Saturday, October 31, 2020

Vardy afunguka sababu nyingine ya kuikataa Arsenal

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Leicester City, Jamie Vardy, amesema kuwa aliwakataa Arsenal kutokana na aina ya soka wanalolicheza.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa England aliiongoza Leicester kufanya vizuri msimu uliopita wa Ligi Kuu England kwa kuifungia jumla ya mabao 24 katika mechi za ligi.

Kiwango hicho cha Vardy, mwenye umri wa miaka 29, kilipelekea Arsenal kutaka kumsajili, lakini alihofia kuhusu aina ya soka linalochezwa ndani ya klabu hiyo na badala yake akaamua kusaini mkataba mpya na Leicester.

“Kukiwa na watu kama Alexis Sanchez na Mesut Ozil ambao wanatengeneza nafasi, Arsenal ilihisi itafaidika na mimi kama vile mimi ambavyo ningefaidika nao,” alisema.

“Lakini pia nilifikiria na upande wa kiufundi, ukiangalia aina ya uchezaji wa Arsenal ambao hawapeleki mpira mbele kwa haraka kama Leicester wanavyofanya.

“Kitu kimoja ambacho nilikuwa na wasiwasi nacho ni kwamba nisingekuwa mshambuliaji muhimu ndani ya Arsenal,” alisema.

Vardy aliongeza kwa kusema kuwa, anataka kubaki Leicester na kuwa sehemu ya mafanikio yatakayopatikana, licha ya kujengwa kwa kile kidogo kilichopatikana.

“Ninafurahia jinsi kila kitu kilivyokwenda.”

Vardy ameanza msimu huu taratibu akitikisa nyavu mara mbili katika michezo sita ya awali waliyocheza mpaka sasa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -