Wednesday, November 25, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Ilipoishia jana

Njia hiyo ilikuwa ni ya matumaini kwao. Kwani Roika aliamini kuwa lazima wapiganaji wa Swaba watakuwa kule chini hivyo mbinu hiyo itawasaidia.

SASA ENDELEA

Saa 12:05 basi la shule ya Jabir International liliwasili katikati ya mtaa wa Alisun. Mtaa huo uliokuwa na majengo mengi ya wakazi waliopanga, ulikuwa umezungukwa na majengo yenye ghorofa saba.

Tayari watoto walishakuwa wamevaa sare za shule. Wenyeji wa nyumba hiyo, watu waliowapokea Roika na Shazayi, walishakuwa wamewaandaa watoto wao. Shazayi alishakuwa amevaa hijabu na nikabu ili kuificha sura yake.

Lakini mama mwenyeji wa nyumba hiyo, alimshauri Roika kuvaa nguo za kike. Na pia alimtaka Shazayi kubadilisha gauni alilokuwa amelivaa na badala yake avae baibui. Roika alivaa baibui na kujifunga nikabu na hijabu na kuonekana kama mwanamke na mwenyeji wa maeneo hayo. Roika alipomaliza kuvaa hivyo, Shazayi alicheka na kumtania.

“Umependeza, unatakiwa uwe unavaa hivi kila siku.”

“ Nitakupiga, nani awe anavaa hivi?” aliongea Roika huku akicheka akitishia kumpiga Shazayi.

Baada ya hayo, Roika aliwaaga wenyeji wa nyumba hiyo na kuwashukuru sana. Aliwaahidi siku moja kurudi kuja kuwalipa fadhila.

“Nitatangulia kutoka mimi pamoja na mtoto mmoja na wewe utafuata nyuma na mtoto mwingine,” aliongea Roika jambo ambalo liliungwa mkono na wenyeji.

Roika alitoka nje na mtoto wa kike ambapo alimshika mkono na kushuka naye ngazi kutoka ghorofa ya saba hadi chini. Baada ya Roika kufika chini, Shazayi naye alianza kupiga hatua kushuka chini akiwa na mtoto wa kiume. Nje kulikuwa na utulivu mkubwa ingawa kulikuwa na kelele za watoto wa nyumba za jirani, ambao nao walikuwa wakilikimbilia basi. Roika alitembea taratibu kulifuata basi la shule. Alipogeuka kushoto, hatua kumi mbele, aliwaona wapiganaji wa Swaba wakiwa nje ya gari lao, wakiwa na bunduki. Usoni walikuwa wamejifunga vitambaa vyeusi kwa kuacha macho tu.

Kwa kiasi kikubwa aliogopa sana. Alianza kumwomba Mungu kimya kimya, awafanikishe kuondoka hapo kabla wapiganaji hao hawajagundua chochote.

Wazazi wengi walikuwa wakitoka na watoto wao kuwapeleka kwenye basi la shule. Wakazi wengi wa eneo hilo, walijawa na uwoga mkubwa, kutokana na kuwepo kwa wapiganaji hao pale mtaani. Walishindwa kufanya chochote kwa kuhofia maisha yao, huku watu wengine wakijua  kuwa watu hao walikuwa ni polisi. Lakini uvaaji wa watu hao ulikuwa si wa kawaida. Watu wanaowafahamu kupitia taarifa za habari na mitandao, walishajua kuwa watu hao ni wapiganaji wa kikosi cha kigaidi cha Swaba.

Roika aliingia pamoja na mtoto ndani ya basi. Alibaki kumsubiri Shazayi aliyekuwa njiani kuja. Mwili wake ulikuwa ukitetemeka pindi alipokuwa akigeuka kwa siri kuwatazama wapiganaji hao. Mara kwa mara alikuwa akigeuka kutazama mlango wa jengo alilotoka, kuona kama Shazayi anakuja. Wakati huo wapiganaji wa Swaba walikuwa wakitazama huku na kule kuona kama kuna dalili zozote za Shazayi na Roika kuwapo maeneo yale. Mpiganaji mmoja alimtazama sana mwanamke aliyeingia kwenye basi la shule.

Punde Shazayi alikuwa akitoka kwenye mlango wa jengo  akijongea kuja kwenye basi akiwa na mtoto.  Alipowaona Swaba, mapigo ya moyo wake yaliongezeka, jasho jembamba lilimtoka alihema kwa siri. Aliongeza hatua za haraka kidogo. Wakati huo Roika alikuwa akiomba  wawepo wazazi wengine, wanaondoka na basi hilo la shule, maana aliona wakiwa yeye na Shazayi peke yao, wapiganaji hao, watashtuka pindi watakapoona basi hilo linawatoto wengi na watu wazima wawili.

Shazayi aliingia kwenye basi hilo na kukaa kiti kilichokuwa mbali na Roika. Mpiganaji mmoja aliwauliza wenzake.

“Hivi wenzangu hamna mashaka na wale wanawake walioingia kwenye basi la shule?”

Wale watatu wengine waligeuka kutazama kule kwenye basi, walipoanza kuonyesha mashaka, bahati nzuri wanawake wengine wawili walikuja na kuingia pamoja na watoto wao ndani ya basi.

“Hapana, achana na hilo basi wala hakuna kitu,” aliongea mpiganaji mmoja akiendelea kutazama sehemu nyingine.

Muda mfupi mwalimu wa shule ya Jabir alipoona watoto wamekwisha kuingia kwenye basi, aliwauliza wanafunzi wake.

“Jamani kuna mwenzenu hajaingia kwenye basi?”

“Tupo wote mwalimu,” walijibu watoto wote kwa pamoja.

Mwalimu alimruhusu dereva kuondoa basi kuianza safari. Basi la shule ya Jabir International liliondoka mtaani hapo bila wapiganaji wa Swaba kushtuka kuwa ndani ya basi hilo, kulikuwa na binti wa Rais Shazayi binti Galim.

Liliingia barabara kubwa ya mji wa Nuruwan likiianza safari ya kuelekea mjini Islamabad. Roika alikuwa akigeuka mara kwa mara kutazama nyuma ili kuona kama wapiganaji wa Swaba, wanakuja, lakini haikuwa hivyo, mbinu yao ilikuwa imefanikiwa vema.

Basi lilipofika mwanzoni mwa mji wa Islamabad, Roika na Shazayi walishuka, ambapo walichukua taksi na kuomba iwapeleke hotelini. Dereva wa taksi hiyo, aliwapeleka hoteli iliyokuwa karibu na barabara ya kwenda mji wa Masjid, ambako huko kuna ikulu ya Rais. Baada ya dakika 15, Roika na Shazayi walikuwa wamefika hotelini hapo, ambapo walichukua chumba cha ghorofa ya pili.

Shazayi alimkumbatia Roika na kulia sana kwenye kifua chake. Roika alimfuta machozi na kumbusu. Nguvu ya mapenzi ilikuwa kubwa kwa wawili hao. Roika aliamini bila Shazayi hawezi kuishi na Shazayi aliamini bila Roika hawezi kuishi. Siku hiyo Shazayi alivaa vizuri, hakika alipendeza na kuonekana si mwanamke wa kawaida. Roika naye alivaa suti nyeusi zilizomfanya kuonekana mwanamume wa tofauti.

Muda wa kwenda ikulu ya Rais Galim Halim ulikuwa umefika.

Nini kitafuatia, usikose Alhamisi.   

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -