Tuesday, January 19, 2021

USIACHE UPENYO KWA MWENZAKO, FANYA HIVI

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

USALITI umezidi siku hizi. Kila watu watano uwaonao, watatu kati yao wanasalitiwa na wapenzi wao. Unadhani ni kwanini? Unadhani na wewe uko salama sana katika uhusiano wako?

Wengi wanatoa sababu ya kusalitiwa kuwa ni tamaa za wapenzi wao. Wengine wanasema maendeleo ya sayansi na teknolojia yaliyoleta simu na mitandao ya kijamii imekuwa sababu ya usaliti kuzidi kutamalaki katika jamii kutokana na upana wa mawasiliano kuzidi.

Kwa namna moja ama nyingine zinaweza kuwa sababu. Ila jiulize, kwanini wengine wanasalitiwa na wengine hawasalitiwi na wote wapo katika dunia hii yenye makorokoro yote hayo?

Sababu za usaliti ni nyingi ila moja na ya msingi sana, ni wahusika kutoweka ulinzi katika mahusiano yao. Wewe una ulinzi upi katika mahusiano yako? Mpenzi wako unamfanyia nini hata asione sababu wala haja ya kukusaliti?

Zamani watu waliamini ulinzi katika uhusiano ni kumpa ngono mhusika kwa kiwango cha kutosha. Ila cha kushangaza pamoja na kufanya hivyo tena kwa kiwango kikubwa bado wakajikuta wakisalitiwa.

Baadaye wengine wakaona ulinzi bora wa mahusiano ni fedha. Katika hili nadharia nyingi zikazuka. Wapo waliosema pesa ndiyo chanzo kikuu cha usaliti.

Na wengine wakasema shida za kimaisha ambazo kimsingi ni ukosekanaji wa pesa ndiyo husukuma wengi kusaliti.

Ila pamoja na kutoa hela, kuwanunulia wahusika kila wakitakacho ila bado waliendelea kusalitiwa hata wakibaki wasiamini macho yao.

Swali likazuka, ni nini sasa kifanyike kuzuia usaliti katika uhusiano? Kama ngono na pesa vimeshindwa, nini kidhibiti zimwi hili la usaliti katika mahusiano.

Baada ya tathmini nyingi za wataalamu mbalimbali, ikajulikana ili kupambana na hili tatizo la usaliti kila mmoja ni lazima aweke ulinzi katika uhusiano wake.

Kila mmoja kwa kutumia mbinu na maarifa ni lazima ajitoe kwa mpenzi wake ili mahusiano yawe imara na zimwi la usaliti liweze kushindwa.

Wewe unamfanyia nini mpenzi wako? Unayofanya yanamfurahisha kwa kiwango gani mpenzi wako? Namna yenu ya maisha hayamfanyi akuchoke wala kutamani vya nje?

Hapa inabidi ieleweke vizuri. Namna ya kufanya mahusiano yako yawe na msisimko na yasichoshe, haihusiani na pesa hata kidogo.

Kufanya mahusiano yako yasisimke ni vile namna unavyoishi na mwenzako, namna unavyokuwa mbunifu kwake na jinsi unavyoepuka kumkera kila mara.

Wapo wenye pesa nyingi na bado mahusiano yao yanachosha. Mtu anatoka kazini na gari la kifahari, anaingia katika jumba lake la kifahari kisha yuko busy tu na runinga. Hapa vipi mahusiano hayataboa?

Ama mwanamke yeye kila muda yuko na mavazi mazito mwilini, ana gubu, hamfanyi mwenzake afurahi wala kusisimka kwa furaha. Kwa namna hii hata kama mna bilioni 100 benki, ni kwa namna gani mahusiano haya yasichoshe na kuleta vishawishi vya usaliti?

Ulinzi wako ili mwenzako asikusaliti inabidi umfanyie kila analopenda kwa ubunifu na kwa umakini, umsikilize, umfanye akufikirie kwa maneno yako, kwa matendo yako na kwa uwepo wako.

 

Kila binadamu ana asili ya tamaa. Na tamaa mbaya zaidi ni ile itokanayo na matamanio ya kutaka kufanya ama kufanyiwa kitu fulani. Sasa ili asifikirie kufanyiwa ama kufanya kwingine hakikisha huduma hiyo anaipata kwako.

Jiulize maswali haya kwa umakini ili ujue kama kweli umeweka ulinzi imara kwa mpenzi wako dhidi ya usaliti. Unamfanyia matendo anayopenda mwenzako? Ana shauku ya kukuona, kukusikiliza na kukutana na wewe kimwili?( Kwa wana ndoa), mwenzako akiwa na huzuni anakutegemea wewe kumpa faraja na raha katika maisha? Wewe ni wangapi katika nafsi yake.

Kwa muda wako tafakari kwa kina juu ya maswali hayo na jipe majibu kwa dhati bila kujidanganya. Baada ya kufanya hivyo, hakikisha mahali penye ufa unaziba haraka kabla muda wa kujenga ukuta hujawadia.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -