Friday, October 30, 2020

USIPOGOMBANA NA MOURINHO UTAKUWA ‘CHIZI’

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

KWA lugha nyepesi unaweza kusema usipogombana na Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ukiwa karibu naye, pengine unaweza kuonekana kuwa chizi.

Hii ni kutokana na tabia ya Mreno huyo kuwa mchokozi dhidi ya wenzake, wawe makocha, madaktari wa timu na hata wachezaji.

Tabia hiyo unayoweza kuiita chafu imedhihirika tena katikati mwa wiki hii, baada ya Mourinho kukwaruzana na kocha wa viungo wa timu hiyo, Carlos Lalin, wakiwa kwenye uwanja wao wa mazoezi wa Carrington, wakati timu hiyo ikijiandaa na mechi yao  ya Ligi ya Europa dhidi ya Rostov, iliyopigwa usiku wa kuamkia jana kwenye dimba la Old Trafford na inaelezwa kuwa, tukio hilo si mara ya kwanza kutokea.

Lalin aliwahi kufanya kazi chini ya Mourinho wakati akizifundisha Chelsea na Real Madrid, lakini kwa sasa wawili hao wanaonekana kutokuwa na maelewano mazuri kama ilivyotokea siku hiyo ya Jumatano kabla ya Lalin kuamua kujifungia ndani ya gari lake.

Hata hivyo, Lalin  si mtu wa kwanza kugombana na  Mourinho na ifuatayo ni orodha ya watu 11 ambao  mara kwa mara wamewahi kukwaruzana na ‘Special One’.

1.Anders Frisk

Mwamuzi huyo raia wa  Sweden alikumbana na mdomo wa Mourinho wakati alipomshutumu kwa kumshambulia Kocha wa Barcelona,  Frank Rijkaard, wakati timu hizo zikiwa mapumziko katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2005, wakati huo akiifundisha Chelsea.

Baada kumalizika mechi hiyo, Frisk alipokea ujumbe mwingi wa kutishiwa kuuawa na muda mfupi aliamua kustaafu kuchezesha soka.

2.Pep Guardiola

Uhasama wa makocha hao wa jiji la  Manchester ulianza wakati  Mourinho akiifundisha Inter na ukaendelea wakati alipojiunga na Real Madrid

Hali hiyo ilijitokeza kutokana na kauli ya Mourinho aliyoitoa: “Kwa ujumla siipendi timu ya Pep, Barcelona”.

Na baada ya mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo mwaka 2011 walifungwa wakiwa katika uwanja wao wa  Bernabeu, Mreno huyo akatoa tena maneno ya nyodo akisema: “Sifahamu ni kwa sababu ya udhamini wa  UNICEF ama ni kwa sababu wana vijana wazuri. Sifahamu. Wana nguvu na sisi hatukuwa na nafasi”.

3.Arsene Wenger

Huyu ndiye anayeonekana kuwa hasimu wake mkubwa katika kipindi chote alichowahi kufundisha katika michuano ya Ligi Kuu England kutokana na kwamba, wamekuwa wakikwaruzana mara kwa mara na kufikia hatua ya kutaka kukunjana.

4.Tito Vilanova

Jose Mourinho alimpiga singi la jichoni aliyekuwa kocha wa Barcelona, marehemu Tito Vilanova, mwishoni mwa mechi yao ya marudiano ya Kombe la Hispania, iliyoikutanisha Real Madrid  na mahasimu wao hao mwaka 2011.

Hata hivyo, katika kujitetea, Mourinho aliomba radhi kwa tukio hilo ambalo halikutarajiwa.

5.Antonio Conte

Kocha wa Chelsea, Muitaliano huyo alisherehekea ushindi wake wa kwanza wa mabao 4-0 dhidi ya Manchester United Oktoba, mwaka jana.

Ushindi huo unaonekana kwa asilimia  100 kumuuma Mourinho, ambapo kwa sasa anamuandama kocha huyo kuhusu mtindo wake wa ufundishaji, akidai kuwa timu hiyo imepoteza soka la Ulaya kutokana na kuwa inacheza soka la kujihami, maarufu kama kupaki basi.

6.Mashabiki wa Liverpool

Kocha Jose Mourinho alionesha ishara ya kuwatukana mashabiki Liverpool, jambo ambalo lilimfanya atolewe uwanjani wakati wa mechi ya fainali ya michuano ya Kombe la Ligi iliyopigwa Februari 27, 2005, kwenye Uwanja wa Millennium.

Mwaka 2004 Mourinho kidogo ajiunge na Liverpool, kabla ya kujiunga na  Chelsea na alikuwa kipenzi kikubwa cha mashabiki wa timu hiyo, lakini tangu awaoneshe ishara hiyo ndipo uhasama ukaanza.

Wabaya wengine wa Mourinho ni pamoja na aliyekuwa daktari wa timu hiyo, mwanamama Eva Carneiro, aliyekuwa mlinda mlango wa Real Madrid, Iker Casillas na nyota wake wa sasa, Juan Mata.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -