Friday, October 23, 2020

UWEZO, NIA NA SABABU ZA UGANDA KUPIGWA TUNAZO

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA AYOUB HINJO


KILA Mtanzania amekuwa na imani kubwa na kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars ambao wanakipiga na Uganda leo katika Uwanja wa Nelson Mandela, Uganda.

Kikosi cha Taifa Stars hivi sasa kina wachezaji wenye uwezo mkubwa ambao wanacheza soka la kulipwa maeneo mbalimbali.

Ukianza na nahodha, Mbwana Samatta (Ubelgiji), Shaaban Idd Chilunda, Farid Musa (Hispania), Abdi Banda (Afrika Kusini), Himid Mao (Misri), Simon Msuva (Morocco), Hassan Kessy (Zambia) na Rashid Mandawa (Botswana).

Hao ni wachezaji waliopo katika kikosi hicho wanaokipiga soka la kulipwa ambao matumaini ya mashabiki wengi yamelala kwao wakiamini wana kitu kikubwa cha kukifanya dhidi ya Uganda leo.

Rekodi zinaonyesha Uganda huwa wanapata matokeo mazuri pindi wanapokuwa uwanja huo wa Mandela hivi karibuni wakicheza dhidi ya timu za Misri ambao walifungwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na Emmanuel Okwi pia walitoa sare na Ghana.

Pamoja na Uganda kuamini wanayo nafasi kubwa ya kupata matokeo dhidi ya Tanzania, hilo linaweza kuwa tatizo kubwa kwao sababu tayari wanaingia uwanjani wakiwa wanajiamini.

Kwa aina ya wachezaji ambao wapo kwenye kikosi cha Tanzania hasa katika safu ya ushambuliaji, unaweza kuona jinsi gani safu ya ulinzi ya Uganda itakavyokuwa kwenye wakati mgumu.

Samatta ni moja ya washambuliaji bora katika ukanda huu wa Afrika Mashariki anayefanya vizuri kwenye timu ya Genk huko Ubelgiji hivi karibuni ametoka kuisaidia timu hiyo kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Europa.

Samatta alifanikiwa kufunga mabao matano katika michezo mitatu ya hivi karibuni akiwa kwenye kiwango cha juu huku akitabiriwa kuondoka ndani ya kikosi cha Genk dirisha la usajili lijalo.

Pia, Msuva yupo kwenye kiwango kizuri ikiwa ameanza kwa kishindo kikubwa katika kikosi chake cha Difaa El Jadid ya Morocco.

Uwezo alioonyesha ndani ya kikosi hicho unatoa nafasi kubwa kwake kuweza kuisaidia timu ya Tanzania leo kuinyoosha Uganda pale katika Uwanja wa Nelson Mandela.

Tukiacha rekodi zetu mbovu dhidi ya Uganda, hivi sasa tunaweza kusimama mbele kujitamba kuwa tunaweza kufanya chochote dhidi yao.

Si wachezaji wanaocheza soka la kulipwa tu hata wanaokipiga hapa nyumbani wamekuwa na kiwango kizuri kinachoweza kutoa msaada mkubwa ndani ya kikosi cha Taifa Stars.

Ni mchezo ambao utatoa taswira yetu katika Kundi L lenye timu za Lesotho, Cape Verde na Uganda ikiwa mchezo wa kwanza uliopigwa hapa nyumbani tulitoa sare ya 1-1 na Lesotho.

Jambo kubwa zaidi kwa wachezaji wa Tanzania ni kuzingatia kila wanachopewa na kocha wao, Emmanuel Amunike, ambaye huo utakuwa mchezo wa kwanza kwake.

Rekodi za mchezo huo kati ya Uganda na Tanzania katika michezo mitano iliyopita zinaonekana kumbeba zaidi mwenyeji mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela.

Uganda wamefanikiwa kushinda mara tatu dhidi ya Tanzania huku wakitoa sare mara mbili, huku Septemba 1, 2007 ikiwa mara ya mwisho kwa vijana hao wa Emmanuel Amunike kupata ushindi dhidi ya majirani zao.

Jumla timu hizo zimekutana mara  53, Uganda wakifanikiwa kupata ushindi mara 29, Tanzania mara 10 na sare 14.

Mara ya mwisho Uganda kupata ushindi dhidi ya Tanzania ilikuwa Juni 20, 2015 mchezo ambao walishinda mabao 3-0 katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Huku mchezo wa mwisho kuzikutanisha timu hizo ulimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 katika Uwanja wa Nelson Mandela, Uganda ilikuwa Julai 3, 2015.

Taifa Stars wanaweza kufuta aibu hiyo iliyodumu kwa miaka 11 kwa kushindwa kuwafunga Uganda tukijivunia wachezaji na kocha tuliye naye.

Uwezo, nia na sababu ya kuwafunga tunazo hakika kwa aina ya kikosi tulichonacho tunaweza kupata matokeo ya ushindi pale Uwanja wa Nelson Mandela ambao wanajivunia nao kwa rekodi nzuri.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -