Wednesday, October 28, 2020

UTAMU MIGUUNI MWA MKHITARYAN NA MAAJABU YA ‘DA VINCI’

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

ABDUL KHALID NA MITANDAO (TSJ)


NI karne nne na takribani siku kadhaa zimepita tangu kilipotokea kifo cha mwanadamu aliyewahi kuwa na vipaji murua duniani, Leonardo da Vinci.

Mzaliwa wa Jamhuri wa Florence (hivi sasa Italia). Da Vinci alikuwa ni mwanadamu wa kipekee sana duniani na inasadikika hakuna mwingine aliyewahi kutokea kwa kuwa na vipaji kama alivyokuwa navyo yeye. 1452 ndio mwaka aliozaliwa na alifariki miaka 67 baadaye.

Umaarufu wa Mwitaliano huyu ulichagizwa zaidi na vipaji lukuki vya kuvutia alivyojaliwa.

Mungu alimjalia kuwa na uwezo mzuri katika idara ya sanaa (uchoraji na muziki) pamoja na masuala ya hesabu na sayansi.

Ukiwa ofisini, haitatokea upite mwaka mzima bila bosi wako kukwambia upende unachokifanya, Da Vinci alipenda kazi zake na ndio maana alizidisha ubunifu na kazi zake zikawa bora.

Huyu jamaa alifikia kipindi akawa na uwezo wa kuchora picha akitumia mikono yote miwili kwa ufasaha kabisa na bila kupepesa macho.

Ndiyo, aliweza kukitazama kitu na akakichora kama kilivyo tena akitumia mikono yake yote miwili, Mungu huyu acheni aitwe Mungu!

Huyo ndiye Da Vinci bwana na hata angetaka kucheza mpira labda angeweza kuwa nyota wa kukumbukwa sana nchini kwao na duniani leo hii.

Lakini wakati dunia ikiwa imesahau kabisa uwepo wa wanadamu wenye vipaji vya hali ya juu kama hivi na namna ya kuhakikisha wanavitumia mbali na wao kupeleka watu kusomea vitu kama kuchora, kuimba na hata kucheza kabumbu, lakini bado wenye vipaji wanazidi kutuonesha namna wanavyoweza kuvitumia katika sekta mbalimbali.

Nakumbuka wakati ‘nakodoa macho’ kuitazama mechi kati ya Manchester United na Sunderland wiki hii, nilishuhudia kwa mara ya tatu kocha wa United, Jose Mourinho, akibebwa tena na ubora wa kiungo wake kutoka Armenia ‘a.k.a’ Da Vinci wa soka, Henrik Mikhitaryan.

Kwa mara nyingine tena kiungo huyo alipachika bao kwenye uwanja wa Old Trafford na si bao tu, bali lilikuwa ni bao tamu kuwahi kushuhudiwa na mashabiki wa kugaragazwa wa jiji la Manchester, akiwaacha mashabiki na wapenzi wa soka wakitahamaki na kushindwa kumlaumu mwamuzi wa mchezo ule kwa kile kilichoonekana ni kama alizidi, lakini wakajikuta wakibwatuka kwa mshangao ‘ebwana eeh!’

Ndio, acha washangae maana mpira wa zama za sasa umeingiliwa sana na wakufunzi kutoka katika akademi za soka huku vipaji halisi vikionekana kupotea kabisa.

Tukubali tukatae mpira unapoteza ladha yake bwana, hebu jiulize, usipokaa chini na kumtazama Mkhitaryan au Xherdan Shaqiri wa Stoke City akiuamuru mpira, ni nani atakayekufanya uione ladha ya mpira huu uliojaa haja ya matokeo na mbinu nyingi?

Ipo haja ya kumwacha Mkhitaryan aonyeshe ubora wake kwenye kizazi cha akina Diego Costa na Andy Carroll na huku kiungo akiwa N’Golo Kante kwenye timu pinzani ambayo kwao sera yao ni ‘tusifungwe kwanza kisha tutashambulia kwa kushtukiza’.

Oooh! Machozi yananilenga hasa ninapokumbuka ubora waliokuwa nao wachezaji kama Ronaldinho Gaucho, Zinedine Zidane na Ricardo Kaka, aliyekuwa akikabidhiwa majukumu ya kuiendesha timu dimbani chini ya kocha Carlo Ancelotti takribani miaka nane iliyopita.

Labda kipindi hicho cha nyuma kingemfaa zaidi fundi Henrikh ambaye kocha Mourinho hamuoni kama ni mchezaji wa kuanza kila wiki.

Ndiye Mkhitaryan huyu huyu mwenye uwezo wa kuwa na mpira mguu wa kushoto na kisha akauhamishia upande wa pili na akapiga shuti na likawa bao safi.

Mkhitaryan huyu huyu ndiye aliyetumia mechi 90 kufikisha mabao 23 pale Dortmund alipohamia mwaka 2013 akitokea Shaktar Donetsk.

Kama Mourinho ataendelea kukiamini kipaji hiki halisi cha Mkhitaryan ‘Da Vinci wa soka’ kwa kumpa uhuru wa kuuchora na kuupaka rangi mpira huku akiwaimbisha wenzake muziki wa soka maridadi ndani ya dimba la Old Trafford, basi yapo mengi mazuri atakayovuna huku akitafuna ‘jojo’ zilizobakia kwenye kabati la kocha Sir Alex Ferguson.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -