Friday, October 23, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

Jumbe alizojibiwa ni chache kuliko zile alizotuma. Hakika alihisi moto unawaka kupita kiasi katika maumivu yake ya mapenzi. Hali hiyo ilichangia kutokula chakula na kutofanya kazi yoyote siku ya tatu mara baada ya Roika kuelekea Mexico.

SASA ENDELEA

Alianza kumtafuta Roika kwenye simu akitaka kuongea naye, maana ilikuwa ni siku ya tatu Roika hakuwa amemjibu kuwa atarudi lini, licha ya kuulizwa mara kadhaa. Jumbe zilizojibiwa ni chache kulingana na zile alizomtumia siku mbili zilizopita.

Biyanah alianza kumuomba Mungu amlinde Roika asije kuchukuliwa na mtu mwingine au kupata tatizo lolote. Maisha yake kwa kiasi kikubwa yalitegemea uwepo wa Roika. Mwanamume aliyekuwa tayari kumpa nusu ya utajiri wake. Muda mwingine alikuwa akijisemea kuwa ikitokea mwanamke yeyote amemchukulia mpenzi wake, basi atakuwa na uwezo wa kufanya lolote lile pingine hata kumuua.

Mapenzi yalishaanza kumuweka katika mawazo mabaya na ya kishetani. Ugonjwa huo mbaya ulimzidi kila inapoitwa leo.

Ikiwa ni Jumapili baba yake Biyanah, Branko Rumo, alimtembelea mwanaye, baada ya kurudi kutoka Afrika Kusini. Bilionea huyo ambaye ni mtu wa tatu kwa utajiri barani Afrika, makazi yake yalikuwa nchini Afrika Kusini, ambako  ndiko kwenye mfumo wake mzuri wa biashara.

Akitumia ndege yake binafsi, alifika jiji la Dar es Salaam saa 12:00 jioni, ambapo alipitiliza moja kwa moja hadi kwa Biyanah, mwanawe mpendwa, mtoto wake wa pekee, anayempenda kuliko hata utajiri wake. Lakini alishangaa kuona binti yake hajaja kumpokea uwanja wa ndege, ukizingatia si kawaida yake, ilibidi ampigie simu Biyanah na kumuuliza yuko wapi kwa muda huo.

“Ndiyo baba niko nyumbani, samahani kwa kutokuja airport kukupokea, ninahisi kuwa ninaumwa,” aliongea Biyanah akijitetea vilivyo.

Ili kuhakikisha kama ni kweli mwanawe yuko nyumbani, Branko Rumo aliwapigia simu walinzi kuwauliza. Walinzi walimjibu kuwa Biyanah hajatoka siku hiyo, kutwa nzima ameshinda ndani. Branko Rumo akiongozwa na msafara wa magari manne pamoja na polisi, alikuwa njia kuelekea nyumbani kwa Biyanah.

Branko aliwasihi madereva wake waongeze mwendo maana huenda mwanawe yuko katika hali mbaya. Baada ya dakika 15, bilionea Branko Rumo alikuwa anawasili nyumbani kwa mwanawe. Alishuka haraka kwenye gari na kuingia ndani, ambapo alimkuta mwanawe, Biyanah katika hali isiyo ya kawaida. Biyanah alimkimbilia baba yake na kumkumbatia huku akilia.

“Nini tena mwanangu, unaumwa?” aliuliza Branko Rumo kwa huzuni, maana hali ya mwanaye ilikuwa imemuogopesha kwa kiasi kikubwa.

“Nisaidie baba, nisaidie, nateseka sana,” aliongea Biyanah akiwa katika kifua cha baba yake.

Baba yake hakujua nini tatizo, maana alipomshika mwanaye, alimkuta na joto la kawaida na si joto la ugonjwa wowote. Alikaa naye chini na kumuuliza nini hasa chanzo cha yeye kuonekana amedhoofika mwili kiasi kile. Biyanah hakumueleza kitu kingine zaidi ya kuuhusisha udhaifu na unyonge aliokuwa nao na mapenzi. Alimueleza baba yake kuwa maisha kwake ni magumu bila mwanamume anayeitwa Roika. Branko Rumo alishangaa kusikia hivyo, maana hakutegemea ataambiwa kuwa mapenzi yamemuweka katika hali ile na si homa, wala ugonjwa wowote.

“Mwanangu kupenda ndio kunakuweka katika hali hiyo?” aliuliza mzee Branko Rumo.

“Ndiyo baba, maisha yangu kwa sasa yamekuwa na wakati mgumu. Maana nimekuwa nikihitaji kuwa na mtu nimpendaye muda wote,” aliongea Biyanah, huku akitokwa na machozi.

“Kwani ni nani unayempenda hadi ukafikia kuwa katika hali hii?”

“Baba ina maana umemsahau yule anayenitesa usiku na mchana. Nimpendaye kwa dhati. Mbona nilishakwambia kuwa kuna kijana nampenda?”

“Mwanangu mimi nimesahau, si unajua nina mambo mengi kichwani, ila nakumbuka hukuwahi kuniambia kuhusu kijana huyo. Kwani anaitwa nani?”

Biyanah alimtazama baba yake kwa huruma, huruma iliyopenya vizuri hadi kwenye macho ya mzee Branko Rumo. Kwa sauti ya kujiamini Biyanah alijibu..

“Roika Malino.”

“Roika?” mzee Rumo aliuliza huku akipatwa na mshangao.

“Ndiyo baba, Roika Malino. Nakumbuka nilishawahi kukuambia kuhusu kumpenda kijana huyu.”

“Roika, yule kijana anayefanya kazi Umoja wa Mataifa?”

“Ndiyo baba.”

Biyanah alipojibu hivyo, baba yake alicheka kidogo akamtazama mwanawe kwa makini, na kumwambia:

“Mwanangu kumbe ni kijana yule. Hata hivyo nimeanza kukumbuka kuwa ulishawahi kuniambia, kwanini sasa hadi leo hujamwambia kuwa unampenda, ina maana hajui.”

“Sio hivyo baba, ukweli nilisha mwambia, na akanielewa vizuri. Ni siku ya tatu sasa tokea tulipoanza mahusiano yetu.”

“Sasa mwanangu, kumbe tayari nyinyi ni wapenzi, sasa nini tena tatizo, maana kwa ninavyomjua yule kijana, sidhani kama anaweza akakufanyia kitu kibaya, ni kijana mpole na mwenye tabia nzuri. Namkumbuka vema, nilishawahi kumualika kwenye sherehe yangu ya kuzaliwa.”

“Ni kweli baba uyasemayo, lakini usifikiri kuwa mpole au mwenye tabia nzuri ni mtu atakaye kuwa amepewa kila kitu na Mungu, huenda ana mapungufu yake. Ni siku ya tatu leo tokea Roika asafiri kwenda Mexico na ni siku ya tatu tokea mapenzi yetu yaanze. Lakini, hadi sasa kanijibu jumbe tatu tu tofauti na idadi ya zile nilizomtumia, alichelewa kunijibu kuwa amefika salama. Hadi kufikia leo mchana, amenijibu ujumbe mmoja tu. Mara nyingi nimemuuliza unarudi lini lakini hajanijibu. Nilianza kumtafuta kwa kumpigia simu lakini namba yake, imekuwa hewani mara chache sana na haipokelewi. Hali hiyo inaninyima raha kabisa, naanza kufikiri labda Roika hakunipenda, huenda alinikubalia tu ili kuniridhisha, baada ya kuona ninavyoteseka juu yake, huenda hajanipenda,” aliongea Biyanah kwa machozi.

Mzee Branko Rumo aliposikia hivyo, alimtazamaa mwanaye aliyekuwa anazidi kumpa machungu, maana hakupenda mwanawe aumie kiasi kile tena kwa ajili ya mapenzi.

“Mwanangu usiwaze mbali kiasi hicho, kama alisha kwambia kuwa anakupenda basi, haina haja ya kuwa katika hali hiyo. Huwezi jua anafanya nini kule. Kumbuka yule ni mtu mkubwa sana katika kazi yake. Umoja wa Mataifa unamtambua vizuri. Huenda kazi yake kwa sasa inambana. Hujui amekwenda Mexico kwa kazi gani. Nilishawahi kuzungumza naye na akaniambia kuwa kazi yake kubwa akiwa ndani ya UN ni kuwatazama watu wanaoishi katika mazingira magumu kama vile ya vita, magonjwa na dawa za kulevya. Watu hao huwatafutia makazi mpya ya kuishi, hivyo kazi yake si rahisi kiasi kwamba akafanya kila kitu kwa ajili yako tena akiwa nje ya nchi.

Kama alifanikiwa kukujibu ujumbe mara tatu, basi jua anakujali na anakupenda, wala usiwe na hofu. Hofu kama hii mwanangu haisaidii na zaidi utakuwa unajipa kilema cha ufahamu,” aliongea mzee Branko Rumo huku akiwa amemshika mashavu mwanawe.

“Baba una hakika kuwa Roika ananipenda kwa dhati?”

“Nina hakika.”

“Kweli?”

“Don’t worry, Roika loves you.”

Maneno ya Branko Rumo yalimuweka mwanawe, Biyanah katika ahueni na kumfariji. Alihisi kupungua kwa maumivu makali ya mapenzi, maumivu ya kumuwaza Roika, katika vitendawili vingi.

Baadaye alifarijika na kuendelea na maongezi mengine na baba yake, wakiendelea kufurahi na kuulizana mengi yanayohusu biashara zao. Wote wawili ni mabilionea wakubwa. Baba akiwa tajiri wa tatu barani Afrika na mwanawe akiwa ni mwanamke wa sita kwa utajiri katika upande wa wanawake barani Afrika.

Kwa muda huo, Biyanah alifarijika, maana baba yake alifanikiwa kumrudisha binti yake katika hali nzuri tofauti na ile aliyomkuta nayo mwanzo.

NCHINI MEXICO

“Asante,” aliongea Roika,  akageuka na kurudi chumbani kwake. Alipofika chumbani, aliufungua ujumbe huo na kuusoma. Moyo wake ulishtuka akajihisi mwili mzima umekosa ushirikiano.

Ujumbe huo ulisema:

“Habari Roika, samahani kwa kutokuja chumbani kwako kukuaga. Mimi nimeshasafiri, nimekwenda Haiti. Naomba uni follow katika akaunti yangu ya Twitter. Nitaonana na wewe wakati mwingine, kwa kheri Roika, take care”

Ulikuwa ni ujumbe mbaya sana kwa Roika, alijihisi amekosa kila kitu katika dunia hii. Hakika alisikia maumivu makali yasiyokuwa na mfano. Mwili wake ulinyong’onyea ghafla, kutokana na kuzidiwa na moyo uliopenda kuzidi hali yake ya kufikiri. Kwa hasira aliuchana ule ujumbe.

Alisimama na kutembea huku na kule akijizungusha pale sebuleni kama mshale wa saa. Aliwaza maisha bila Ramona yatakuwaje. Akitazama upweke unaoukuja mbele yake, ambao bado ulikuwa haujamfikia, aliogopa sana.

Alikaa na kufikiria, akijiuliza kwa nini Ramona amemfanyia unyama ule, wa kuondoka kienyeji bila kukutana naye, alishasahu kuwa, katika ujumbe aliopewa, Ramona alianza kwanza kwa kuomba msamaha. Yeye hakufikiria hilo, alichojali yeye ni mapenzi tu.

Ukizingatia alikuwa katika maandalizi makubwa ya kumtamkia Ramona kuwa anampenda, basi aliumia sana kwa njiwa wake kuruka, ikiwa yeye ana hitaji kubwa la moyo. Alifikiria nini afanye, maana kumuacha Ramona ni jambo gumu linalohitaji ushujaa, ushujaa kama ule wa Daudi kupigana na Goliati, huku nafsi yake ikikiri kuwa haina ushujaa huo mbele ya Ramona Fika, mrembo wa dunia wa Kiafrika.

Hakuwa na muda hata wa kutazama ujumbe wowote wa mpenzi wake Biyanah, katika barua pepe na katika akaunti yake ya Twitter. Hata simu alishakuwa ameizima. Alikaa na kutafakari nini cha kufanya. Alijiuliza arudi nyumbani Tanzania au amfuate Ramona nchini Haiti?

Wazo la kumfuata Ramona ndilo wazo lililokuwa na nguvu kimaamuzi katika akili yake, kuliko wazo lingine lolote lile. Maana alitambua kuwa ameshakuwa mgonjwa anayehitaji dawa inayoitwa Ramona Fika.

Nini kitafuatia? Usikose kesho

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -