Monday, October 26, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU [95]

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

Ilipoishia jana

 “SAWA naomba tukutane Nuruwan leo jioni,” aliongea Roika na kumfanya Ramona afurahi na kupata nafuu ya  moyo huku akijua njia rahisi ya kumpata Shazayi.

SASA ENDELEA

Bado huruma ya mapenzi ilizidi kumwandama Roika, kila alipoisikia sauti ya Ramona, moyo wenye asili na uliokuwa mali ya Ramona, toka nafsi yake ilipokuwa imeanza kufikiria mapenzi, ulimfanya kuisikia sauti ya mrembo huyo na kuinyenyekea kwa kiasi fulani.

Alikubali kuonana na Ramona jioni ya siku hiyo. Ukweli ni kwamba si kweli alikuwa mjini Islamabad, bali alikuwa Nuruwan na wakati anapigiwa simu na Ramona, alikuwa duka moja akiwa anamnunulia Shazayi gauni. Hakuwa amelijua lengo lingine la Ramona la kutaka wakutane. Alijua ni mapenzi tu ndiyo yanayomsumbua Ramona.

Lakini ukweli ni kwamba, Ramona alihitaji kukutana na Roika kwa lengo la kumwona Shazayi ili aweze kufanya jitihada za kuwasiliana na Swaba. Ingawa suala hilo lilikuwa likimuumiza sana Ramona, kwa jinsi anavyokwenda kumwangamiza binti huyo wa Rais, asiye na hatia, lakini aliona hana njia nyingine ya kuokoa penzi lake zaidi ya kufanya dhambi hiyo.

Saa moja jioni Roika alikuwa mgahawa mmoja uliokuwa hatua 40 kutoka hoteli ya Free Pakistan Embassy akiwa anamsubiria Ramona aliyekuwa njiani kuja. Akiwa anakunywa kinywaji cha Pandora, alikuwa ni mwenye mawazo. Alikuwa anawaza ni jinsi gani atamweleza Ramona ukweli kuwa kwa sasa moyo wake umehamia kwa Shazayi. Akiwa anafikiria hayo, simu yake iliita. Alikuwa ni Ramona aliyekuwa anampigia. Aliipokea na kuiweka sikioni.

“Niko hapa njiapanda inayokwenda Rutak na Free Pakistan Embassy. Niko kwenye mgahawa umeandikwa Al hajili,” aliongea Roika.

“Sawa nakaribia,” alijibu Ramona.

Punde tu Ramona alikuwa anaegesha gari pembeni ya mgahawa huo. Roika alikuwa akimuona kupitia dirisha kubwa la mgahawa. Ramonna akiwa anapiga hatua Roika aliutazama mwendo wake, alizidi kuushangaa uzuri wa Ramona ambao unamtenganisha na tabia yake.

Ramona aliingia na kuangaza huku na huku ndani ya mgahawa huo, uliokuwa na watu wachache. Alimwona Roika akiwa amekaa kwenye kona  ya mwisho. Kwa unyonge na moyo wenye majonzi, alipiga hatua kumsogelea Roika.

“Karibu Ramona,” Roika alimkaribisha.

“Asante sana,” alijibu Ramona huku akikaa.

Aliitoa nguo kichwani iliyokuwa kama hijabu. Alimtazama Roika kwa macho mazuri, macho yaliokuwa yanaonyesha kuwa yamechoka kutokwa na machozi mara kwa mara. Roika alimtazama Ramona kwa sekunde kadhaa na baadae aligeuka kutazama dirishani, kisha akageuka tena kumtazama Ramona.

“Vipi hali yako inaendeleaje toka ulipoondoka hospitalini?” Roika aliuliza.

“Ni njema, hata hivyo kuanguka kwangu hakuwa na madhara makubwa,” alijibu Ramona.

“Usiseme hivyo, daktari alisema ulipatwa na mshtuko mkubwa wa moyo na kichwa. Ulitakiwa ukae hospitalini kwa siku kadhaa.”

“Tuachane na hayo Roika. Mimi ni mzima.”

“Sawa kama hujali afya yako.”

Walikaa kimya kwa muda wa sekunde kumi kila mmoja akiwa na uwoga wa kuanzisha maongezi mapya, ambayo ndio lengo kuu la kukutana.

“Nakumbuka nilipokwenda kwa mama yako. Mama yako aliniambia kuwa mimi ni mwanamke mwelevu na kwa kuwa niko hivyo, aliniambia amenisamehe bila kinyongo. Nilimpenda sana mama yako. Mdogo wako aliyekuwa shabiki yangu naye tulitokea kupendana sana. Hali hiyo ilizidi kuniumiza kwani ilinifanya kuendelea kujuta kwa kitendo kile cha kukupiga risasi,” aliongea Ramona.

Akiwa anataka kuendelea kuongea hayo, Roika alimkatisha kwa kusema.

“Ramona hupaswi kuzungumza yaliyopita, kwa nini uumie juu ya hayo.”

“Roika kwa nini nisizungumze yaliopita wakati hayo ndiyo yanayojenga hiki kinachoonekana leo? Roika umebadilika, hutaki kunielewa, hunipendi tena. Yote kwa sababu ya kile kilechotendeka nyuma,” alijibu Ramona kwa ukali huku akitokwa na machozi.

Roika alibaki kimya huku moyo wake ukiwaka moto. Alimuonea huruma lakini alishindwa amueleze nini.

“Roika uko wapi upendo wako? Leo unataka kunihukumu bila huruma nimeshakiri makosa yangu lakini bado moyo wako uko mbali nami.”

“Ramona kabla ya yote nakuomba uachane na biashara unayofanya achana kabisa na wale watu. Umekwisha ua wengi wasio kuwa na hatia sasa inatosha. Japo hujanyanyua silaha yako kumuua mtu lakini silaha unazosambaza zinazidi kuleta maafa makubwa kila kona ya dunia.”

Roika aliposema hivyo Ramona aliinama chini. Aliinua uso wake kwa uwoga na aibu kisha akasema.

“Roika naijua dhambi yangu.  Tayari nimekwisha kuiacha biashara hii na tayari ninafikiria kurudi nyumbani Tanzania ili nirudi kuanza maisha mapya.”

“Ramona wewe ni mwanamke mzuri sana, uzuri wako haupswi kuchanganywa na mambo hayo. Naomba uachane kabisa na biashara hiyo kwani sipendi kuona unapotea,” aliongea Roika kwa uchungu mkubwa.

Wakiwa wanaongea hayo simu ya Roika iliita na kwa muda huo ilikuwa mezani karibu na Ramona. Shazayi ndiye aliyekuwa anapiga, hivyo Ramona naye alilijua hilo. Roika alipokea na kuiweka sikioni.

“Mpenzi uko wapi mbona umechelewa unaniogopesha usijekuwa umepatwa na matatizo,” aliongea Shazayi.

“Usijali niko njia nakuja,” aliongea Roika.”

Nini kitafuatia? Usikose Alhamisi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -