Saturday, October 31, 2020

URAFIKI KANYE WEST, TRUMP BADO WAZUA MJADALA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NEW YORK, Marekani

URAFIKI uliopo kati ya rapa mahiri, Kanye West na Rais wa Marekani,  Donald Trump, umezidi kuzua mjadala jinsi wawili hao wanavyopatana.

Mjadala huo uliibuka tena juzi baada ya rapa huyo kuibuka akisema kwamba kofia ya Trump imempa nguvu za Superman na huku akizikosoa za siku hizi.

Kauli ya rapa huyo imekuja ikiwa ni baada ya muda mrefu kuwa akionyesha hisia zake wazi wazi za kumsifu Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter na mahojiano mbalimbali.

Hata hivyo, amekuwa akiwakosoa wanaomkemea kwa kuwataka wamwache awe na uhuru wa mawazo yake.

Kanye West alialikwa katika Ikulu ya Marekani kwa ajili ya chakula cha mchana kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mageuzi katika magereza, ajira na masuala ya Wamarekani weusi.

Ni mjadala uliojaa vioja vingi kutokana na ukweli kwamba, Trump na Kanye wote ni wazungumzaji sana na hutumia zaidi mtandao kuweka wazi hisia zao.

Katika majadiliano hayo yaliyolenga siasa, mageuzi na uzalishaji, West alinukuliwa akisema: “Wamejaribu kunitisha, marafiki zangu kuhusu kuvaa hii kofia, lakini hii kofia inanipa nguvu.”

Kanye alienda mbali zaidi na kusema kofia hiyo iliyoandikwa “Make America great again,” maneno yanayowakilisha kauli mbiu ya utawala wa Trump inamfanya anajionea fahari sana na anajiona kama Superman na aliongeza kuwa Trump ametengeneza kofia shujaa kwa ajili yake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -