Monday, November 23, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Ilipoishia jana

BAADA ya kuwaua walinzi hao, dereva alianza kulisogeza gari kuelekea hotelini kwa kasi. Watu waliokuwa nje ya hoteli waliokuwa wameliona tukio la walinzi wale kuuawa, nao walianza kukimbia huku na kule wengine wakirudi ndani ya hoteli.

SASA ENDELEA

Kabla wahudumu wa mapokezi hawajawataarifu polisi, wapiganaji wa Swaba walishakuwa wameshuka kwenye  gari, ambapo waliingia ndani ya hoteli na kuwaua haraka. Wageni waliokuwa eneo hilo waliamuriwa kulala chini na waliokaidi agizo hilo walipigwa risasi.

“Wote lala chini asionekane mtu anayeinua uso wala kupiga simu,” aliongea mpiganaji mmoja aliyetoka kuwaua watu wawili.

Utulivu fulani ulianza kuonekana eneo zima la mapokezi. Wageni waliokuwa vyumba vya juu bado hawakujua chochote kile kilichokuwa kikiendelea kule chini.

Mpiganaji mmoja alichukua laptop ndogo waliyokuja nayo.  Aliitazama alama nyekundu kwenye eneo ambalo wanalitafuta. Tayari laptop hiyo iliwaonyesha kuwa wamefika eneo la tukio na wamebakiza hatua chache kumfikia Ramona. Mpiganaji mmoja aliwauliza wenzake.

“Jamani si mnakumbuka madam Ramona alisema tusimuue mtu yoyote tutakayemuona na Shazayi. zaidi tumchukue Shazayi na kuondoka.”

“Hilo ni jambo muhimu ambalo tunatakiwa kulizingatia,” alijibu mpiganaji mwenzake.

Wapiganaji wanne kati ya sita, walikuwa wanajiandaa kupandisha juu kwenda kwenye chumba alicho mtoto wa Rais, Shazayi binti Galim, ambaye kwa muda huo yuko yeye, Roika pamoja na Ramona.

Hali ya sintofahamu ilizidi kutanda mle chumbani, Shazayi hakujua nini kilichokuwa kikiendelea. Tayari Roika alishajua kuwa Ramona amekwisha kuwasiliana na watu wake nao wako njiani kuja. Hakujua lengo la Ramona lilikuwa ni kutaka yeye akamatwe au Shazayi, lakini asilimia themanini, aliamini Ramona amekusudia kumuingiza Shazayi matatani. Hisia kali za hatari zilizidi kumsumbua Roika alianza kuhisi kuwa huenda watu hao walishakuwa wamewasili hotelini hapo.

Hofu kubwa ilianza kumshika Ramona, tayari alianza kuhisi kuwa huenda Roika ameshazijua njama zake. Mwili wake ulianza kutetemeka jasho jembamba lilianza kumtoka.

“Shazayi nakuomba uje kwangu,” aliongea Roika huku akimtazama Ramona usoni.

Shazayi akiwa hajui kabisa nini kilichokuwa kikiendelea, alimtazama Ramona na kisha alipiga hatua kumsogelea Roika.

“Kwani kuna nini jamani mbona siwaelewi?” aliuliza Shazayi.

“Nisamehe Shazayi sikujua kama Ramona alikuja kwa nia hiyo?”

“Nia gani niweke wazi.”

“Roika, kwani mimi nimefanya nini?” aliuliza Ramona.

“Ramona sikutegemea. Nilikuamini sana, lakini leo unataka kuniangamiza.”

“Roika sikuelewi.”

“Ramona usifikiri sijui, zaidi ya miaka saba nimefanya kazi umoja wa mataifa, nikiwa katika nchi zenye machafuko. Hebu niambie mkononi umevaa nini?” aluliza Roika.

Ramona alibaki kimya huku akilini mwake akijua tayari Roika alishakuwa amelijua dhumuni lake.

“Unashirikiana na Swaba sio?” Roika aliuliza.

“Whaaaat! Swaba?” Shazayi alishtuka, haraka alimkumbatia Roika kwenye ubavu wake wa kulia.

Roika akiwa anauliza hayo, alikuwa anabeba begi lake lililokuwa kwenye meza huku akimshika Shazayi mkono.

“Sawa naona lengo lako limetimia, lakini sikubali Shazayi apatwe na hatari.”

Roika akiwa amemshika Shazayi mkono, alianza kupiga naye hatua akitaka kutoka naye nje ya chumba walichokuwamo. Kabla hawajafika mlangoni, Ramona alifunua gauni lake na kuchomoa bastola iliyokuwa kwenye paja lake la kulia na kuwaelekezea Roika na Shazayi. Roika alipogeuka alishangaa kuona mdomo wa bastola, bastola iliyoshikwa na mrembo Ramona ukiwa unawatazama. Macho yalimtoka hakuamini ingawa alikuwa kwenye hatari. Shazayi naye alibaki mdomo wazi, hofu ilitanda, haraka akamkinga Roika kwa kumuweka mgongoni mwake. Roika hakuwa tayari kuona Shazayi yuko mbele yake, alimuweka nyuma na kumsogelea kidogo Ramona.

“Ramona unataka kunipiga tena risasi,” aliuliza Roika kwa masikitiko makubwa.

Ramona hakujibu lolote, alibaki kushika bastola kwa ujasiri wa kujilazimisha huku akitokwa na machozi mengi.

“Sawa naona mwanzoni hukuridhika sasa unataka kuniua kabisa.”

Kwa hasira na machozi mengi Ramona alijibu.

“Siwezi kukuua wewe nataka nimuue mtu anayetaka kuvuruga penzi langu. Naomba upishe mbele yangu.”

“Unataka kumuua Shazayi kwa sababu yangu. Ramona hebu fungua akili. Kwa nini ufanye jambo kama hilo?”

“Roika unajua ni jinsi gani navyokupenda. Siwezi kuwa tayari kuona mtu ninayempenda, akichukuliwa na mtu mwingine. Sikupenda kufanya jambo baya kwa mwanamke mwenzangu asie na hatia lakini upendo unaoushinda ufahamu wangu umenituma kufanya hivi.”

“Naomba utuache tuondoke tafadhari sana Ramona. Unataka Shazayi aingie kwenye mikono ya Swaba? tafadhari usiruhusu jambo hilo litokee, endapo litatokea, watu wa Pakistani watakufa na watakulaani kwa kitendo cha kumpoteza malikia wao na Mungu wao hata kusamehe.”

“Roika siwezi bila Shazayi kuangamia, penzi langu lazima litakufa tu naomba unipishe.”

Hakika Ramona alikuwa amechanganyikiwa, akijua tayari amekwisha gundulika, aliona hana budi kueleza hisia zake zilizompelekea kufanya unyama huo. Na kwa vile aliona wanataka kuondoka kabla Swaba hawajaingia mle ndani, aliwanyoshea bastola ili kuwachelewesha. Tayari alikubali Roika auone unyama wake, ambao chanzo chake ni kupenda.

“Ramona ukifanya hivyo unaweza kuharibu upendo wangu kwako uliobaki na unaoishi ndani yangu. Ni afadhali kumnusuru Shazayi asipatwe na jambo lolote baya, kuliko kunipoteza kabisa mimi. Kwani endapo Shazayi atapatwa na tatizo, naamini mimi sitakupenda milele. Ni bora tutafute  muda tukae mimi na wewe tuone ni jinsi gani ya kurudisha upendo wetu.”

Maneno ya Roika yalianza kupunguza hasira ya Ramona, taratibu alianza kuushusha mkono wake chini mkono uliokuwa na bastola.

Nini kitafuatia usikose alhamisi    

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -