Sunday, November 29, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Ilipoishia jana

WALIPOFIKA chumbani, Shazayi hakuamini kumwona mama yake akiwa kwenye hali mbaya. Kwa wakati huo mama yake alikuwa usingizini.

SASA ENDELEA

Kwa Shazayi ilikuwa ni kama ndoto, kwani hakuamini haraka kumwona mama yake akiwa amedhoofika mwili kiasi kile. Hakika ilimshangaza sana, alimtazama baba yake mara kadhaa na kumgeukia tena mama yake. Sura yake ilikuwa imetawaliwa na maswali mengi juu ya hali aliyonayo mama yake. Machozi mengi yalianza kumbubujika. Apumua kwa tabu huku akimsogelea mama yake pale karibu kabisa na kitanda.

“Baba nini kimemkuta mama. Anaumwa nini ?” aliuliza Shazayi huku akilia sana.

Kwa masikitiko makubwa Rais Galim alimjibu binti yake.

“Mwanangu, ujio wako unaweza kuokoa maisha ya mama yako. Maana alianza kudhoofika siku ile tu, aliposikia wewe kuwa uko mikononi mwa Swaba. Hakuna ugonjwa unaomsumbua, madaktari wamelithibitisha hilo.”

Kilio cha Shazayi kilimfanya mama yake kufumbua macho.  Sauti ya mwanaye, alikuwa ameisikia kutoka usingizi. Taratibu na kwa tabu, mama yake alifumbua macho. Salma hakuamini kumuona mwanaye mbele yake, alihisi labda alikuwa ndotoni. Macho yalimtoka alibaki kushangaa.

“Mama ni mimi mwanao Shazayi.”

“Shazayi mwanangu,” alijibu Salma huku akizidi kupigwa na bumbuwazi.

Aligeuka kushoto na kumuona mume wake. Rais Galim alitabasamu na kumwambia.

“Amini, mwanao amekuja.”

Upesi aligeuka tena kumtazama binti yake aliyekuwa akitokwa na machozi mengi.

“Mama,” aliita tena Shazayi.

“Shazayi mwanangu, umekuja ni wewe?” aliuliza Salma huku akitokwa na machozi ya furaha.

Shazayi alijilaza kwenye kifua cha mama yake. Salma alimshika binti yake ili kuhakikisha kuwa si mzimu bali alikuwa ni mtoto wake halisi. Kilio kilikuwa ni kikubwa kwa mke wa Rais mama Salma Galim. Taratibu nguvu zilianza kumjia kitu ambacho kilimshangaza sana muheshimwa Galim.

“Mwanagu Shazayi naomba uniletee chakula njaa inaniuma,” aliongea Salma kauli iliyozidi kumshangaza Rais Galim na kumpa furaha isiyopimika.

Upesi Shazayi alitoka chumbani na kuelekea jikoni ambako aliwakuta wahudumu watano wakiandaa chakula.

“Bila shaka chakula cha mama kiko tayari,” aliuliza Shazayi.

“Ndio madam.”

“Tafadhari nipeni upesi.”

Shazayi alichukua supu ya kuku iliyochanganywa na viazi pamoja na matunda ya mizabibu. Ni chakula kilichokuwa kikipendwa sana na mama yake. Upesi alikipeleka  chumbani na kuanza kumlisha mama yake. Ilizidi kumshangaza Rais Galim, baada ya kuona mke wake akila chakula bila shida yoyote. Alitabasamu, huku akijifuta machozi.

Alitoka chumbani na kuelekea kwenye chumba chake maalum ambacho ni chumba cha swala. Alisujudu mara nyingi na kulia mbele ya Mungu, akimshukuru kwa kuikoa familia yake iliyokuwa ipotee mara moja.

Baada ya swala ya shukurani, alielekea sebureni walikokuwa wamemuacha Roika. Aliketi kwenye kiti na kumtazama sana Roika. kitendo kilichomfanya Roika  kujawa na uwoga.

“Umetoka wapi na binti yangu?”

Swali hilo lilikuwa gumu kwa Roika, kwani hakuwa amelijua lengo la Rais na kile alichokuwa akifikiria. Roika hakujibu, zaidi aliinamisha kichwa chini.

“Usiogope, Shazayi yuko chumbani pamoja na mama yake. Ujio wake umeweza kuokoa maisha ya mke wangu, kwani alikuwa kwenye hali mbaya kutokana na kumuwaza binti yake. Nieleze wala usinifiche jambo lolote.”

“Muheshimiwa, najua utakuwa ukijiuliza maswali mengi, imekuwaje binti yako ametoka kwenye mikono ya Swaba je Swaba wameamua kumuachia? Lakini ukweli ni kwamba, mwanao hakuwa akishikiliwa na Swaba.”

“Whaaat! Una maana gani?”

“Swaba walikutangazia wewe na serikali yako kuwa wanamshikilia mwanao, lakini ukweli ni kwamba walikuongopea.”

“Waliniongopea, kivipi?”

“Ni hadithi ndefu kidogo muheshimiwa, ila itategemea kama utahitaji kunijua mimi ni nani?”

“Nieleze kila kitu, tafadhari Mr Roika.”

“Mimi naitwa Roika Malino nafanya kazi umoja wa mataifa (UN),” aliongea Roika kwa umakini mkubwa.

Lakini mara tu Roika alipojitambulisha, Rais Galim alikumbuka kitu.

“Samahani hebu subiri,” aliongea Galim.

Alisimama pale kwenye kiti na kuelekea kwenye kabati la vitabu. Alichukua jarida la The century Human. Jarida hilo lilikuwa limewazungumiza vijana watatu, vijana waliofanya vitu vikubwa na wenye mvuto kwa watu. Rais Galim alikuwa amelihifadhi jarida hilo kutokana na mwanaye Shazayi naye kutajwa kwenye jarida hilo la The Century Human.

Ukurasa wa mbele wa jarida hilo, ulikuwa umepambwa na picha mbili, zilizokuwa zimelipamba jarida hilo maarufu duniani. Picha ya kwanza ilikuwa ni ya Roika Malino na picha ya pili ilikuwa ni Shazayi Galim Halim. Jarida hilo lilimtaja Roika kama ni mtu anayejali uhitaji wa watu masikini, wakiwemo watoto na wanawake wanaoishi kwenye mazingira ya vita na magonjwa. Mtu anayemiliki vituo vingi vya kulea watoto yatima na wazee. Licha ya kipato kidogo alichokuwa nacho, pia alikuwa akimiliki  hospitali mbili kwenye nchi tofauti.

Vile vile jarida hilo lilimtaja Shazayi kuwa ni mtoto wa Rais mwenye mvuto kwa watu, miongoni mwa watoto wengi wa marais hapa duniani. Ni mwanamke mwenye msaada mkubwa kwa watu wasiojiweza.

Lengo la Rais Galim  kununua jarida hilo, lilikuwa ni kumkumbuka mwanaye, kwani kipindi jarida hilo linatoka, Shazayi tayari alishakuwa amepotea.

RAMONA

Ramona alikuwa kwenye kilio kikubwa, kilio ambacho aliamini yeye mwenyewe ndiye aliyekisababisha. Hakutamani kula wala kunywa chochote, maana alijua kuwa anakwenda kumkosa Roika, mwanaume mwenye mvuto kwenye moyo wake. Pia alishajua  kuwa maisha yake yanaweza kuwa hatarini kutokana na kushindwa kufanikisha kukamatwa kwa Shazayi. Lakini alichokifikiria sana ni kwamba, Swaba hawatataka tena kumuona akifanya kazi kwenye mtandao wa biashara, mtandao unaoshirikiana na wao.

Nini kitafuatia usikose jumatatu

Je nini hatima ya mrembo wa dunia Ramona Fika? 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -