Tuesday, October 27, 2020

Utatu wa CTN wazaliwa Yanga

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR,

KITENDO cha straika Mzambia Obrey Chirwa kufunga bao lake la kwanza la mashindano akiwa na kikosi cha Yanga kwenye pambano dhidi ya Mtibwa Sugar, kimeibua utatu mpya hatari wa CTN kwenye safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo ya Jangwani.

Utatu huo wa CTN ambao unatokana na majina ya Chirwa, Tambwe (Amissi) na Ngoma (Donald), unakuja kuchukua nafasi ya utatu wa MTN (Msuva (Simon), Tambwe na Ngoma) ambao uliipa Yanga ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na Kombe la Shirikisho Afrika.

Kombinesheni hiyo mpya ilizaliwa rasmi baada ya kiwango kikubwa ambacho kilionyeshwa na Chirwa, Ngoma na Tambwe kwenye mchezo wa juzi dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na miamba hiyo ya Jangwani kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Baada ya mchezo wa juzi kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm, alionekana kukunwa na kiwango kilichoonyeshwa na mastraika hao watatu na kusisitiza kuwa walikuwa chachu ya ushindi wao katika mechi hiyo ambayo timu hiyo ilipata mabao yake kupitia kwa Chirwa, Msuva na Ngoma.

Akizungumza na BINGWA, Pluijm alisema kitu kikubwa ambacho kilimfurahisha kwenye mchezo wa juzi ni kuona straika wake Chirwa akifunga bao lake la kwanza tangu asajiliwe kitu ambacho anaamini kitamrudishia kujiamini kwake.

“Ni mtu (Chirwa) ambaye nilikuwa nategemea ipo siku atafanya vizuri kadiri anavyofanya bidii akiwa mazoezini, nampa pongezi anaweza kuanza kujiamini sasa,” alisema Pluijm.

Mholanzi huyo alisema aliamua kumwanzisha Chirwa kucheza kama pacha wa Tambwe na kumwacha Ngoma akianzia benchi, hiyo inatokana na mpango wake mbadala alioingia nao katika mchezo huo.

“Angalia nina mastraika watatu; Chirwa, Tambwe na Ngoma (CTN), niliamua kumpumzisha Ngoma kutokana na kucheza mechi nyingi sana, lakini pia nilitaka kuwashangaza Mtibwa kwa kumpanga Chirwa,” aliendelea kusema kocha huyo.

Na baada ya mchezo huo, Pluijm sasa anaamini kuwa kiwango walichoonyesha mastaa hao watatu kwenye mechi hiyo ngumu dhidi ya Mtibwa kitakuwa chachu ya kutoa dozi kwenye mechi zijazo za timu hiyo ambayo imepania kutetea taji lake.

Ushindi wa juzi dhidi ya Mtibwa unamaanisha kuwa Yanga sasa imefikisha pointi 14 baada ya kucheza mechi saba ikishinda nne, kutoka sare mbili na kufungwa moja huku ikiwa na kiporo cha mechi moja mkononi.

Mwisho wa wiki hii Yanga inatarajiwa kukutana na Azam kwenye mchezo mwingine wa VPL, lakini safari hii watamkosa Tambwe ambaye anasumbuliwa na majeruhi aliyoyapata kwenye mechi dhidi ya Mtibwa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -