Tuesday, November 24, 2020

USHINDI WA YANGA WAIFUNGULIA MILANGO YA NEEMA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAINAB IDDY


 

BAADA ya ushindi wa bao 1-0 walioupata juzi kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ushindi huo ni kama umefungua milango ya neema kwa klabu ya Yanga baada ya uwepo wa taarifa za kuoga noti kutokana na udhamini mpya wa klabu hiyo.

Yanga ambayo imekuwa haina mdhamini baada ya kumalizika kwa mkataba wake na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na sasa kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Spoti Pesa kutoka Kenya imejitokeza na kuweka kitita cha maana cha fedha kwa klabu hiyo.

Taarifa za uhakika ambazo BINGWA imezipata jana, zinasema kampuni hiyo tayari imeweka dau nono mezani linalokadiriwa kufikia Sh bilioni 3.7 kwa ajili ya kuidhamini klabu hiyo.

“Ni kweli tupo kwenye mazungumzo ya mwisho na wadhamini hawa, walileta mapendekezo yao ya udhamini ambao unafikia Sh bilioni 3.7, kwa miaka mitano na ongezeko la asilimia 6 kila mwaka, lakini na sisi kama klabu tuna mapendekezo yetu ambayo tumewapatia hivyo tunaamini tutafikia mwafaka,” alisema mtoa habari wetu wa kuaminika kutoka ndani ya uongozi wa Yanga.

Alisema katika mapendekezo ya mkataba huo, Kampuni ya SportPesa inataka kuidhamini kwa dau la Sh milioni 750 kwa mwaka na kwamba kama suala hilo litakamilika, maana yake Yanga itaanza kuvaa jezi mpya za mdhamini huyo mapema iwezekanavyo.

“Kwa sasa tunavaa jezi zenye nembo ya Quality Group, maana yake kama tutaingia mkataba na SportPesa basi mara moja tutaacha kuvaa nembo hiyo, kwa sasa kinachosubiriwa ni mapendekezo ambayo uongozi umeyatuma kwa kampuni hiyo, kwa kuwa kama unavyojua Yanga ni timu kubwa na hivyo imetoa mapendekezo ya ongezeko la kiwango cha udhamini kwa mwaka hadi kufikia Sh bilioni 1.5 ambayo tunaamini tutafikia mwafaka,” alisema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwassa, alikiri kuwepo kwa dili hilo, huku akifafanua kwamba yapo makampuni takribani matatu  lakini SportPesa ndio waliokaa nao mezani, ingawa bado hawajafikia mwafaka wa kuingia mkataba wa miaka mitano walioutaka.

“Hilo suala lipo na si hao tu, yapo makampuni si chini ya matatu yanahitaji kutudhamini lakini siwezi kuweka wazi hivi sasa kwa kuwa hatujafikia makubaliano rasmi, muda si mrefu suala la fedha halitakuwa tatizo kwetu,” alisema.

Yanga ilitangaza kuhitaji udhamini kutoka kwa makampuni mbalimbali baada ya kumalizika kwa mkataba wake na TBL, ambapo makampuni kadhaa ya ndani na nje ya nchi yaliripotiwa kujitokeza kuwania nafasi hiyo kwa kutoa dau mbalimbali, lakini baada ya mazungumzo ya awali makampuni matatu makubwa ikiwepo SportPesa wamejitokeza kuwa wadhamini wakuu, huku makampuni mengine manne yakitaka udhamini wenza.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -