Wednesday, November 25, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Ilipoishia Jumamosi

LAKINI alichokifikiria sana ni kwamba, Swaba hawatataka tena kumwona akifanya kazi kwenye mtandao wa biashara, mtandao unaoshirikiana na wao.

SASA ENDELEA

Ramona alishakuwa amekata tamaa. Huzuni na majonzi vilimfanya kujiona ni mwanamke asiye na thamani. Alianza kuyachukia mapenzi kwani ndiyo yaliyokuwa yamemfikisha hapo. Alijuta kwanini Roika alikuja kwenye maisha yake, maana bila Roika asingeuharibu uhusiano wake na watu wake wa biashara.

Alijilaumu kumpenda Roika, kwani leo anakwenda kuachwa, ihali kuwa bado anampenda. Aliona ni bora angekosa kazi, lakini mapenzi na Roika yaendelee kusimama. Lakini leo anakosa kila kitu, anamkosa Roika na pia anaikosa kazi yake, kazi inayomuingizia mamilioni kila inapoitwa leo. Alilia sana mrembo huyu wa dunia kutoka Afrika.

Wakati huo huo taarifa mbaya ilifika kwa kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Swaba Zahil Bin Shaq, kuwa mtoto wa Rais Shazayi binti Galim, amefika ikulu. Taarifa hiyo, alipewa kutoka kwa mtu wao anayefanya kazi kama askari wa jeshi la polisi. Hakika Zahil na viongozi wake walichanganyikiwa juu ya taarifa hiyo.

Taarifa nyingine ilikuwa ni juu ya wapiganaji wao wawili waliouawa kule hoteli ya Free Pakistan Embassy. Askari huyo alimwambia Zahil kuwa mmoja wao ni mzima na mwingine amefariki. Hivyo huyo mzima tayari yuko mikononi mwa serikali akifanyiwa matibabu. Serikali inasubiri apone ili aweze kutoa taarifa kuhusu wao.

Zahil alichanganyikiwa, ilibidi ajitahidi kuzituliza hasira zake ili aweze kufanya jambo la msingi. Baadae aliwapigia simu wapiganaji wale wanne waliokuwa mtaa wa Alisun na kuwahitaji kurudi kwani, Shazayi alikuwa amekwisha fanikiwa kurudi ikulu. Siku hiyo hiyo, Zahil aliitisha mkutano wa ulimwengu, ambao uliwakutanisha wao na mtandao wa biashara pamoja na viongozi wa vikundi mbalimbali.

Makx Viego alitaka kumpigia simu Ramona ili aje kuhudhuria mkutano huo, lakini Zahil alimwambia asimpigie kwanza. Mkutano huo ulianza saa nane usiku na ulitegemea kufanyika kwa masaa mengi.

IKULU

Lengo la Rais Galim  kununua jarida hilo, lilikuwa ni kumkumbuka mwanaye, kwani kipindi jarida hilo linatoka, Shazayi tayari alishakuwa amepotea.

Roika alishangaa kuona Rais Galim, analiweka jarida  mezani. Alilichukua na kulitazama, alistaajabu kujiona yeye akiwa mbele ya  jarida hilo, akiwa pamoja na Shazayi. Pale pale alikumbuka kuwa, waandishi wa jarida hilo la The Century Human, walishawahi kumuita akahudhurie mkutano wao nchini Marekani, ambapo walichukua habari nyingi zinazomhusu yeye. Hiyo ilikuwa ni kabla ya kuja Pakistani.

“Waandishi wa jarida hili nilishawahi kuwapa habari zangu. Nao waliyafuatilia maisha yangu,” aliongea Roika.

“Inamaana wewe na mwanangu mmefahamiana kupitia jarida hili?” Rais Galim aliuliza.

“Hapana, nadhani hata Shazayi toleo la jarida hili halikumfikia, kwani ndio muda aliokuwa amepotea. Hata mimi ndio naliona sasa.”

“Ni kweli, mwanangu hajaliona. Sasa wewe na mwanangu mlikutana wapi? Maana mimi uliponiambia unaitwa Roika Malino, nikakumbuka kuwa nilikuona kwenye jarida hili.”

“Kwa mara ya kwanza mimi na mwanao tulikutana hospitali ya Mohamed Words, nilipokuwa nimekwenda kuwatembelea watoto waliokumbwa na shambulio la bomu.”

“Ni kweli hata mwanangu alikuwa anapenda sana kuwatembelea watoto hao na aliwasaidia kwa kiasi kikubwa. Bila shaka unatabia kama ya mwanangu au ulikuwa unatimiza kazi yako kama  mfanyakazi wa UN?”

“Hapana muheshimiwa, licha ya kutimiza kazi yangu, mimi ni mtu ninayejali maisha ya watu wengine, kama navyojijali mimi mwenyewe. Ndio maana jarida hili, lilipenda kuandika habari zangu.”

“Nakupa hongera kwa hilo Mr Roika. ila ilikuwaje mwanangu akapotea na umesema hakuwa akishikiliwa na Swaba?”

“Kwanza nisamehe mimi, pia msamehe  na mwanao. Ukweli ni kwamba nilipokuwa kwenye kazi yangu kama mwakilishi wa UN, nilipata matatizo nikiwa kwenye upeleleza wa kuwatafuta watu waliotekeleza shambulio la bomu. Kwa bahati mbaya watu hao walifanikiwa kunikamata. Walinipiga risasi na kunitupa wakidhani nimekwisha kufa. Mtu mmoja alifanikiwa kuniokota na kuniwaisha hospitali, ambapo alinipeleka hospitali ya Mohameds Words. Bila mwanao, ilikuwa ni lazima nipoteze maisha, kwani alijitolea damu ambayo ilinifanya kuwa mzima. Siku zote ambazo wewe na serikali yako mmekuwa mkimtafuta mwanao, alikuwa hospitalini akiitazama afya yangu. Hapo ndipo kikundi cha Swaba kikajitokeza na kudai kinamshikilia Shazayi na kiliendelea kumtafuta Shazayi ili kiwe kimemshikilia kiukweli si kama kilivyowaongopea. Baada ya mimi kupona, tulikuwa kwenye mipango ya kuja ikulu, lakini hata hivyo, tulipata misukosuko kwani Swaba walikuwa nyuma yetu. Hivyo ndivyo ilivyokuwa muheshimiwa.”

Hata hivyo Roika hakuwa amemueleza Rais Galim kila kitu, vingine ilimlazimu kumficha.

Baada ya Roika kueleza hayo, Rais Galim alishusha pumzi, akamtazama Roika kwa sekunde kadhaa na kisha akamuuliza.

“Inamaana katikati yenu kuna nguvu ya mapenzi inayoendelea?”

Roika alishtuka, alimtazama Rais Galim kisha akainamishwa kichwa chini bila kujibu swali hilo. Rais Galim alimuliza tena.

“Bila shaka kupotea kwa mwanangu kumesababishwa na mapenzi si ndivyo, alihatarisha maisha yake kwa sababu yako nadhani majibu ninayo mwenyewe.”

Maswali hayo yalimfanya Roika kuogopa. Alishindwa kujibu lolote kutokana na kutokuwa na haki ya kufanya hivyo. Wakiwa katika maongezi hayo, Shazayi alikuja pale akiwa mwenye furaha. Lakini alimkuta Roika akiwa na huzuni na mwenye uwoga mwingi. Rais Galim alipogeuka kumtazama binti yake, aliona amekosa furaha ya ghafla mara tu alipokuwa amemuona Roika akiwa na sura ya uwoga na huzuni kubwa.

Nini kitafuatia usikose kesho          

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -