Wednesday, October 28, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

Ilipoishia Jumanne

RAMONA alishuka kwenye gari baada ya kuwa amefika Hoteli ya New Bitaika. Hoteli aliyokuwepo kipenzi rafiki yake, Biyanah Rumo mwanamke tajiri. Alipiga hatua kuelekea ndani. Wafanyakazi wawili wa Biyanah walimpokea na kumkaribisha. Alipofika chumbani kwa rafiki yake, alimkuta Biyanah akiwa amesimama dirishani akitazama nje.

SASA ENDELEA

Ramona akiwa mwenye furaha na uchangamfu mkubwa, alimsogelea Biyanah pale karibu na dirisha.

“Niambie rafiki yangu. Uko makini dirishani una mawazo gani mtoto wa kike? Aliongea Ramona huku akimshika  Biyanah bega.

Biyanah hakujibu neno lolote, zaidi aliendelea kutazama mji wa Nuruwan kwa kupitia dirisha.

“Biyanah vipi uko sawa?” aliuliza Ramona huku akimtazama rafiki yake usoni.

Lakini Biyanah aliendelea kukaa kimya. Kwa maringo ya kudeka Ramona alimgeuza Biyanah ili watazamane. Ramona Alishtuka kumuona rafiki yake, akiwa na uso wa majonzi, huku akiwa na michirizi ya machozi.

“Heee! Biyanah kuna nini, mbona uko hivyo. Ulikuwa unalia, niambie rafiki yangu nini kimetokea, kuna mtu kakuudhi?” aliongea Ramona kama mtu aliyekuwa amechanganyikiwa, huku akimshika rafiki yake kichwa na mabega, maana hali ya Biyanah ilizidi kumshtua.

Lakini Biyanah alijitoa kwa Ramona na kwenda kukaa kwenye kiti. Akachukua chupa ya Pandora na kumimina vinywaji kwenye glasi mbili, akamtazama Ramona kisha akamwambia.

“Kaa chini na karibu kinywaji.”

Ramona akiwa kwenye sintofahamu na wasiwasi mkubwa, alipiga hatua za kinyonge hadi pale kwenye kochi ambapo alishuka taratibu na kukaa huku akimtazama Biyanah kwa umakini mkubwa.

“Biyanah unanitisha, hebu niambie kuna nini?” aliongea Ramona.

“Hebu kunywa kinywaji kwanza,” alijibu Biyanah, safari hii uso wake ulibadilika na kuwa wenye furaha kidogo.

Hata hivyo Ramona Fika, mrembo wa dunia, alizidi kuwa katika wakati mgumu asimuelewe kabisa rafiki yake kipenzi Biyanah Rumo. Kwa umakini na unyonge wa hali ya juu, Ramona alikaa kimya kumsikiliza rafiki yake. Ukimya ulitawala kwa dakika moja, baada ya ukimya huo, Biyanaha alisema.

“Nasikitika kukwambia kuwa, mapenzi yanaweza kuwa doa la uchafu ndani ya  urafi wetu mweupe.”

Aliposema hivyo, aliinyanyua glasi na kuinywa waini ya Pandora, baada ya kuitoa mdomoni akaiweka tena ile glasi mezani. Wakati huo Ramona alizidi kuwa katika kitendawili kikubwa asimuelewe kabisa rafiki yake.

“Najua kwa maneno hayo, unahangaika sana kunielewa, lakini utanielewa kadri utakavyozidi kuifungua akili yako.”

“Biyanah hebu nyosha sentensi nikuelewe unajua unanipa wasiwasi?” Ramona aliongea.

Biyanah alimtazama rafiki yake kwa sekunde 20 zingine kisha akaendelea kuzungumza.

“Ramona lengo la kuja hapa Pakistani si kuja kumpuzika ama kukumbuka wewe. Ingawa kweli nilihitaji kuwa nawe, tukae tufurahie upepo popote pale, lakini kwa sasa sikuwa nimekuja kwa lengo hilo. Nilikuja kwa lengo la kutaka kujua uhusiano wako na Roika.

“Roikaaaaa!?

Kwa mshangao mkubwa na wa aina yake Ramona alishtuka kusikia jina la Roika. Macho yalimtoka, alibaki kumtazama Biyanah asiamini kama jina la Roika limetamkwa mdomoni mwake.

“Biyanah umemjulia wapi Roika?” Ramona aliuliza.

“Hata mimi nilishangaa sana, uliponitumia picha ukiwa na Roika. Ilinishangaza kupita kiasi. Kwangu ilikuwa ni maajabu ya pili ya dunia. Nimekuja Pakistani kwa lengo la kuja kukuuliza uhusiano wako na Roika. Nilipofika jana, nilikuwa na lengo hilo hilo.  Lakini sina haja ya kuuliza hilo tena kwa kuwa tayari nimekwisha jionea mwenyewe, nimejionea kabla hata sijakuuliza.” Aliongea Biyanah huku akitokwa na machozi.

“Biyanah mbona sikuelewi, hebu niambie wewe unamfahamu vipi Roika na mlikutana wapi?” Ramona aliuliza.

“Sio tulikutana wapi Roika is my boyfriend, mume wangu mtarajiwa, mtu atakae kuwa baba wa watoto wangu.”

“Whaaaat!? Sijakuelewa, what are you talking about?” (unaongelea nini) kwa mshangao mkubwa Ramona aliuliza.

Kwa machozi mengi Biyanah alimpigia  Ramona magoti.

“Ramona rafiki yangu, naomba uniachie Roika wangu. Nampenda sana, siwezi kuishi bila yeye, tafadhari sana nakuomba, niko chini ya miguu yako.”

Ramona alizidi kuwa kwenye kitendawili kikubwa, alibaki kuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, yaani hakuelewa chochote, imekuwaje na nini maana ya jambo lile. Alibaki kumtazama rafiki yake aliyezidi kutokwa na machozi.

“Biyanah hebu kaa kwanza tuzungumze.  Bado sijaelewa ni nini kinaendelea kati yetu na Roika. Kwa kifupi nipo gizani sitambui lolote lile.”

Biyanah alikaa kwenye kochi na kusema.

“Ramona siwezi kukulaumu wewe kwa kuwa hujui chochote. Roika amekuwa mtu wangu kabla hata hajawa na wewe ninafikiri alikutana na wewe akiwa safarini.”

Bado Ramona hakuamini wala kuelewa kile alichokuwa akiambiwa na Biyanah, aliinamisha kichwa chini, mwili wake ulianza kutetemeka, alihisi maumivu makali ndani ya moyo wake. Alimtazama rafiki yake kwa huzuni kubwa kisha akamuuliza.

“Ni kwa muda gani wewe na Roika ni wapenzi?”

“Nakumbuka siku ambayo mapenzi yetu yalianza ndio siku ambayo wewe ulikuwa unakwenda kushiriki miss world. Lakini nilianza kumpenda Roika mwaka mmoja uliopita kabla wewe haujarudi kutoka Afrika kusini. Sikuwa nimejiandaa vema kumtambulisha Roika mbele yako, nilipanga kufanya hivyo wakati mwingine,” aliongea Biyanah huku akizidi kutokwa na machozi.

“Biyanah sawa yote yanaweza kuwa sahihi mimi sipingani na wewe, lakini je Roika anakupenda wewe kwa dhati. Kama anakupenda kwa nini akusaliti?”

“Ramona wewe ni mrembo wa dunia tena mzuri sana. Wanaume wengi hata wenye wake na wapenzi wao wanatamani kuwa na wewe. Naamini Roika ananipenda ila alipokutana na wewe akaingia katika kishawishi.”

Ramona aliposikia hivyo, aliumia sana machozi yalianza kumtoka. Maneno ya Biyanah ya kuwa Roika hakumpenda tu bali alimtamani na kuingia katika kishawishi yalimpa maumivu makali ya mapenzi. Alianza kuhisi kuwa huenda ni kweli Roika alitaka kuyachezea maisha yake. Alianza kumuonea huruma rafiki yake, alimsogelea Biyanah na kumshika mabega na kumwambia.

“Biyanah hata mimi nampenda sana Roika, lakini kwa kuwa wewe ndiye mpenzi wake halali, uliyekutana naye kabla yangu, siwezi kuendelea kuudhurumu moyo wako. Nakuacha uendelee na mpenzi wako, mimi nimeutoa muhanga moyo wangu kama sadaka ya urafiki wetu.”

Maneno hayo ya Ramona, yalimfanya Biyanah kufarijika kupita kiasi, aliamini kweli ana rafiki wa kweli.

“Asante sana Ramona, umenipa zawadi njema, kwani siwezi kuishi bila mwanaume yule. Licha ya kuwa amenisaliti, lakini nimekubali kuingia gharama yoyote ile ili nifunge nae ndoa, niko yatari kujifanya mimi ndiye mkosaji. Nampenda mwanaume huyu nampenda sana. Nakushukuru kwa kuuona upendo wangu kwake,” aliongea Biyanah akiwa amejilaza kwenye kifua cha Ramona aliyekuwa akitokwa na machozi.

Baada ya maongezi hayo, maongezi yaliochukua takribani saa moja na nusu, Ramona alimuaga rafiki yake Biyanah. Hakutaka kusemeshwa tena kuhusu suala lililomuhusu Roika, kwani alishakuwa na  hasira kuzidi uwezo wake wa kubeba hasira.

“Tutaonana kesho,” aliongea Ramona huku akielekea kufungua mlango, akionekana kuwa hakuridhika na jambo lile kwa upole.

“Ramona kabla hujatoka nisikilize kwanza. Naomba usijisike vibaya, nisamehe kwa kuharibu penzi lako na Roika. Wewe huna makosa kabisa mwenye makosa ni Roika” aliongea Biyanah.

“Haina haja ya kuongeza maongezi mengine kuhusu Roika, naona inatosha. Usijali, nitamwambia aje maana hajui kama wewe uko hapa Pakistani na ninafikiri hajui kama mimi na wew ni marafiki.”

Ramona aliposema hivyo, alifungua mlango na kutoka mle chumbani, moja kwa moja alielekea kupanda gari ambapo alirudi hoteli ya Alashak.

Kichwa kilimuuma mrembo wa dunia Ramona Fika, sasa alianza kuyajua vizuri maumivu ya mapenzi, maumivu ambayo mwanzo alikuwa akiyasikia tu na kuyaona kwenye tamthilia. Alijiuliza swali kuu, kwa nini Roika alitaka kuyachezea maisha yake. Alijuta sana kujiingiza kwenye penzi la mwanaume asiyemjua vizuri.

Baada ya dakika 10 alifika hotelini, wakati huo ilikuwa ni saa 12: 45 jioni. Hakutaka kuelekea chumbani kwa Roika moja kwa moja alielekea chumbani kwake. Ambapo alijifungia na kulia sana.

“Roika ulikuja kufanya nini kwenye maisha yangu, kwa nini umenipa mumivu makali kiasi hiki? Naanza kumchukia sana mwanaume huyu. Hata sijafaidi penzi lake tayari kashauvunja moyo wangu?” alijisemea Ramona kwa machozi mengi.

Baadaye aliinua simu yake ya mkononi na kumpigia Roika.

“Njoo chumbani kwangu,” aliongea Ramona na kuikata simu kabla hata Roika hajazungumza lolote.

Roika akiwa chumbani kwake alishangazwa na simu aliyopigiwa na Ramona. Akatoka chumbani kwake, akaingia kwenye lifti na kushuka chumbani kwa Ramona. Alipofika, alimkuta Ramona akiwa amesimama pembeni ya meza iliyokuwa na vinywaji, akiimimina waini ya Alamos kwenye glasi.

“Mpenzi umerudi saa ngapi,” aliongea Roika huku akimsogelea Ramona.

Alipofika karibu yake alimkumbatia kwa nyuma. Hasira zilizidi kuwa kubwa kwa Ramona baada ya kukumbatiwa. Lakini alijitahidi kuzivicha ili Roika asizione mapema.

“Mpenzi uko sawa kweli?” aliuliza Roika huku mdomo wake ukiwa karibu kabisa na shingo ya Ramona.

Ramona alizidi kuumia na kujisikia vibaya kupita kiasi. Kwa hali ya kujikaza alimgeukia Roika. Wote wakawa wanatazamana usoni.

“Naomba uwende hoteli ya Bitaika gholofa ya kwanza chumba namba sita.  Ili uingie, utawaambia walinzi kuwa umetumwa na Ramona.” aliongea Ramona kwa  umakini, akijaribu kuificha sura yake, sura iliyokuwa na hasira na majonzi.

“Mh! Mpenzi kuna nini huko?” aliuliza Roika kwa tabasamu.

“Mwanaume hatakiwi kuuliza maswali. Bali anafuata kile anachoambiwa na mpenzi wake. Ngoja nikutoe wasiwasi. Nataka ukaonane na rafiki yangu. Si unakumbuka nilikwambia kuwa kuna rafiki yangu amekuja kutoka Tanzania?”

“Kwanini tusiende wote,” Roika aliuliza.

“Mimi nina wageni muda mfupi ujao hivyo siwezi kutoka.”

“Rafiki yako anaitwa nani?”

“Anaitwa Sheila, anapenda mfahamiane kama mtu na shemeji yake. Ana hamu sana ya kukuona. Kesho ndio tutakaa wote watatu tuzungumze, sawa mpenzi,” aliongea Ramona safari hii akimbusu Roika.

Lakini ndani ya moyo wake moto mkali ulizidi kumuunguza. Alijikaza vilivyo ili Roika asifanikiwe kuyajua majonzi na hasira alizokuwa nazo.

“Sawa mpenzi ngoja niende. Wewe utamaliza kikao na watu wako saa ngapi?”

“Nafikiri hatutamaliza nusu saa.”

“Sawa mpenzi,” alijibu Roika.

Alimbusu Ramona,  akafungua mlango na kutoka mle chumbani. Lakini hata hivyo, bado alitawaliwa na wasiwasi. Kwa kuwa sura ya Ramona, ilikuwa tofauti kidogo na ya siku zote.

Alipanda gari kuelekea hoteli ya Bitaika kwenda kumuoa rafiki yake Ramona. ambaye ameambiwa na Ramona kuwa anaitwa Sheila. Lakini ilikuwa si kweli, bali mtu huyo anayekwenda kuonana naye alikuwa ni Biyanah.

Nini kitafuatia usikose kesho  

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -