Friday, November 27, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU [52]

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Ilipoishia Jana

“Mimi ndio nimeamua kufa au kupona, lolote litakalokuwa, nataka Roika apone sawa, haya ingiza sindano kwenye mishipa au unataka nijitoe mwenyewe.”

SASA ENDELEA

“Madam namuogopa sana baba yako. Hivi akijua kuwa nimetekeleza zoezi la kukutoa damu unafikiri itakuwaje? Nitakuwa sina kazi mimi na huenda nitanyongwa. Nina familia ya watoto wanne na ndugu sita, wote wananitegemea. TafadhaLi muache Roika apumzike.”

“Sikiliza, siwezi kufa, lazima nitaishi. Siwezi kumuacha Roika afe, wakati mimi nipo. Unajua nimemtoa mbali sana. Kwanini afike hospitalini afe? fanya upesi nitoe damu yangu. Akifa nitakushtaki wewe kwa kumuua.”

Hakika upendo ulikuwa umeizidi akili ya kawaida ya binti huyu wa Rais. Daktari alibaki kumeza mate akijawa na woga wa hali ya juu.

Daktari hakuwa na jinsi, aliuchomeka mrija wa damu kwenye mishipa ya Shazayi na mrija huo akaupeleleka  kwenye kifaa cha kuPUnguza kasi ya damu, hadi moja kwa moja kwa Roika. Shazayi alilala pembeni ya Roika, akimtazama Roika usoni. Wakati huo Roika hakujua chochote. Macho mazuri yenye machozi, yalimtazama Roika kwa muda wote wakati damu ikisafiri pole pole, kitokea kwenye mishipa ya Shazayi kwenda kwenye mishipa ya Roika.

Kadri damu ya Shazayi ilivyozidi kumtoka, ndivyo Shazayi alivyozidi kuishiwa na nguvu. Mstari wa afya ya Roika ulizidi kugeuka na kuwa wa kijani, ikimaanisha kuwa Roika anakwenda kuwa katika hali nzuri. Baada ya dakika 15, hali ya Shazayi ilizidi kuwa mbaya, lakini alionekaNA ni mwanamke mwenye nguvu, kutokana na jinsi alivyotabasamu, pindi alipozidi kumuona mwanamume wa maisha yake, akielekea kupona. Ilishangaza sana, daktari alizidi kujiuliza ni mapenzi gani ya mtu kujitolea kufa kwa ajili ya mtu mwingine. Pia alizidi kuwa na hofu, maana mtoto wa Rais wake alikuwa akielekea kwenye hali mbaya.

Baada ya dakika nyingine 10, katika hali isiyo ya kawaida, Roika alifumbua macho. Aliangaza huku na kule na kujigundua yuko hospitalini. Mbele yake alimuona daktari. Kwa hali iliyoshangaza Roika aliweza kuongea.

“Dk nimefikaje hapa?” aliuliza Roika akimtazama daktari, huku akivuta kumbukumbu juu ya mahali alipowahi kumuona daktari huyo.

Kwa wakati huo daktari hakuwa na furaha kwa sababu mawazo yake yote yalikuwa ni jinsi atakavyokabiliwa na kesi, endapo Shazayi atapoteza maisha. Hivyo hakumjibu Roika lolote.

Roika alipogeuka upande wa kulia alipatwa na mshangao mkubwa, kumuona mwanamke. Alimtazama mkono wake uliokuwa na mrija wa damu, mrija uliokwenda moja kwa moja kwake. Moja kwa moja alijua mwanamke huyo, alikuwa akimuongezea damu. Alimtazama Shazayi usoni na kuanza kuvuta kumbukumbu juu ya mahali alipowahi kumuona mwanamke huyo. Shazayi alizidi kuishiwa nguvu. Lakini macho yake hayakuacha kumtazama Roika. Alitabasamu huku machozi yakimtoka. Kwa wakati huo Roika alizidi kuwa katika kitendawili.

Baada ya kuvuta sana kumbumbu alimkumbuka mwanamke huyo kuwa ni Shazayi mtoto wa Rais. Kwa hali isiyo ya kawaida Roika alipata nguvu za kuinuka kitandani. Haraka akauchomoa mrija wa damu ili damu isiendelee kumtoka Shazayi. Daktari alibaki ameduwa asijue nini cha kufanya. Kwa sauti ya tabu na yenye hasira Roika alimuuliza daktari.

“Kwa nini umekubali kumtoa damu unataka kumuua?”

Daktari hakuwa na jibu la haraka. Zaidi naye alianza kutokwa na machozi.

“Nakuuliza Dk nani amekuruhusu kufanya hivi?”

Roika akiwa juu ya kitanda huku akimtazama daktari kwa hasira, alishtuka baada ya kuona akishikwa mkono. Alipogeuka, alishangaa kuona Shazayi akimtazama kwa macho ya huruma, huku akitabasamu. Lakini hali yake ilikuwa mbaya.

“Roika nitazame mimi, usimtazame daktari tafadhali. Ningependa swali hilo uniulize mimi.” Aliongea Shazayi kwa tabu sana.

Kwa huzuni isiyo ya kawaida huku akitokwa na machozi mengi, Roika alilala, akamgeukia Shazayi na kuusogeza uso wake karibu naye.

“Kwa nini Shazayi unafanya hivi why Shazayi why?”

“Because, I Love you,” (kwa sababu nakupenda) alijibu Shazayi huku macho yake yakisinzia, kutoka na kuzidi kuishiwa nguvu.

“Hata kama unanipenda, hukupaswa kufanya hivi Shazayi, angalia sasa unaweza kufa.”

“Endapo utanipenda, naamini nitaishi ila kama hutanipenda nitakufa tu,”  Shazayi alijibu.

“Kuanzia sasa nakupenda, lakini kwa nini hukujali kwanza uhai wako?”

“Mimi niliamini nitaishi, lakini sikuamini wewe kwa hali uliyokuwa nayo kama utaishi.”

“Hapana Shazayi, ulichokifanya si sahihi.”

“Roika macho yangu yanakwenda kufumba sio muda mrefu, kama unanipenda, nibusu mdomoni mwangu ili nilale kwa furaha. Na mara utakapofanya hivyo, malaika watatumwa na Allah kuja kunilinda mkeo mtarajiwa maana Mungu atakuwa amekwisha shuhudia upendo wangu wa ajabu kwako.”

Maneno hayo mazuri, yaliupasua moyo wa Roika kama kuni mbichi.

Hakika Roika alizidi kuchanganyikiwa, kwani tayari yeye alishakuwa na nguvu, lakini Shazayi hakuwa na nguvu na ilionekana kuwa muda si mrefu hali ya huzuni itakwenda kutokea.

Tararibu huku machozi yakimtoka, Roika aliusogeza mdomo wake karibu kabisa na mdomo wa Shazayi, akambusu. Shazayi alitabasamu na kisha akasema.

“Thank you Roika.”(asante Roika).

Aliposema hivyo, alifumba macho.

Nini kitafuatia? usikose kesho

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -