Friday, October 30, 2020

USITUMIE NJIA HII KULINDA PENZI LAKO NI HATARI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA RAMADHANI MASENGA


 

KATIKA kila maamuzi yako kuna furaha au huzuni yako. Kuwa makini. Neno hili unatakiwa kuliweka akilini na kuliheshimu.

Katika mapenzi suala la umakini ni jambo linaloweza kuamua hatima yako. Ya aidha uwe na furaha au huzuni. Ya ama baadaye ujute ama ufurahi.

Ila kwa bahati mbaya neno umakini huwa halieleweki vizuri kwa baadhi ya watu na ndiyo maana japo wengi hujiita watu makini, ila mara nyingi kuliko kawaida hujikuta wakifanya makosa ya kijinga.

Tunapaosema kuwa makini katika uhusiano maana yake ufanye mambo kwa misingi na tabia za kimapenzi na si vinginevyo.

Kuwa tu mtulivu kwa mpenzi wako haitoshi kama hufanyi masuala mahususi katika mapenzi.

Huenda ukatamani kumpa amani na furaha mpenzi wako. Kwa wazo hilo unaweza kuamua kumpa fedha na baadhi ya zawadi za gharama kwa kuona unafanya umakini wa kumpa furaha. Unakosea!

Umakini katika mapenzi ni kuishi katika misingi ya kimapenzi inayokubalika. Umjali kwa namna inavyofaa na si kwa aina ya kununua.

 

Kama unampa tu pesa bila kumjali, kwa maana ya kuongea naye katika namna ya kimapenzi, kumjulia hali unapoona yuko katika hali tofauti au kumpa tumaini unapoona kuna dalili ya kukata tamaa kuhusiana na jambo lake. Hauko makini.

Mara nyingi nimeona watu wakijiumiza kwa kuingia gharama kubwa hata zile wasizomudu kwa kuamini wanayalinda mahusiano yao.

Wako radhi hata kuuza baadhi ya vitu vya ndani kwa sababu ‘mtu wake’ kahitaji kitu fulani. Haya si mapenzi. Huu ni utumwa wa kisasa.

Ni kweli unahitajika umjali mpenzi wako. Unatakiwa kumfanya kuwa muhimu na maalumu katika maisha yako ili aione dhana ya upendo katika maisha yako.

Ila huwa si hivi. Kufanya hivi japo kwa jicho jingine watu watasema unamjali sana mwenzako ila kimapenzi haiko sahihi.

Kivipi tuseme unamjali sana mwenzako kwa kufanya hivi wakati unajikaanga mwenyewe?

Dhamira ya kuingia katika mapenzi si kuumizana na kutesana, iwe kiuchumi au kihisia. Ni kupeana raha na amani.

Kama unahisi bila kumpa pesa nyingi na kumtoa ‘out’ katika ‘mahoteli’ ya thamani na gharama kubwa kubwa atakuacha. Ni  bora ukubali akuache.

Mpenzi wako katu huwezi kumlinda kwa kivuli cha pesa na kubaki salama. Kama anakupenda, kwa kumjali kwako na kumthamini bila kujiumza atakupenda  zaidi na atakuwa wako.

Kama hakupendi, hana hisia na wewe, kila siku unaweza kumpa pesa na bado kuna kitu muhimu anaweza kukosa kwa ajili yako.

Anaweza asikujali wala kukuheshimu. Pesa sawa, ila haiwezi kufanya mpenzi wako akawa wako.

Atakuwa na wewe na pengine kukutekelezea kila kitu unachotaka, ila akakosa uaminifu wa sababu hana hisia na wewe.

Ni kweli unampenda, unamjali na kumthamini sana ila kuwa makini na matumizi ya fedha juu yake.

Kama kuna ulazima wa kumpa fanya hivyo ila pia usifanye hivyo mpaka ikafikia hatua ya kuumizana.

Mapenzi ni amani na furaha. Kama mwenzako hawezi kukujali kama humpi fedha au kumnunulia vitu vya gharama, hapo hakuna mapenzi.

Kama hutofanya uamuzi wa kuachana naye basi atakuacha wewe ukiwa hoi  kwa matumizi makubwa na yasiyokujali wala kukuonea huruma.

Pesa yako inaweza kukupa ulinzi wa nyumba yako ila sio ulinzi wa penzi lako. Unaweza kumuwekea hata walinzi.

Ukaweza pia hata kumfanya asionane na watu hovyo ila jua dakika atakayokusaliti ni dakika unayoweza kudhani uko salama.

Mapenzi ni mapenzi, si suala la cheo chako wala heshima yako. Kama hakujali pia hatajali fedha yako wala heshima yako. Wangapi wamefanyiwa hayo? Kuwa makini.

Mjali  sana mpenzi wako, mthamini na mfanye kuwa bora katika maisha yako. Ila  kama unahisi penzi lako kwake haliwezi kukolea bila kuwa na kiungo cha pesa, ni vyema ukajiuliza sana kabla hujajiweka kando.

Kwa kuamini pesa zao zinaweza kufanya kitu katika mahusiano, wengi wanajuta leo. Waliwapa pesa nyingi, wakawanunulia hiki na kile ila kwa kuwa wenzao hawakuwa na hisia nao, leo kila mmoja na maisha yake.

Wengine walisalitiwa baada ya fedha kuisha. Wengine walisalitiwa kwa sababu walitokea wenye fedha zaidi yao ila pia wengine waliachwa kwa sababu wahusika waliamua kuwa wa kweli maisha yao.

 

Mbali na kupewa pesa na zawadi, waliamua kwenda mahali nafsi zao zinapohitaji kuwa.Anza kupima leo, huyo anayekwambia nakupenda.

Ni kweli, au anasema hivyo kwa sababu kila wiki unampa laki mbili za matumizi? Huyo anayekwambia hawezi kuishi bila wewe, ni kweli au kwa kuwa unamfanya aishi maisha ya kisasa?

Mapenzi ni furaha ila haiwezi kuwa furaha kama ukiwa na tapeli wa mapenzi. Mapenzi ni furaha kwa kuwa na mtu anayekupenda na kukuthamini kwa namna ulivyo.

Kwa hali yoyote utakayokuwa nayo, si kwa fedha wala cheo chako.  Mapenzi ni raha kama hujanasa katika mtego wa kitapeli. Wengi wanalia leo. Kuwa makini.

Mwanamke kuhudumiwa na mwenzake ni suala zuri. Mwanamke kupewa pesa sio suala la hovyo. Mwanaume kutoa na mwanamke kupokea ni suala la asili.

Ila je, unampa kwa sababu gani? Unampa kwa sababu kasema ni lazima umpe na usipofanya hivyo atakuacha?

Instagram:ramadhan.masenga

Mwandishi wa makala hii ni mtaalamu mbobezi wa masuala ya ushauri wa uhusiano, maisha na utulivu wa hisia( Psychoanalyst)

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -