Saturday, October 31, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU [82]

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

Ilipoishia Jana

Kama mtu aliyechanganyikiwa Ramona alimkumbatia Roika na kumshika vilivyo. Alianza kulia kama mtoto mdogo.

 SASA ENDELEA

Hakika lilikuwa ni jambo la kushangaza sana machoni mwa mrembo wa dunia, Ramona Fika. Hakuamini kumshika mtu aliyekuwa anajua kuwa ni marehemu. Mapigo ya moyo wake yalikuwa yakimuenda mbio. Mwili wake ulikuwa ukitetemeka, jasho jembamba lilikuwa likimtoka.Hofu haikuondoka kwake, hofu ya kuona kama amekutana na mzimu wa Roika ilizidi kumwandama. Japo alikuwa ni mwenye dhambi, lakini aliendelea kung’ang’ania kulala kwenye kifua cha Roika.Alikuwa akikiinua kichwa chake mara kwa mara akimtazama Roika usoni na kurudi tena kifuani mwake.

Roika alibaki kama mtu asiye elewa cha kufanya, kwani aina fulani ya upendo kwa Ramona, ilikuwa bado inaishi ndani yake.Huruma na chembe za mapenzi zilimfanya atokwe na machozi. Hakuwahi kuona kilio kikubwa toka kwa mrembo huyo wa dunia, toka walipokuwa wamekutana. Pindi Ramona alipokuwa akilia kifuani kwake, alikuwa akitamka maneno yaliozidi kumuweka Roika katika wakati mgumu.

“Roika mpenzi wangu nisamehe, sikukusudia kufanya vile. Najuta mimi Ramona najuta. Nimeishi katika mateso makubwa sana pindi wewe ulipokuwa haupo mbele yangu. Nakupenda sana Roika siwezi kuishi bila wewe. Mimi kukupiga risasi, haikumaanisha kuwa sikupendi ila ni jambo gumu lililonikuta mbele ya watu wangu wa biashara. Nina…….”

“Shiiiiiii,” Roika alimtaka Ramona asiendelea kuongea.

Naye alimshika na kumkumbatia vizuri, akamtazama Ramona usoni na kumwambia.

“Yale yalishapita, hupaswi kujilaumu. Fanya kama jambo lile halikutokea. Mimi leo niko mbele yako.”

“Roika kama hujanisamehe ni bora unipige risasi  kama mimi nilivyokupiga, ili nafsi yako itulie kwani mara nyingi nilikuwa nafikiria kujiua.Lakini mkono wa mama na mdogo wangu ulikuwa ukinizuia kufanya hivyo.”

“Ramona haina haja ya kufanya hivyo, mimi naona hujanikosea. Cha muhimu ni kuangalia maisha yanayokuja.”

“Roika nimeishi bila amani hadi ikanipelekea kurudi Tanzania kwenda kumuomba mama yako msamaha juu ya kitendo nilichokifanya.”

Roika aliposikia hivyo, alibaki kushangaa alimtazama Ramona na kumuuliza.

“Ulikwenda wapi?”

“Nilifika nyumbani kwa mama yako. Maana nilijiona ni mtu mwenye hatia sana mbele ya familia yenu. Niliona nikimueleza mama yako ukweli juu ya kile kilichokupata na kumuomba msamaha, huenda itanipunguzia maumivu niliyokuwa nayapata kila siku.”

Ingawa Ramona alikuwa ni mwanamke gaidi, lakini machoni mwa Roika alianza kuonekana ni mwanamke mzuri. Kitendo chake cha kwenda kumuomba mama yake mzazi msamaha, kiliufanya moyo wa Roika kukifurahia kitendo hicho na kukiona ni cha kishujaa. Alianza kumuona Ramona ni mwanamke fulani wa tofauti, ingawa nafsi yake iliendelea kupata mateso makubwa kwa sababu Shazayi binti wa rais, ndiye aliyekuwa ameitawala sehemu kubwa ya moyo wake kwa muda huo.

“Nashukuru kwa kufanya hivyo, wewe ni mwanamke mwerevu.”

Ramona alimtazama Roika kwa muda wa dakika moja ya ukimya. Kisha akausogeza uso wake karibu kabisa na uso wa Roika. Taratibu alianza kuupeleka mdomo wake kuelekea kwenye mdomo wa Roika. Roika alibaki ameganda asielewe nini cha kufanya, mwili wake ulianza kutetemeka.Hofu isiyoelezeka ilianza kumshika. Ramona alipougusanisha mdomo wake  na mdomo wa Roika, kwa uwoga wa hali juu, alianza pia kuhangaika akihitaji kuukutanisha ulimi wake na ulimi wa Roika, ulimi uliokuwa umejificha ndani ya kinywa chake, usitake kutoa ushirikiano. Wakati kitendo hicho kikifanyika, sehemu kubwa ya moyo wa Roika, moyo unaompenda Shazayi ilianza kupigana vita na sehemu ndogo inayompenda Ramona. Penzi la Ramona linaloishi ndani ya Roika, lilionekana kuwa na nguvu kubwa.

Roika hakutaka kuonyesha ushirikiano huo ambao ni moja ya ishara kubwa ya wawili wanaopendana. Kitendo kile kilianza kumpa Ramona wasiwasi mkubwa. Kwa aibu, aliutoa mdomo wake mbele ya mdomo wa Roika. Alimtazama Roika usoni na kisha akarudi tena ili kurudia tendo lile. Lakini bado Roika hakutaka kushiriki kitendo hicho.

NURUWAN

Wapiganaji sita wa kikundi cha Swaba waliokuwa wamevaa mavazi ya kawaida, walikuwa wanawasili hoteli ya Alashak. Nia yao ikiwa ni kuja kumfuata malikia wa mtandao wa biashara, mtandao unaofanya biashara na kikundi chao, mwanamke Ramona Fika. Kwani toka juzi mrembo huyo wa dunia hakuwa ameonekana kwenye maskani yao. Wala hakupata kuhudhuria kikao chao muhimu cha wao na wanamapinduzi wa Urusi kilichofanyika jana jioni. Sababu ya mrembo huyo kutohudhuria kikao hicho hakijulikana. Hivyo wapiganaji sita walitumwa na kiongozi wao Zahil Bin Shaq kwa ombi la kiongozi wa mtandao wa biashara ambaye ni kiongozi wake na Ramona Makx Viego.

Baada ya kukaguliwa na walinzi wa hoteli, wapiganaji hao walipanda lifti kuelekea ghorofa ya tatu kwenda kumwangalia Ramona. Walipofika chumbani kwake hawakumuona mrembo huyo. Zaidi waliuona mkoba wake, uliokuwa mezani. Waliingia vyumba vyote ikiwemo chumbani, bafuni na chooni, lakini hawakumuona.

“Inaonyesha alikuwepo muda si mrefu au ametoka nje?” aliuliza mmoja wao, kwa lugha ya kiarabu.

“Labda, hebu tumsubiri.”

Walikaa pale sebuleni kwa muda wa dakika 20 lakini bado hakukuwa na dalili zozote za kuja kwa Ramona.

Wakiwa wamekaa, mmoja wao aliuchukua mkoba wa Ramona na kuufungua. Ndani yake alivikuta vitu vingi lakini kilichomshangaza, aliiona waleti ya Roika.

Nini kitafuatia? usikose kesho   

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -