Wednesday, January 20, 2021

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

Ilipoishia jana

Japo kabla ya kujiunga na watu hao alishawahi kusema kuwa yuko tayari kufanya lolote ili kuutafuta utajiri.

SASA ENDELEA

Alikuwa amepewa mtihani wa kuthibitisha uaminifu wake kwao. Alikuwa amepewa kuchagua mambo mawili ya kufanya ili kuthibitisha uaminifu huo. Kwa kuwa kanuni ya mitandao hiyo ya biashara, inayoshirikiana na vikundi vya kigaidi na vya mapinduzi, inasema ulinzi wa mitandao hiyo ni kutokuwa na mashaka. Chembe ndogo ya mashaka ni adui mkubwa kwenye kikosi cha Swaba na washirika wake.

Ramona aliambiwa achague kutekeleza shambulio la bomu au kumuua waziri wa ulinzi. Lakini mambo hayo yote mawili kwake yalikuwa ni magumu, kwani hakuwahi kufikiria kuyafanya katika maisha yake. Alijikuta kwenye mtihani mwingine mkubwa, baada ya ule wa kumuua Roika kuufanikisha. Ingawa Roika hakufa,  baada ya kuolewa na Shazayi binti wa Rais saa chache kabla ya kuchomwa moto.

Ramona alilia sana pale pale alimkumbuka kipenzi chake Roika, ambaye kwa muda huo alishakuwa amenaswa na binti wa Rais aliyekuwa anakwenda kumfanya kichaa wa mapenzi siku zote za maisha yake. Baada ya kumkumbuka Roika mwanamume wa thamani ndani ya moyo wake, alimkumbuka Shazayi mwanamke ambaye anakwenda kuliua penzi lake na Roika. Ghafla alijikuta anaingiwa tena na ile roho iliyomwingia muda ule ya kutaka kumwangamiza Shazayi.

Kwa kuwa nafsi yake ilishakiri kuwa haitamwacha Roika, Ramona aliamua kumwangamiza Shazayi au kumfanya akae mbali na Roika wake. Alifikiria jambo la kufanya baadaye alikumbuka kuwa Shazayi anatafutwa na Serikali na pia kikundi cha Swaba kinamtafuta ili kiwe kimemtia mikononi kiukweli si kama kilivyoidanganya Serikali.

Baada ya saa kadhaa kupita wajumbe wote wa mkutano walikuwa wamekwisha rudi meza kuu ili kuhitimisha mkutano huo uliokuwa umeanza saa moja jioni. Mkutano uliokuwa mahususi kumjadili malkia wa silaha, Ramona Fika, mrembo wa dunia kutoka Afrika. Watu walikuwa wamekwisha kukaa kwenye viti. Wanaohudhuria mkutano huo kwa njia ya intaneti nao walishakuwa wamewasha video zao huko waliko wakisubiri mkutano uanze kwa saa kadhaa zilizokuwa zimebaki.

Ramona akiwa bado yuko chumbani, alijitazama kwenye kioo na kujiuliza maswali mengi. Alijiuliza hivi ni kweli anakwenda kuchagua uamuzi huo mgumu. Wakati akijiuliza hayo, machozi yake yalikuwa yakidondokea kwenye gauni lake lenye thamani ya shilingi milioni kumi. Lakini kila akikumbuka uzuri na mapenzi aliyokuwa nayo Roika kwake nguvu zilijitokeza na kumpa moyo wa kutotenda kusudio lake. Alijifuta machozi kwa kitambaa cheupe na kujiweka vizuri. Alifungua mkoba wake  akaitoa lipstiki nyekundu na kuiongezea kwenye midomo yake.

Watu wote wakiwa wanamsubiri yeye, Ramona alitoka chumbani na kujongea meza kuu. Alizipiga hatua kwa unyonge mkubwa hadi pale alipokwenda kukizungusha kiti na kukaa. Kiongozi wa Swaba aligongameza kuashiria kuwa mkutano ulikuwa anakwenda kuanza.  Alisimama na kumtazama Ramona, sekunde kadhaa mbele alisema.

“Ramona tunakuthamini ndio maana tumeutoa muda wetu ili kuweza kukulinda wewe na kujilinda sisi wenyewe. Tumekupa jambo moja kati ya hayo mawili ili ukatuonyesha kuwa una nguvu ya uaminifu kwetu. Tafadhali uambie ulimwengu utafanya lipi kati ya hayo?”

Baada ya kusema hayo, Zahil Bin Shaq, alikaa kwenye kiti. Kwa unyonge ule ule Ramona alisimama. Aliwatazama watu waliokuwa meza kuu na kisha akaitazama skrini kubwa iliyokuwa mbele yao iliyokuwa ikiwaonesha viongozi wengi wa vikundi vya kigaidi, waasi na wanamapinduzi wengine. Alihema kwa siri na kisha akasema.

“Sitafanya lolote kati ya hayo.”

Aliposema hivyo, watu wote waligeukiana na kuongea machache. Walibaki wameduwaa kuona Ramona anakataa uamuzi ule. Lakini kabla maongezi yao hayafika mbali aliwakatisha na kusema.

“Ila nitafanya jambo lingine, ambalo naamini mtalidhika nalo hasa kwa kikundi cha Swaba. Kwa kuwa tukio la kukamatwa kwa mpenzi wangu lilitokea ndani ya jengo hili la Swaba, mimi nitafanya jambo kwa ajili yao.”

Aliposema hivyo alitulia kwa sekunde tano na kisha alimalizia kwa kusema.

“Nitafanikisha kumpata binti wa Rais mwanamke Shazayi binti Galim.”

Aliposema hivyo, watu wote walishtuka hasa kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Swaba, Zahil Bin Shaq. Wote walitazamana na kuongea mengi kwa sauti ya chini. Zahil Bin Shaq alisimama na kumuuliza Ramona.

“Itawezekana vipi kwani unajua mahali alipo binti huyo?”

“Ninajua mliongopea Serikali ya Rais Galim Halim, kuwa mnamshikilia mwanaye. Hii ni baada ya Shazayi kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Lakini mimi nafahamu yuko wapi kwa sasa na ninaweza nikafanikisha nyie kumpata,” alijibu Ramona maneno yaliozidi kuwafanya Swaba wote waendelee kushangazwa.

“Madam unaousema ni ukweli upi, maana unanishangaza wewe Shazayi umemuona wapi?”

“Sikiliza Zahil, usihoji kuhusu mimi kumuona wapi Shazayi, bali fikiria endapo utamtia mikononi mwako mwana huyo wa Rais, ambaye takribani  wiki mbili umekuwa ukiidanganya Serikali ya Pakistani na dunia kwa ujumla kuwa unamshikilia binti huyu. Nitafanikisha wewe kumpata pasipo Serikali kujua.”

Hakika Ramona alikuwa amewashangaza sana Swaba, ambao hawakuamini kumbiwa hivyo. Kwani kwao kumtia mikononi Shazayi lilikuwa ni jambo zuri ajabu na ni tunu ya thamani kubwa. Kwani wiki mbili wamekuwa wakihenya kumtafuta Shazayi ili wawe wamemtia mikononi mwao kiukweli si kama walivyoidanganya Serikali kuwa binti huyo wanaye.

Nini kitafuatia? Usikose kesho

Hadithi hii inakupa mafunzo jinsi gani nini umejifunza kupitia simulizi hii?

Unafikiri nini hatima ya Ramona? 0654076265

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -