Saturday, November 28, 2020

USIYEMPENDA KAJA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA SAADA SALIM

USIYEMPENDA kaja. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya kiungo wa Wekundu wa Msimbazi, Mohamed Ibrahim ‘Mo’, kupona majeraha yake na tayari amerejea uwanjani.

Kurejea kwa Mo kunaifanya safu ya ushambuliaji ya Simba kuimarika kuelekea mchezo wao dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Februari 25, mwaka huu.

Hilo linatokana na umahiri alionao kiungo mshambuliaji huyo katika suala zima la kuchezesha timu, kutengeneza nafasi za mabao na kufunga.

Kwa kutambua umuhimu wa mchezo huo wa Februari 25, sasa Simba watakuwa na kila sababu ya kutembea vifua mbele na kuwa na uhakika zaidi wa ushindi dhidi ya Yanga.

Kupona kwa Mo kunazidi kuipa uhai safu ya ushambuliaji ya Simba inayoongozwa na Ibrahimu Ajib na kumeibuka matumaini ya mashabiki wake kuona timu yao hiyo ikifanya mauaji ya kutisha kwenye mchezo dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumamosi ya wiki ijayo.

Ni wazi sasa uwepo wa Mo, Jonas Mkude, James Kotei, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto na Mzamiri Yasin, unalifanya benchi la ufundi la Simba likiongozwa Joseph Omog kutamba, wakiwa na matumaini ya kuwamudu mahasimu wao hao.

Kutokana na majeruhi aliyoyapata akiwa katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, Mo hakucheza mechi tano za Simba zilizopita, tatu zilikuwa za Ligi Kuu Tanzania Bara na mbili za Kombe la Shirikisho (FA).

Kiungo huyo amekuwa msaada mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya Simba ambapo amekuwa tegemeo na kuipa timu yake matokeo.

Huenda kurejea kwa Mo kukawa ni habari mbaya kwa mashabiki wa Yanga kutokana na ukweli kwamba nyota huyo amekuwa mwiba mchungu kwa walinzi wa timu pinzani kutokana na ubunifu wake uwanjani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -