Wednesday, October 28, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU [69]

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

Ilipoishia Jumamosi

“MAMA nisamehe, mama sikufiria kufanya hivyo, najutia dhambi yangu,” aliongea Ramona huku akiwa ameishika miguu ya mama Roika, akilia kupita kiasi.”

Kilio kikubwa kilikuwa kimetawala mle ndani, kila mmoja aliendelea kulia. Lakini kilio cha mama Roika kilikuwa ni kilio cha kuigiza kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa  akifahamu kuwa mwanaye yuko wapi na anafanya nini kwa muda huo. Lakini kilio cha Ramona kilikuwa ni zaidi ya kilio cha kusaga meno. Maana yeye hadi kufikia muda huo, alikuwa akijua kuwa mpenzi wake yuko kaburini.

SASA ENDELEA

Maumivu ya Ramona yalikuwa ya kweli. Alilia sana, hii ilitokana na kujiona mtu asiyetakiwa kusamehewa.

Mbele ya mtu aliyemuulia mtoto wake, Ramona alihitaji kusamehewa. Mama Roika hakuhitaji kuwa na kinyongo na Ramona. Kwanza alishangaa ni ujasiri gani alionao mwanamke huyo wa kuja kumuomba msamaha kwa kitendo alichokuwa amekifanya. Ingawa alikuwa akijua kuwa mtoto wake alipona katika kisa hicho cha kuhuzunisha, ilibidi ajifanye hajui chochote kama mwanaye alipatwa na matatizo hayo na tayari alishakuwa amekufa.

Mama Roika alilia kilio cha kuigiza ili mrembo Ramona asijue chochote. Ndio maana kabla hawajaanza kuzungumzia hayo, mama Roika aliamua kumtoa mwanaye Dina kwa kumwambia aende sokoni akanunue mchele. Kwani Dina hakufahamu lolote kuhusu kaka yake.

Ramona aliendelea kulia mbele ya mama Roika akiomba asamehewe kwa kitendo cha kinyama alichokuwa amekifanya. Ingawa jambo lile lilikuwa limemuumiza mama Roika, aliona hana budi kumsamehe Romona. Kwanza alimuona ni mwanamke jasiri na aliyekubali kosa. Alimuona ni mwanamke mwenye tabisa nzuri. Hata kama alikuwa ni mwanamke gaidi.

Ramona akiwa chini ya miguu ya mama Roika, mama Roika alimuinua. Ramona alishtuka kuguswa, akakiinua kichwa chake na kumtazama mama Roika usoni.

“Inuka mwanangu,” aliongea mama Roika kwa huruma.

Ramona aliinuka na kusimama mbele ya mama Roika, huku akiyafuta machozi yaliokuwa yakipenda kutoka muda wote. Alianza kushangazwa na upole wa mama Roika, upole ambao hakuutegemea kama ungekuwepo mara moja.

“Hebu kaa kwenye kiti kwanza futa machozi,” aliongea tena mama Roika akimuacha Ramona katika mshangao.

Baada ya Ramona kukaa mama Roika alimtazama Ramona kwa dakika kadhaa za ukimya , huku akiyafuta machozi kwa kitambaa alimwambia.

“Siku zote nimekuwa nikiishi kwa mashaka nikiutilia shaka mwenendo wa mwanangu. Alikuwa ni mtu wa kupenda kusafiri nchi nyingi zilizokuwa na amani na zisizo kuwa  na amani. Nilimwambia mwanangu kazi hii ya UN ni kazi ya hatari, nilimwambia kuwa atakuja uniache mama yake, hakutaka kunisikia. Kifo chake leo hakijanishangaza sana, ingawa kimeniumiza sana. Toka mwezi uliopita, ukimya wa Roika kwetu sisi familia yake, ulikuwa unatia mashaka, tayari mimi nilianza kuhisi kuwa huenda kuna jambo baya limemkuta.  Nachotaka kusema mwanangu ni kwamba mimi nimekusamehe na nimekusamehe kwa moyo mweupe kwa kuwa umekuja kwa miguu yako kuja kuongea jambo la hatari kama hili. Kweli naamini hukudhamilia kufanya hayo.”

Ramona hakuamini kama mama yake Roika amemsamehe, aliona kama ni kitendo rahisi sana. Lakini ilibidi kuamini maana asingeweza kuomba msamaha zaidi ya hapo ili aweze kusamehewa kwa msamaha amabo ungeonekana kwa macho.

Mama Roika akiwa analia alimfuata Romna na kumkumbatia.

“Usiogope mwanangu, Mungu ametufundisha kusamehe hata kama tumetendewa vitendo vya kutisha. Nimekusamehe kwa kitendo ulichokifanya, nakuomba uwe na amani ili uonyeshe kwamba, umeupokea msamaha wangu kwa mikono yote miwili. Futa machozi.”

“Mama nashindwa kuamini kama umenisamehe. Unajua ni ngumu kwa mtu kumfuata mtu uliyemuulia mtoto wake na kumuomba msahama. Halafu naye akakupokea na kukusamehe. Simaini kama kweli umenisamhe ,” aliongea Ramona kwa machozi mengi.

“Amini hivyo mwanangu. Mimi nimekusamehe kwa sababu ya kitendo chako cha kusafiri mbali kuja kuniomba msamaha nakuona ni binadamu wa tofauti na unaestahili kuhurumiwa na kusamehewa.”

“Asante mama.”

Wote walikumbatiana huku Ramona akizidi kulia pindi alipokuwa akiiona picha ya Roika iliyokuwa nyuma ya mama Roika. Picha iliyomuumiza kwani Roika alikuwa ni kijana mzuri na mpole. Mwanaume aliyetokea kumpenda kuliko wanaume wote hapa duniani. Alijiuliza ni shetani gani aliyompitia hadi akakubali kumpiga risasi mpenzi wake.

Baadaye walikaa wote pale sebuleni na kuongea mengi. Mama Roika alijitahidi kumfariji Ramona, Ramona naye alijitahdi kumfariji mtu aliyemuulia mwanaye.

Muda mfupi mdogo wake na Roika, Dina aliingia mle ndani na kuwakuta wote wakiwa na nyuso zisizo za kawaida, nyuso zilizoonyesha kuwa watu hao walikuwa wametoka kuyafuta machozi yao.

Pakistani

Biyanah mwanamke bilionea alikuwa kwenye wakati mgumu usioelezeka. Maisha yake yalianza kumtofautisha yeye na utajiri aliokuwa nao. Kwani alikuwa analia kila siku. Hakujua hadi muda huo Roika alikuwa amekwenda wapi. Aliamua kuongea na uongozi wa hoteli ya Alashak ambapo walikaa na kuulizana kuhusu mahali alipo kijana huyo.

Nini kitafuatia? Usikose kesho

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -