Tuesday, October 27, 2020

Ushauri wa Scholes kwa Paul Pogba

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

MANCHESTER, England

PAUL Scholes amefunguka kuwa mchezaji ghali wa Manchester United, Paul Pogba, hachezi sawa na mtu mwenye thamani ya pauni mil 86.

Haya yamekuja baada ya Pogba, aliyeanza vyema michezo ya Premier League kuchemka katika mechi mbili za hivi karibuni, ikiwemo ya Uropa, United waliyochezea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Feyenoord.

Licha ya nyota kadhaa wa United kucheza chini ya kiwango kwenye pambano kama Marcos Rojo, Morgan Schneiderlin na Matteo Darmian, bado gwiji huyu wa Man United, Scholes alitupa jicho lake kwenye kiwango kilichoonyeshwa na Pogba.

“Bado amekuwa akipata shida sana mpaka sasa,” alisema Scholes, alipokuwa akichambua pambano hilo katika kituo cha BT Sport. “Usiku wa leo amechemka tena, hakuwa katika kiwango chake bora, nililitegemea hili mapema.

“Mpaka sasa sifahamu ni eneo gani anacheza uwanjani. Kuna anayefahamu namba ya Pogba uwanjani? Sidhani, namuona akiwa huru na kutembea tu uwanjani, lakini ndio jukumu alilopewa?

“Yuko kila upande uwanjani. Nafikiri anajaribu kuwaza kufanya vitu vingi sana kila anapokuwa na mpira.

“Mara zote anajaribu kupiga chenga watu watatu au wanne, anakimbia sana na mpira. Nafikiri angetulia sasa na kufanya kazi yake iwe nyepesi.

“Uchezaji wake wa sasa si aina ya mchezaji Manchester United waliyemuhitaji katika dirisha la usajili. Hawakumsajili Lionel Messi ili apige chenga watu watano na kujificha pembezoni mwa uwanja kila mara. Walimsajili kiungo imara, mwenye nguvu na kiongozi katikati ya uwanja anayeweza kupokonya mpira na kupandisha mashambulizi.”

Hivi karibuni baada ya pambano la United dhidi ya Manchester City, Pogba alipondwa na mchambuzi wa kituo cha Sky Sports na mchezaji wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher kwa kitendo cha kukosa nidhamu ya mchezo na kuigharimu timu yake kulala bao 2-1 kwenye ‘Manchester derby’.

Lakini kwa upande wa Scholes, ameonyesha kutokuwa na mashaka na uwezo wa Pogba na kutabiri atakuja kufanya vyema kama akibadilika.

“Kama akiamua kucheza tachi moja na kuachia mpira kwa haraka kwa straika kama Zlatan Ibrahimovic, hakuna mtu wa kupambana naye. Ana nguvu, kasi na uwezo wa kufanya hivyo kama akiamua.”

Katika hatua nyingine, Scholes alisema kuwa licha ya usajili wa nguvu uliofanywa na Jose Mourinho, bado anaamini United inahitaji kiungo mwingine kwa ajili ya kuja kucheza sambamba na Pogba.

Akifafanua zaidi, Scholes alisema kiungo huyu wa Kifaransa anakosa msaada wa kiungo mwenye uwezo wa kusoma mchezo na kupoza mashambulizi nyuma yake kama alivyokuwa Andrea Pirlo wakati akiichezea Juventus ya Italia.

“Anahitaji kiungo wa kuimiliki timu nyuma yake ili tuweze kuona zaidi ubora wake,” aliongeza Scholes.

“Mourinho anatakiwa kurudi tena sokoni na kusaka mtu wa aina hiyo, kwa sasa kwenye kikosi wanaye Michael Carrick, anaweza kufanya kazi hiyo vyema.

“Nafikiri wanaweza kurudi sokoni na kusaka kiungo mwingine aina ya Carrick na hapo naamini Pogba anaweza kumiliki dimba na kucheza vyema katikati ya uwanja.

“Najua Mourinho ameridhika na wachezaji wanne aliowasajili, lakini naamini bado atarudi tena sokoni kwa ajili ya kutafuta wachezaji kama Luka Modric au Toni Kroos (viungo wawili wanaokipiga Real Madrid).

“Nafikiri hawa wachezaji wanapatikana na mazungumzo yanaweza kufanyika, namuona Pogba akiimarika zaidi kama akipata watu wabunifu na imara wa kucheza nyuma yake,” alimaliza Scholes.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -