Wednesday, November 25, 2020

USAJILI DIRISHA DOGO BAO LA DAKIKA YA 90

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MARTIN MAZUGWA

UKISIKIA bao la dakika ya 90 basi ndio hili ambalo klabu kongwe za Simba na Yanga zimefanya katika mbio za kuimarisha vikosi vyao kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu soka ya Vodacom utakaoendelea kesho kwa baadhi ya viwanja hapa nchini kuwaka moto.

Wakati dirisha hilo likiwa limefungwa usiku wa kuamkia leo, Simba imesajili wachezaji wapya wanne huku Yanga ikikamilisha usajili wa wachezaji wawili, hata hivyo, hadi tunakwenda mitamboni Simba walikuwa wanakwenda resi sana  kuinasa saini ya beki kiraka wa Yanga, Mbuyu Twite, ambaye pia alikuwa akiwaniwa na Majimaji ya Songea.

Pamoja na timu zote kufanya mabadiliko kwa kuongeza wachezaji wapya, lakini Azam, Simba na Yanga ndio walionekana kutikisa usajili wao kwani ndizo zinazoonyesha ushindani wa soka.

Katika usajili huo, Simba wamefanikiwa kuongeza sura  ya wachezaji wapya  wakiwamo wa kigeni wawili ambao ni kipa Daniel Agyei aliyetokea klabu ya Medeama ya Ghana na kiungo aliyetokea katika nchi hiyo, James Kotei.

Lakini Simba wamesajili wachezaji wazawa washambuliaji, Pastory Athanas kutoka Stand United na Juma Liuzio ambaye ni Mtanzania aliyekuwa akichezea klabu ya Zesco ya Zambia.

Simba wameingia askari wapya huku wakiwatema kipa Vincent Angban raia wa Ivory Coast na Mussa Ndusha wa Congo, lakini wakiwatoa kwa mkopo Juma Awadh na Malika Ndeule katika klabu ya Mwadui.

Kwa upande wa Yanga wenyewe hawajafanya mabadiliko makubwa katika kikosi chao, baada ya kufanikiwa kumleta kiungo, Justin Zulu kutoka Zambia ambaye ametua nchini na kupachikwa jina la Mkata Umeme kutokana na uhodari wake wa kusakata soka.

Zulu amesajiliwa katika kikosi hicho baada ya Yanga kumtema kiraka, Mbuyu Twite raia wa Rwanda mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Yanga wamemsajili mzawa, Emmanuel Martin, kutoka JKU ya Zanzibar ambaye alifanikiwa kuwafunga mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Azam ambao wanajiandaa mzunguko wa pili wa ligi hiyo na michuano ya kimataifa mwakani, wamefanya usajili wa wachezaji wapya wa kigeni, Yakub Mohamed, Abdul Mohamed kutoka klabu ya Aduana Stars ya Ghana na Stephane Mpondo kutoka Cotton Sports ya Cameroon na mzawa Joseph Mahundi Mbeya City.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -