Wednesday, November 25, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Ilipoishia jana

KWA hasira alipiga kelele ambapo alichukua chupa ya Pandora na kuitupa kwenye runinga ikavunjika.

SASA ENDELEA

Alilia kama mtoto mdogo. Hakuishia kuvunja runinga tu, alitupa mito huku na kule, alivunja glasi na kuvuruga vitu vingine mle hotelini. Kitendo alichokiona kwenye televisheni cha Roika kutambulishwa kama mke wa Shazayi, aliona kama cha kishetani. Alimlaumu Roika kwa kumfanyia kitendo cha kinyama, ambacho ni kigumu kukisahau kwenye maisha yake.

“Roika umeharibu maisha yangu, umeharibu mapenzi yangu, nakuchukia Roika nakuchukia tena sana,” aliongea peke yake akiwa mwenye hasira huku akilia sana.

Wakati Ramona akiugulia maumivu hayo, maumivu makali ya mapenzi, kule maskani ya Swaba, nao walikuwa wakiufuatilia mkutano unaofanyika ikulu. Nao walikuwa wakiendelea na mkutano wao wa ulimwengu, pamoja na mtandao wa biashara wa Ramona. Hasira ilikuwa kubwa kwa kiongozi wa kikundi hicho Zahil, pamoja na wapiganaji wake. Walimtupia lawama kiongozi wa wafanyabiashara Makx Viego, wakisema kuwa, mfanyakazi wake amewatia aibu na amesababisha wapiganaji wake mmoja kuuawa na mwingine kushikiliwa na serikali, ambapo anaweza kuwaweka matatani kwa kutaja mfumo wao wa kuisalama.

Lakini wakati wakiendelea kuutazama mkutano huo, kiongozi Zahil Bin Shaq, alipigwa na butwaa baada ya kumuona mtu anayemfahamu kwenye runinga, akitambulishwa na Rais Galim. Aliyekuwa akitambulishwa alikuwa ni Roika. Zahil alikuna kichwa na kujiuliza mtu huyo alimuona wapi. Lakini muda si mrefu, alimkumbuka mtu huyo kuwa ndiye yule waliyemuua mle ndani. Na waliyempa jukumu la kumuua alikuwa ni Ramona.

Zahili alishangaa, aliona kama muujiza. Wenzake waliposhangaa kuweweseka kwake aliwauliza.

“Jamani huyu mtu mnamkumbuka, si yule mpenzi wake na Ramona ambaye yeye mwenyewe Ramona alimpiga risasi? Ni yeye haswaa, naye si alikuwa anaitwa Roika?”

Aliposema hivyo, wote walishangaa baada ya kumkumbuka Roika kuwa ndiye mtu waliyedhani wamemuua. Watu wote ndani ya chumba cha mkutano walishangazwa na hilo. Ilibidi Zahil amuite mpiganaji wake, ambaye siku Roika alipopigwa risasi na Ramona, alimtuma akauchome moto mwili wake.

“Hebu nieleze, ilikuwaje, huyu mtu ulimchoma moto?” aluliza Zahil kwa hasira.

“Ukweli mkuu siku ile nilifanya makosa. Pindi nilipotaka kuuchoma moto mwili wake, niligundua kuwa nimesahau kiberiti na sikuwa na siraha yoyote. Ilibidi niuache mwili wake pale pale na kurudi kuchukua kiberiti na nilipourudia sikuuona,” alijibu mpiganaji huo kwa uwoga.

“Whaaat! Hukuona, sasa nani aliuchukua au Ramona?”

“Hapana si Ramona, kwani kwa wakati huo Ramona alikuwa hapa maskani.”

“Sasa ni nani aliyekuja mtaa wa maskani yetu na kujua kile tunachokifanya?” aliuliza Zahil kwa hasira zingine kuu.

“Sifahamu mkuu ila nisamehe kwa uzembe huo.”

“Kosa lako si kushindwa kuuchoma moto mwili wa yule mtu, bali kosa lako ni kukaa kimya na kutokutueleza kuwa mwili wa Roika ulichukuliwa na mtu asiyefahamika. Sasa kwa  kosa hili la kufanya siri, adhabu yake ni ndogo.”

“Sawa mkuu nitaipokea adhabu kwa nidhamu ya hali ya juu.”

“Kaniletee vidole vyako vya mwisho vya mikono na miguu sawa!”

“Sawa mkuu.”

Tayari Swaba na wafanyabiashara wote, walijua wako kwenye wakati mgumu. Muda si mrefu walijua jeshi la nchi hiyo, litaingia na kuivamia maskani yao, maskani iliyojificha katikati ya nyumba za wafanya ibada wa mtaa wa Ramat. Maskani iliyokuwa eneo lililojificha, ambalo serikali ya nchi hiyo ilishindwa kulibaini kwa zaidi ya miaka saba.

Hivyo vikundi vingine vya kigaidi vinavyofungamana na wao, viliwashauri kuhama mtaa huo na kutafuta maskani mpya. Zahil Bin Shaq alikubaliana na ushauri huyo, kwani naye alijua wako hatarini kwa sababu hakujua Ramona au Roika amewaweka mahali gani.

Makx Viego alimpigia simu Ramona na kumtaka afike maskani ya Swaba mara moja. Ramona aliipokea simu hiyo, akiwa mwenye hasira na huzuni kubwa baada ya kuachwa na Roika mwanaume aliyemfanya kuwa kichaa wa mapenzi.

“Haloo Ramona nakuomba ufike kabla ya saa moja jioni ni muhimu sana.”

“Nitafika,” alijibu Ramona na kukata simu.

Ramona alikuwa amepanga kuachana na mtandao huo wa biashara kwani alikuwa na hasira za kuachwa na Roika huku akiwalaumu wafanyabiashara pamoja kikundi cha Swaba kuwa ndio waliosababisha. Alijua kwa makosa yaliojitokeza ya kushindwa kufanikisha zaoezi la kukamatwa kwa binti wa Rais Shazayi binti Galim, lazima watamfukuza kwenye mtandao wa biashara. Lakini hakujua lengo walilonalo ni kumuua kabisa.  Naye alipanga kuwalaumu kwa kusababisha hayo yote, baada ya kumpa jukumu la kumpiga risasi mtu ampendaye.

Alipanda gari ikiwa ni saa 12: 30 na kuelekea mtaa wa Ramat, kunako maskani ya Swaba. Alifika maskani hapo saa moja usiku akiwa na walinzi wake watano. Alikuta mkutano wa ulimwengu ukiendelea, walimkaribisha kwa heshima fulani, ambapo alielekea kukaa kwenye kiti. Watu wengi wakiwemo wanawake wenzake walimtazama kwa jicho la hasira. Kila mjumbe wa mkutano, alikuwa na glasi ya maji juu ya meza, hata Ramona aliwekewa glasi yake ya maji. Lakini glasi ya Ramona, ilikuwa imewekwa kidonge cha usingizi kiitwacho Venoc kidonge hicho kiliwekwa kabla ya Ramona kufika maskani hapo.

Mkutano ulianza kumjadili Ramona aliyekuwa anajua lazima atalaumiwa na baadaye kuachishwa kabisa ushiriki wake kwenye mtandao wake wa biashara, mtandao unaoshirikiana  na Swaba pamoja vikundi vingine mabalimbali vya dunia.

Hakujua lengo lao lilikuwa ni kumuondosha kabisa duniani.

Nini kitafuatia usikose jumatatu

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -