Monday, November 30, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU [112]

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Ilipoishia Jumamosi

Hakika lilikuwa ni jambo la kushangaza hasa pale Rais Galim aliposema:

SASA ENDELEA

“Sijawapa Swaba kile walichokitaka, ambacho ni umiliki wa eneo la Ramadan Kash na fedha. Hivyo uchumi na usalama wa nchi yangu, uko vile vile. Wapakistani wote msihofu, msihofu kuhusu kumpoteza malkia wenu na wala msihofu kupoteza mali za nchi yenu. Mwanangu amerejea Ikulu akiwa salama kabisa.”

Waandishi wa habari walihoji maswali mengi. Shazayi ametoka vipi  kwenye mikono ya Swaba kama serikali haikuwapa Swaba kile walichokitaka. Rais Galim alijibu kuwa, kikundi hicho cha kigaidi kiliiongopea Serikali.

“Ukweli ni kwamba, Swaba hawakuwa wakimshikilia mwanangu. Sababu za madam Shazayi kupotea katika mazingira ya kutatanisha, siwezi kuzielezea, kwani ni siri yake binafsi. Ingawa kwa nyakati hizo hizo, Swaba walikuwa wakimsaka kila kona ya nchi. Sina haja ya kuwazungumzia sana Swaba, watu waongo na wenye jeuri, walio tayari kuona watoto wa nchi hii wakifa kwa masilahi yao binafsi.” Aliongea Rais Galim.

Baada ya kuongea hayo, Rais Galim alimsimamisha binti yake ili aweze kuwasalimia wananachi na dunia kwa ujumla. Kwa jinsi alivyopendeza, watu waliamini kweli kiongozi wao mtarajiwa, hakuwa kwenye mikono ya Swaba. Shazayi aliposimama na kuonekana mbele ya kamera, kila mtu aliyekuwa karibu na runinga, alipiga kelele za shangwe.

Furaha ilikuwa kubwa kwa Wapakistani  wote, raia  wanaojua umuhimu wa mwanamke huyo kwenye nchi yao. Kwa furaha ya machozi, Shazayi alikaa kimya kwa muda wa sekunde kumi. Baadaye alijifuta machozi kwa kitambaa cheupe na kisha alisema:

“Nilikuwa napenda kutembelea hospitali ya Mohamed Words ili niwajulie hali watoto waliokumbwa na shambulio la bomu. Nikiwa huko, nilipata matatizo fulani yaliopelekea kuto rudi nyumbani kwa siku kadhaa na wakati huo tayari Swaba walikuwa nyuma yangu wakinitafuta. Lakini namshukuru Mungu na pia namshukuru Mr Roika kwa kuweza kunirudisha nyumbani salama. Nadhani wengi mtajiuliza Mr Roika ni nani, Mr Roika ni kijana kutoka Tanzania aliyekuja kutembea hapa nchini. Tulikuwa wote hospitalini kila siku, kwani yeye pia aliguswa na tukio la watoto kushambuliwa na bomu. Kurudi kwangu nyumbani salama, kumeweza kuwapa matumaini wapakistani wote, kwani naamini raia wote wa nchi yangu, wananipenda kama mimi niwapendavyo. Siku zote huwa nawaambia wanawake wenzangu, hata nyinyi mnaweza kuwa jeshi kubwa la kupigana na ugaidi.

Ugaidi unasababisha mambo mengi ikiwa ni kuwafanya wototo wetu kuwa vilema. Nililia sana kuona watoto wa chekechea wakiwa wamepoteza viungo vyao, hakika ilinisikitisha na kunifanya niumie sana. Swaba kokote mlipo, inabidi mtambue haki za mwanadamu kuishi, Allah hakutupa mamlaka ya kuondosha uhai wa mtu asie na hatia tena raia wa taifa lako.

Ni vema mkashusha silaha zenu chini. Mkakibadilisha kikundi chenu kutoka kuwa kikundi cha kigaidi na jeuri na kuwa chama cha siasa, kitachopigana na vyama vingine kisiasa kwa njia ya amani ili mpate kuingia ikulu kwa uhuru na sheria. Baada ya kusema hayo naomba kuwashukuru wapakistani wote mlio lia pamoja nami asanteni sana.”

Maneno hayo machache, yalikuwa maua mazuri kwa wapakistani na dunia kwa ujumla, hakika Wapakistani walijivunia kuwa na mwanamke mwenye akili kama Shazayi, watu wa mataifa mengine waliona wivu kwa mtoto huyo wa Rais kuwa mtu makini na asiyeogopa.Baada ya Shazayi kukaa, Rais Galim alimkaribisha Roika ambaye aliongea maneno machache. Kamera zilivyomchukua tu watu wanaomfahamu Roika walishangaa.

Watanzania waliokuwa wamemsoma kupitia jarida la The Century Human, walipigwa na butwaa kuona raia wa nchi yao, akipata sifa kubwa nchini Pakistani. Katibu  mkuu wa umoja wa mataifa, aliyekuwa hamfahamu kijana Roika, siku hiyo alimfahamu mfanyakazi wake.

“Nchi ya Pakistani ni nchi nzuri, nimependa kuwa hapa. Watu wake ni wakarimu na wenye upendo. Lakini binafsi naamini watu wa kikundi cha Swaba si raia wa nchi hii, hivyo msiumize sana vichwa kuwafikiria, wachukulieni kama maadui zenu. Kwani naamini kabisa wazazi waliopoteza watoto wao kwenye shambulio lile la bomu, nao wanaamini hivyo. Ni kweli uhalifu katika kila nchi upo lakini si wa kufanya kitendo kama kile. Na mimi namuomba mheshimiwa rais unipe watoto wote ambao wazazi wao walipoteza maisha kwenye lile shambulio, niende nikawalee na kuwatunza, naamini kazi hiyo tutaifanya mimi na madam Shazayi. Asanteni sana na Mungu aibariki Pakistani.”

Kelele za shangwe zilikuwa kwenye mitaa mbalimbali ya miji ya nchi hiyo. watu wengi walimpenda Roika mtu mweusi kutoka Tanzania. Baada ya Roika kuongea hayo kabla hajakaa kwenye kiti, Rais Galim bila kusita, alimsimamisha Shazayi na kuwashika wote wawili.

“Kabla hatujahitimisha mkutano huu,  napenda kutangaza jambo muhimu. Mr Roika na madam Shazayi ni vijana wanaopendana, hivyo muda si mrefu wanakwenda kuwa mke na mume,” aliongea Rais Galim kauli iliyowafanya Roika na Shazayi kuhisi aibu ingawa walikuwa na furaha kubwa.

RAMONA

Wakati hayo yote yakiendelea na yakirushwa kupitia televisheni mbalimbali, Ramona alikuwa hotelini akiyatazama. Alihisi maumivu makali ndani ya moyo wake. Hasira zilikuwa kuu kwenye kila kiungo cha mwili. Alihisi dunia nzima inamzomea na kumtesa. Alijihisi yu uchi mbele ya chumba cha ibada. Kwa hasira alipiga kelele, ambapo alichukua chupa ya Pandora na kuitupa kwenye runinga, runinga ilivunjika.

Nini kitafuatia? usikose kesho

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -