia sana maana mtihani mwingine ulikuwa umepiga hodi kwenye maisha yake. Hakuwahi kufikiria kuua kwa mikono yake hasa kwa watu wasiokuwa na hatia. Japo kabla ya kujiunga na watu hao alishawahi kusema kuwa yuko tayari kufanya lolote ili kuutafuta utajiri.

Nini kitafuata usikose kesho

Samahani ndugu wasomaji, kutokana na ujio mpya wa gazeti hili, hadithi hii imekuwa ndefu kidogo hii ni baada ya ukurasa wake kufupishwa. Ila hivi punde itakwenda kumalizika. Maoni 0654076265      

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -