Sunday, November 29, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Ilipoishia jana

Ramona alishtuka, alibaki ameduwaa asiyaamini macho yake mawili.

SASA ENDELEA…

ILIKUWA ni maajabu kwa Ramona kumuona Roika mle ndani. Macho yake yalimtoka, nafsi yake ilishtuka vilivyo, pumzi yake ilisimama kwa sekunde mbili, alibaki kumtazama Roika asiamini kama ndiye yeye

Lakini macho yanayomjua Roika na kumpenda, yalikuwa yamesema kweli. Alitamani kulia pindi alipomuona Roika akiwa chini ya ulinzi mkali, moyo wake bado uliendelea kumdunda kupita kawaida.

Roika alibaki kumtazama Ramona kwa huzuni kubwa na woga wa aina yake. Akijua kuwa amemkosea Ramona kupita kiasi, amemkosea kwa kuingilia mambo yake, aibu ilikuwa imemtawala. Aliinamisha kichwa chini asitake kumtazama Ramona. Ramona alianza kupandwa na hasira za chini chini.

Hakuna mtu aliyekuwa akimfahamu Roika mle ndani, zaidi ya Ramona. lakini kitendo cha Ramona kushtuka wakati Roika akiinuliwa kichwa, kilikuwa kimemshtua mmoja wa wapiganaji wa kikundi cha Swaba. Alimtazama Ramona na baadae akamtazama Roika na kugundua kitu, aligundua kuwa watu hao wawili wanafahamiana. Aliamua kulihifadhi kwa muda tukio hilo la wawili hao kutazamana na kuonyesha kujuana.

Watu wote mle ndani walikaa kimya wakimaanisha kuwa hawamfahamu Roika na suala la kuwa yeye anamtafuta mdogo wake aliyeshikiliwa na wauzaji wa dawa za kulevya, kwao lilikuwa ni geni. Siri kubwa ilikuwa imebaki kwa Ramona aliyekuwa akijua kuwa Roika ni mpenzi wake na amekuja kwenye jengo hilo kwa nia ya kumpeleleza. Alijikaza na kuyaficha macho yake yasimtazame Roika mara kwa mara, asije kunguliwa na wafanya biashara wenzake ya kuwa anamfahamu.

Yule mpiganaji pekee wa kikundi cha Swaba, aliyekuwa amegundua kitu mara baaada ya Roika kuletwa pale, alimfuata kiongozi wake na kumtonya neno. Wakatoka wote na kuelekea katika chumba cho ofisi, ambapo waliongea huko kwa dakika kumi. Ramona alizidi kupatwa na uoga mkubwa baada ya kuona tukio hilo. Roika alijua kuwa heunda, watu hao wamekwisha kugundua kuwa anafahamiana na Ramona. Mapigo ya moyo wake yalianza kumsumbua kupita kawaida.

Baadae mpiganaji wa Swaba, alitoka chumba cha ofisi na kuwaambia wafanya biashara wote watulie kwanza. Akawaita wapiganaji wengine watano pamoja na viongozi wa biashara, waingie kwenye kile chumba. Kisha akamgeukia Ramona na kumwambia.

“Madamu Ramona tunakuomba mara moja.”

Ramona alishtuka. Haraka akajikaza ili watu wasimshtukie. Kwa unyonge mkubwa uliokuwa ndani ya moyo wake, aliinuka kwenye kiti. Wakati akipiga hatua kuuelekea chumba cha ofisi, yule mpiganaji wa Swaba aliwaambia wapiganaji wenzake wammlete pia na Roika. Roika na Ramona wote walishtuka kwa siri, hofu ziliwajaa sana.

Ramona alipoingia ndani ya ofisi, alipewa kiti na kukaa. Roika alipoletwa, alikalishwa chini. Kiongozi kwa kikundi cha Swaba aliyeitwa Zahil Bin Shaq alikuwa amekaa kwenye kiti, pamoja na viongozi wakubwa wa biashara. Pembeni yao walizungukwa na wapiganaji wa Swaba waliokuwa na bunduki.

Kiongozi wa Swaba alimtazama Ramona na kisha akamuuliza.

“Madamu unamfahamu mtu huyu?”

Swali lilikuwa gumu sana kwa upande wa Ramona, alikuwa ameshtuka ndani ya nafsi yake mara baada ya kuulizwa hivyo. Alijikaza kisabuni akageuka kumtazama Roika, aliyekuwa amejivika ungangari wa kutojulikana mapema, kuwa anafahamiana na Ramona. Baada ya sekunde kumi Ramona alijibu.

“Hapana simfahamu.”

Aliposema hivyo wote mle ndani walitazamana.

“Sikiliza madamu, usidhani kwamba inaweza kukuletea shida endapo utatuambia ukweli, ukweli juu ya mtu huyu. Tuambie kama unamfahamu,” aliongea Zahil Bin Shaq.

“Ni kweli na ni hakika, simfahamu mtu huyu,” alijibu Ramona kwa ujasiri mkubwa.

Baada ya kuona Ramona hasemi ukweli na ni mwanamke wanayemuheshimu sana, ambaye huwa hawapendi kumsumbua, Zahil alikaa kimya kwa sekunde 20.

Baadae mpiganaji wake alimsogelea na kumdokeza jambo sikioni. Zahil alimgeukia tena Ramona na kumwambia

“Sawa madamu, ikiwa haumfahamu, tutakuomba wewe kesho umpige risasi,” aliongea Zahil.

Aliposema hivyo, moyo wa Ramona ulishtuka. Alihema ndani kwa ndani, huku mwili wake ukijikaza vilivyo. Zahil aliendelea kuongea.

“Tunakupa muda wa kufikiria. Halafu kesho uje na jibu la kwamba unamfahamu au la na kama hamfahamu, utamuua kwa mikono yako mwenyewe. Maana nakujua wewe ni mwanamke jasiri na huwa nakupongeza sana kwa hilo. Sawa madamu?”

“Sawa,” alijibu Ramona kwa ujasiri hafifu.

Baada ya hapo, Roika alifungiwa kwenye chumba, akisubiri kesho ambayo ni siku ya kupigwa risasi na mwanamke ampendaye. Aliogopa sana.

Baadaye mkutano uliahirishwa, ambapo ulipangwa kuendelea kesho. Wajumbe wote na viongozi wa vikundi vya kigaidi, walikwenda kumpumzika makwao wakiliacha jengo la Swaba kwenye ulinzi mkali. Ramona naye alirudi hotelini.

Alipofika hotelini, aliingia chumbani kwake na kilio kikubwa.

Nini kitafuatia usikose kesho

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -