Sunday, October 25, 2020

USAJILI DIRISHA DOGO JANUARI MAJEMBE HAYA YATATIMKA LA LIGA NA KUTUA ENGLAND

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

LONDON, England

WAKATI wa majira ya kiangazi yaliyopita, mashabiki wa soka hasa wale wa Ligi Kuu England (VPL) walishuhudia ujio wa Shkodran Mustafi, Claudio Bravo na Eric Bailly.

Ni miongoni mwa mastaa wengi wa Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ ambao walihamishia makazi yao England.

Lakini sasa zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili la Januari, kuna orodha ndefu ya wachezaji mahiri wa La Liga wamekuwa wakitajwa kuwaniwa na klabu za VPL.

Ni mastaa gani, wanatoka timu gani kubwa za La Liga na watajiunga na klabu zipi za Ligi Kuu England?

Joao Cancelo (Valencia kwensda Man United)

Valencia wameonekana kupoteza makali yao ya misimu kadhaa iliyopita na hilo limesababisha kukimbiwa na baadhi ya nyota wake.

Moja kati ya mastaa wanaotamba kwa sasa klabuni hapo ni Cancelo ambaye pia haitakuwa rahisi kumzuia kuondoka.

Staa huyo ana umri wa miaka 22 na ana uwezo wa kucheza nafasi ya beki wa kulia na pia utampenda akicheza kama kiungo wa pembeni (winga).

Anatajwa kuwa kwenye mipango ya kocha Jose Mourinho ambaye amepania kumpeleka Old Trafford.

Hiyo ni ishara kuwa Mourinho ameshindwa kushawishika na uwepo wa Antonio Valencia na Matteo Darmian.

Licha ya ukweli kwamba Cancelo si mzuri sana katika kuzuia mashambulizi, lakini staa huyo wa zamani wa Benfica anaweza kubadilika ikiwa atakuwa kwenye timu kubwa kama Man United.

James Rodriguez (Real Madrid kwenda Chelsea)
Kiungo mshambuliaji huyo ni raia wa Hispania, lakini sasa haonekani kuwa muhimu kwenye kikosi cha kocha Zinedine Zidane.

Klabu kadhaa za England zimekuwa zikiisaka saini yake.  Moja ya klabu zinzomhitaji pale England ni Chelsea.

Steven N’Zonzi (Sevilla kwenda Crystal Palace)

Anakipiga katika klabu ya Sevilla na nafasi yake uwanjani ni eneo la kiungo wa kati. N’Zonzi amekuwa hatari tangu alipojiunga na Sevilla. Amekuwa tegemeo la Sevilla chini ya kocha Jorge Sampaoli ambaye alitua klabuni hapo kuchukua mikoa ya Unai Emery.

Aliwahi kuichezea Stoke City lakini kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha akiwa La Liga, tayari klabu nyingi za England zimeanza kuifukuzia saini yake.

Kocha wa Crystal Palace, Sam Allardyce, ameonyesha nia ya kumrejesha England nyota huyo aliyewahi pia kutamba na Blackburn Rovers. Itakumbukwa kuwa Allardyce ndiye aliyemsajili N’Zonzi wakati kocha huyo alipokuwa akiinoa Sevilla mwaka 2009.

Cedric Bakambu (Villarreal kwenda West Ham)

Staa mwingine wa La Liga unayepaswa kumsubiri kwa hamu Ligi Kuu England ni mpachikaji mabao raia wa Congo, Bakambu.

Msimu uliopita alicheka na nyavu mara 22 na ndiye aliyekuwa kinara wa mabao kwenye kikosi cha Villarreal. Baada ya Villarreal kuwasajili Alexandre Pato na Nicola Sansone wakati wa majira ya kiangazi, nyota huyo haonekani kuwa na nafasi kikosini. Ingawa Crystal Palace nayo imepania kumsajili, West Ham inaongoza kwenye mbio za kuitaka huduma ya nyota huyo.

Manu Trigueros (Villarreal kwenda Leicester)

Trigueros raia wa Hispania ni kiungo wa kati wa Villarreal. Kutokana na uwezo wake dimbani, Barcelona wamekuwa wakitajwa kwenye mpango wa kuivizia saini yake.

Akiwa ndiyo kwanza ana umri wa miaka 25, Barca wanamuona nyota huyo kuwa mrithi sahihi wa mkongwe Andres Iniesta. Trigueros anawaniwa na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Leicester City huku kocha Claudio Ranieri akitajwa kuwa shabiki wake mkubwa.

Inigo Martinez (Real Sociedad kwenda Everton)

Ni beki wa kati wa Real Sociedad ambaye kipaji chake kiliibuliwa na academy ya klabu hiyo.

Ana urefu wa futi  5 na inchi 11 na umbo lake halitofautiani sana na beki kisiki wa  Real Madrid na timu ya Taifa ya Hispania, Sergio Ramos. Amekuwa kivutio kwa makocha wa klabu mbalimbali za Ulaya tangu alipokuwa kwenye kikosi cha U21 ya Hispania. Sifa yake kubwa ni uwezo alionao wa kutumia mguu wa kushoto licha ya kuwa mlinzi wa kati. Mabosi wa Everton wamekuwa bize kuhakikisha wanainasa saini ya staa huyo pindi dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa mwezi huu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -