Sunday, November 29, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Ilipoishia jana

Rais Galim alionekana kuchanganyikiwa, bado hakuwa na nguvu ya kuamini taarifa za mwanawe kuja ikulu.

SASA ENDELEA

Rais Galim alibaki na sintofahamu, mara nyingi sana alijiuliza ni taarifa halisi au alikuwa ndotoni. Taarifa za kuja ikulu kwa mwanawe zilikuwa ni kama simulizi ya hadithi za watoto. Alijiuliza inawezekana vipi, wakati binti yake yuko mikononi mwa Swaba. Wakati akijiuliza hayo, simu ya mezani ilikuwa ikiendelea kuita. Aliipokea na kuiweka sikioni kwa woga.

“Haloo,” aliongea Galim.

“Mheshimiwa tayari vikosi viwili vya jeshi vinasogea ikulu kumlaki madam Shazayi,” aliongea mkuu wa majeshi.

“Ni kweli mwanangu anaingia ikulu?”

“Ni kweli mheshimiwa, kwani hujapata taarifa?”

“Ndio nimepata lakini sikuziamini mara moja.”

“Ni taarifa za kweli mheshimiwa.”

“Sawa kama ni hivyo, basi nitaomba ulinzi uimarishwe kuanzia mwanzo wa Masjid,” aliongea Rais Galim.

“Sawa mheshimiwa ondoa shaka.”

Baada ya kuongea hayo na mkuu wa majeshi, taratibu aliiweka simu mezani huku akiwa na nguvu hafifu za kuamini taarifa hizo. Lakini alipiga magoti na kusujudu mara nyingi na kisha alisema.

“Na iwe hivyo.”

Aliposema hivyo, aliinuka na kutoka ofisini kwake, ambapo alipiga hatua kuelekea nje ya jengo la ikulu. Mapigo ya moyo yake yaliendelea kumpiga kwa haraka pasipo kujizuia. Alipofika nje ya ikulu, alikuta polisi wa idara yote ya ulinzi, wakiwa wamejipanga kila mahali na wengine kwenye mistari. Hakika alizidi kustaajabu.

Roika na Shazayi wakiwa ndani ya taksi, waliendelea kusogea taratibu wakilikaribia eneo la ikulu. Wakiwa njiani, tayari magari mengi ya jeshi yalishakuwa nyuma yao. Roika aliposhtuka kuhofia labda ni wapiganaji wa Swaba, Shazayi alimwambia.

“Usihofu hili ni jeshi la nchi yangu.”

Magari mengi ya jeshi yaliwapita na kusogea ikulu kabla yao. Yalipofika, wanajeshi wengi walishuka na kujipanga kwenye gwaride. Rais Galim alizidi kushangaa. Moyo wake ulikuwa na shauku isiyoelezeka ya kutaka kumuona mwanawe. Alijiuliza wema wa Swaba wa kuamua kumuachia mwanaye kabla hajawakabidhi kile wanachokitaka, ulikuwa umetoka wapi. Alisubiri kuona muujiza wa kwanza kwenye maisha yake.

Eneo lote la ikulu lilikuwa ni tulivu sana, ukimya mkubwa ulikuwa umetawala. Ndege za kivita zilishatumwa angani kwa ajili ya kuimarisha ulinzi. Mji wote wa Masjid ulitawaliwa na ulinzi mkali, ndege zilizunguka anga lote la mji huo. Wakazi wa mji huo walianza kuogopa wakijua labda kuna uvamizi umeingia. Kwa mbali Rais Galim aliiona taksi ikiingia kwenye viunga vya ikulu. Macho yalimtoka vilivyo alianza kuona kuwa si ndoto bali ni kweli.

Taksi ilisimama mara tu ilipofika mbele ya jengo la ikulu. Roika alimtazama Shazayi aliyekuwa akitokwa na machozi mithili ya mafuriko. Macho yaliojaa upendo wa ajabu yalimtazama Roika aliyekuwa akitabasamu. Upesi Shazayi alimkumbatia Roika, wote wakiwa ndani ya taksi.

“Asante sana Roika, na sasa namuona baba yangu,” aliongea Shazayi.

“Nenda ukamuone baba yako,” aliongea Roika.

“Tushuke wote.”

“Hapana nafikiri baba yako anahamu ya kukuona kwanza wewe. Shuka akauone.”

Shazayi alitabasamu, taratibu alifungua mlango na kushuka kwenye gari. Vikosi vyote vya majeshi na vile vya idara ya ulinzi, upesi vilipiga saluti. Kiongozi wa gwaride alipaza sauti kuu kuviamrisha vikosi vya jeshi kutoa heshima zote.

Rais Galim alibaki kushangaa, bado hakuamini, ingawa macho yake mawili yalikuwa yakimuona mwanaye akija mbele yake. Machozi yalianza kumtoka, taratibu naye alianza kumsogelea binti yake huku akijawa na uwoga uliokuwa umeambatana na furaha.

Hatimaye Rais Galim alimshuhudia mwanaye akiwa mbele yake.

“Mwanangu,” aliongea Galim.

“Baba,” aliitikia Shazayi.

“Ni wewe mwanangu.”

“Ni mimi baba wala hujakosea.”

Galim alimkumbatia mwanaye kwa nguvu, Shazayi naye alimlaki baba yake kwa furaha isiyoelezeka. Kwa mara ya kwanza Rais Galim alitokwa na machozi mengi. Kumuona mwanaye kwake ulikuwa ni muujiza wa kwanza kutendeka kwenye maisha yake.

“Inawezekana vipi,” aliuliza Galim.

“Baba ni hadithi ndefu iliyoambata na msamaha,” alijibu Shazayi kwa machozi.

Baadae aligeuka kumtazama Roika aliyekuwa ndani ya taksi, aliyekuwa mwenye furaha pindi alipokuwa akiwaona mtu na mtoto wake wakikumbatiana kwa furaha. Shazayi akiwa amemshika baba yake mkono, aliendelea kumtazama Roika. Aliinyosha mkono kuonyesha ishara kuwa alikuwa akimuhitaji asogee kwao.

Roika alifungua mlango wa gari na kushuka. Alitembea hatua chache hadi mbele yao kidogo. Kwa heshima aliinamisha kichwa chini. Rais Galim alibaki kumshangaa.

“Baba anaitwa Roika nakuomba umkaribishe ndani kwani nina mengi ya kukuambia kumuhusu yeye,” aliongea Shazayi kwa tabasamu.

“Karibuni,” alijibu Rais huku akinyosha mkono kuelekeza ndani.

Aliwasindikiza hadi ndani na kuwapeleka meza kuu.  Baada ya hapo aliwaomba kutoka kidogo. Alielekea ofisini kwake ambapo alimuita mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama pamoja na mkuu wa jeshi la polisi.

“Binti yangu amepatikana, na sijajua imekuwaje ametoka kwenye mikono ya Swaba. Sasa nitaomba ulinzi uimarishwe nje ya ikulu,” aliongea Rais Galim.

“Sawa muheshimiwa, Lakini hata mimi imenishangaza, kuna jema kweli?”

“Hata mimi Napata uwoga ila ngoja niongee kwanza na binti yangu. Ili  nijue ilikuwaje,” alijibu Rais Galim.

Baada ya maongezi hayo Rais Galim alirudi sebureni. Wahudumu wa ikulu walikuwa wakichangamka kuandaa vinywaji. Kabla ya yote, Rais Galim alimhitaji Shazayi waende chumbani alikolala mke wake.

“Mr Roika nitaomba utusubirie kidogo,” aliongea Rais Galim.

“Haina shaka,” alijibu Roika kwa tabasamu.

Walipofika chumbani Shazayi hakuamini kumuona mama yake akiwa kwenye hali mbaya. Kwa wakati huo mama yake alikuwa usingizini.

Nini kitafuatia, usikose kesho.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -