Thursday, October 29, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

Ilipoishia Jumanne

Maneno ya Roika yalianza kupunguza hasira ya Ramona, taratibu alianza kuushusha mkono wake chini, mkono uliokuwa na bastola.

SASA ENDELEA

Mwili wake ulishtuka, hisia kali juu ya Roika zilianza kuupozesha moyo wake wenye hasira. Taratibu alishusha bastola yake chini huku akitokwa na machozi mengi. Kwa uchovu wa hali ya juu alikaa kwenye kiti. Aliinua uso wake kuwatazama Roika na Shazayi, ambao walikuwa makini kumtazama yeye.

“Kila siku maisha yangu yanabadilika. Najikuta nafanya makosa. Lakini kosa ambalo sitalifanya kamwe ni kukuacha wewe Roika. Usifikiri nimeridhia wewe kuwa na Shazayi,” aliongea Ramona huku akilia sana.

Mkono wake uliokuwa unatetemeka, uliiangusha bastola chini.

Wakiwa wanamsikiliza Ramona kwa huzuni, kwa mbali Roika alisikia kishindo. Alimshika Shazayi mkono kisha akamwambia Ramona.

“Tutaonana wakati mwingine.”

Aliposema hivyo, alifungua mlango, wakatoka nje na Shazayi na kumwacha Ramona pale ndani akiendelea kulia. Kelele za watu zilisikika ngazi ya pili kutokea chini. Hofu ilitanda kwao, Roika aliamini kwa muda huo tayari Swaba walishakuwa wameivamia hoteli hiyo na wako njiani kupandisha ngazi za kuja juu. Roika alimtazama Shazayi kisha akamwambia.

“Usiogope hakuna baya litakalokukuta.”

“Siogopi kwani nimejivika moyo wako wa ujasiri,” alijibu Shazayi.

Wakati huo wapiganaji wanne walikuwa ngazi ya pili, wakipiga hatua za haraka kuja ngazi ya tatu ili waifuate ya nne, ambako huko ndiko kuna alama nyekundu, wanayoiona kupitia laptop yao. Wageni waliokuwa wanatoka kwenye vyumba vyao na kupiga kelele walikuwa wanauawa mara moja.

Roika alihitaji umakini mkubwa ili aweze kumwokoa Shazayi. Kwani tayari alikwishakujua kuwa kikundi cha Swaba kimekwisha kuingia hotelini hapo. Alijua akifanya kosa dogo na kushindwa kutoka naye hotelini hapo, basi Shazayi atakuwa mali yao. Aliona ni kheri akamatwe au kuuawa yeye kuliko Shazayi. Hakuwa na nia ya kumuokoa Shazayi kwa sababu anampenda tu, bali kwa sababu watu wa Pakistani wanamuhitaji mwanamke huyo mwenye thamani kubwa kwa nchi yao.

Wakati huo mkanda wa video kutoka kikundi cha Swaba, ulitoka ukiendelea kutoa maneno ya vitisho na jeuri. Mkanda huo ambao ulitangazwa kupitia taarifa za habari duniani kote, ulikuwa umetolewa muda mfupi baada ya wapiganaji wa Swaba kuwa wameondoka kwenda kumkamata Shazayi na wakijua asilimia zote kuwa wana kwenda kumchukua malikia huyo. Swaba walisema, yamebaki masaa kadhaa ili kumchinja binti wa Rais.

Taarifa iliyopatikana kutoka ikulu ilisema kuwa Rais Galim Halim anatarajia kutoa hotuba itakayokwenda kukubali kile Swaba wanachokitaka. Nusu nzima ya watu wake wa serikali, waliridhia juambo hilo. Ingawa ilikuwa ngumu kuwapa Swaba kile wakitakacho, lakini ilibidi kufanya hivyo kwa kuwa mke wa Rais mama mzazi wa Shazayi, alikuwa kwenye hali ambaya ambapo muda wowote angepoteza maisha.

Rais Galim hakuwa tayari kumpoteza binti yake pamoja na mke wake. Hata raia wa Pakistani waliunga mkono jambo hilo. Walisema ni bora awape Swaba kile wanachokitaka. Taarifa hiyo kutoka ikulu, zilikuwa njema masikioni pa Swaba ambao waliamini saa chache zijazo wanakwenda kusheherekea ushindi wa kupata eneo la Ramadan Kash eneo lenye asilimia 40 ya uchumi wa nchi hiyo.

Roika alitazama chini na kuwaona wapiganaji wakiwa wamevaa magwanda meusi na vitambaa usoni, wakipanda kuja juu. Hofu ilizidi kutanda, ukizingatia hawakuwa na silaha yoyote. Ilibidi upesi wagonge chumba cha mgeni mwingine, ambaye alifungua na kuwauliza

“Niwasaidie nini?

Lakini Roika na Shazayi waliingia ndani ya chumba hicho pasipo kuruhusiwa. Mgeni huyo aliyekuwa mzungu kutoka uingereza, aliwashangaa kuingia kwake pasipo kuruhusiwa.

Jibu alilojibiwa lilimfanya kuogopa.

“Ukitoka tu nje unauawa. Kuna watu wabaya wamevamia hoteli wanaua mtu wanayemuona mbele yao,” aliongea Roika akitazama huku na kule ndani ya chumba hicho.

Hofu ilimuandama mzungu huyo aliyekuwa na mtoto wake hotelini hapo.

Kelele za watu wanaopigwa risasi ziliendelea kusikika. Roika alimuuliza mzungu huyo kama alikuwa na silaha.

“Nina bastola hata hivyo ina risasi nne tu,” alijibu mzungu huyo kwa lugha ya kingereza.

“Sawa ninaiomba.”

Mzungu huyo alifungua begi lake na kumpa Roika bastola. Shazayi alizidi kupatwa na hofu.

“Unataka kupigana nao?” aliuliza Shazayi.

“Hapana ni kujilinda tu kwa muda huu,” alijibu Roika.

Wakati huo tayari wapiganaji wa Swaba walishakuwa wamezifikia ngazi za nne. Alama nyekundu iliyokuwa kwenye laptop yao, ilionesha kuwa tayari walikuwa wamelifikia eneo alilokuwepo Ramona. Hatua tano zilibaki. Moja kwa moja walijua Ramona atakuwa chumba namba saba ambacho kilikuwa mbele yao. Haraka walifungua mlango huo na kuingia ndani.

Walipofika ndani, walimkuta Ramona akiwa ameinama, akiwa mwenye huzuni. Walishusha silaha zao chini. Upesi mmoja wao alimfuata Ramona na kumuuliza.

“Madam yuko wapi Shazayi mbona hatumuoni.”

“Wametoka sasa hivi baada ya kugundua njama zangu. Fanyeni hima wasije toka nje ya hoteli,” alijibu Ramona huku akitokwa na machozi.

Walipoanza kutoka nje haraka, Ramona aliwaambia.

“Ila tafadhalini sana naomba msimuue mwanamume aliyekuwa naye, wala msimkamate.”

“Sawa madam.”

Walitoka nje haraka na kuanza kukagua vyumba vyote vya ngazi ya nne. Waliwapigia simu wenzao wawili waliokuwa eneo la chini la mapokezi na kuwauliza kama kuna mwanamke na mwanaume wamefika kule chini.

“Sisi tuko makini huku chini na nyie fanyeni kazi huko juu. Vipi hamjampata?” Mmoja wa wapiganaji wa kule chini aliuliza.

“Wametoka ndani ya chumba walichokuwapo na madam. Tuko njiani tukipita chumba baada ya chumba.”

Nini kitafuatia, usikose kesho.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -