Wednesday, November 25, 2020

USIMCHUKIE ANAYEKUACHA, JIANDAE KWA FURAHA YA KWELI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

HATA kama u mzuri sana, unavutia sana na una utajiri mkubwa sana. Ila si kweli kuwa unaweza kuwa na msichana/mwanamume yeyote na akakupenda kwa dhati kama inavyopaswa. Mapenzi ni hisia.

Japo unaweza kuwa na pesa ila kama hisia za fulani zikikukataa, magari, majumba, pamoja na mwonekano wako, hautakuwa na thamani kwake.

Umeachwa na mpenzi wako? Baada ya kumfanyia kila kitu kizuri na kumjali kwa kila jema, ameona kheri akuache?

Najua inauma sana ila haina jinsi. Kama kweli ulijitoa kwake kwa kila hali, kwa roho na nafsi, kwa maneno na vitendo na bado akaona ni bora akuache. Huna jinsi!

Mapenzi ni hisia. Huenda alifanya kosa kuja kwako huku akijua hakupendi, ila pia si kitu sana, ni vyema kaondoka.

Kama ungekuwa naye asilani usingeweza kupata furaha na raha ya mapenzi. Ili mapenzi yalete maana ni lazima wakutane  watu wanaopendana. Maana hao ndiyo watajaliana, watathaminiana na kuoneana huruma ya kweli. Ila kama unampenda sana fulani, ila yeye hakupendi kwa namna ya kimapenzi, haina haja. Muache aende!

Hupaswi kumlaani, kumuombea mabaya, wala kuwa na kisasi naye. Nani awezaye kulazimisha mapenzi? Angekuwa nawe kama angekuwa anakupenda. Angekujali na kuthamini chozi lako, kama angekuwa na hisia za kweli na wewe. Kwa kuwa kaondoka kwa sababu hakupendi, nyoosha mikono juu shukuru Mungu. Huna unachoweza kufanya zaidi.

Kumlaani au kumwombea mabaya katika namna nyingine ni kama kumwonea. Hakika  hata wewe ungekuwa yeye huenda ungefanya hivyo. Baada ya kugundua humpendi, siku ingekuja na kutaka kuachana naye.

Nilimsikia kijana mmoja akiongea suala la namna hiyo. Alipendwa sana na msichana aliyekuwa na sifa zote za kuitwa mzuri na tabia zote za kuwa mke, ila moyo wake haukuwa radhi kuwa naye, alijitahidi kila njia kujilazimisha ila nafsi yake iligoma kabisa.

“Kaka, nashindwa kufanya kitu juu ya huyu msichana. Ni kweli ananipenda sana ila kila nikijitahidi kumjali na kurudisha upendo anaonioneshea nashindwa. Kuna wakati mpaka najichukia.

Ni msichana mzuri sana ana tabia njema na kila mtu anamsifia ila ndiyo nafsi yangu haimwelewi kabisa,” aliwahi kuniambia kijana mmoja tukiwa ofisini kwangu!

Wengi wapo kama huyo kijana. Japo anaona upendo anaofanyiwa ila kwa kuwa hisia zake hazipo kwa mhusika, anajikuta anakuwa si mwema sana kwake. Iko hivyo!

Upendo haulazimishwi, haung’ang’aniwi wala kununuliwa. Thamani na ubora wake huja wenyewe!

Ni kweli huenda wakati anakutongoza alikwambia kila neno zuri, akakupa kila ahadi tamu yenye kuburudisha moyo na kusuuza nafsi. Ila kwa kuwa anakiri mbele yako kuwa hakupendi. Mpe mkono wa kwa heri. Hakuna unachoweza kufanya.

Acha kumuwaza sana kwa aliyokufanyia. Jua, kadiri unavyomuwaza ndivyo unazidi kuweka ugumu katika akili yako kumsahau.

Kawaida ya akili inanasa na kuhifadhi kitu unachowaza sana au kusikiliza sana. Ukimuwaza sana anakuwa mgumu kutoka katika akili yako ila ukimpuuza ndivyo inavyokuwa rahisi kuishi bila yeye!

Fikiria mengine.

Jichanganye na watu ili akili yako ione na ijaze vitu vingine. Epuka kukaa peke yako. Jitahidi kujiweka katika mazingira ya kufanya jambo. Ukaaji wa peke yako bila kufanya kitu (Being Idle) unakaribisha fikra juu yake kuingia upya katika akili yako.

Mapenzi si kitu rahisi sana, kama hakupendi jua hakupendi. Wema na zawadi zako atazipokea na kukuona mtu bora katika mtazamo wa kujali ila katika maana ya hisia, bado hautokuwa na nafasi. Maisha yako hivyo. Thamani ya hisia zake haziwezi kupimwa na zawadi pamoja  na maneno yako.

Ndiyo, wapo waliofanya ngono kwa sababu ya zawadi na maneno mazuri. Ila tambua kuna tofauti kati ya ngono na mapenzi. Anaweza kufanya ngono na wewe kama fadhila ya zawadi zako ila kwako hatojihisi amani na faraja kwa kuwa humgusi kihisia. Kuwa makini!

ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -