Sunday, October 25, 2020

VARDY, KOBE ALIYEBEBA TASWIRA YA LEO MESSI

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

Jamie Vardy hatafika uwezo wa Lionel Messi, lakini ni mmoja kati ya washambuliaji walio hai ambao ni hatari zaidi Ligi Kuu England.

Vardy ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kuchungulia nafasi, akaiomba pasi huku shingo yake ikiwa nyepesi kugeuka na kuangalia mwelekeo wa pasi hiyo anayopewa.

Ana kasi akiwa na mpira mguuni mwake, ni mtu mwenye uwezo wa kupiga mashuti ya uhakika, kiujumla Vardy anahitaji si zaidi ya mashuti mawili yanayolenga goli ili afunge bao.

Nakiri kusema kwamba, Vardy hana uwezo wa kumzidi straika wa Tottenham, Harry Kane, ambaye ni Mwingereza tishio zaidi kuwahi kutokea England tangu enzi za Alan Shearer.

Lakini Vardy ni mchezaji wa ushindi. Siku zote suala kubwa pekee si kufunga mabao tu, unafanyaje kuisaidia timu yako ishinde? Lazima wachezaji wasaidiane katika kusaka mafanikio.

Vardy ni aina ya wachezaji wanaofanya jitihada zote za kuibeba timu katika kila hali na vile vile kutimiza jukumu lake la kwanza (jukumu kuu) ambalo ni kufunga mabao.

Ni ngumu kusikia Vardy akitupiwa lawama ni kwa sababu anajituma kuhakikisha anacheza katika kiwango chake bora kila kukicha na kufunga mabao ya kutosha anapotakiwa kufanya hivyo.

Kwa miaka mitano aliyocheza Ligi Kuu England, amedhihirisha kuwa ni mchezaji wa kuchungwa katika mechi ambayo timu nzima ya Leicester City inakuwa na hamu ya kusaka ushindi na ikizingatiwa muundo wao wa kiuchezaji ulitengenezwa kumzunguka yeye.

Na kwa sababu hafanani na wachezaji hatari zaidi duniani wenye uwezo wa kutengeneza/kujitengenezea nafasi, siku hizi amekuwa na kasi ya kobe katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu.

Kivipi? Ukitazama orodha ya wafungaji bora wa Ligi Kuu England, kabla ya kuiongoza Leicester City usiku wa leo dhidi ya Arsenal, jina la Vardy ndio kwanza limeambatana na mabao matatu katika mechi sita alizocheza.

Changamoto kubwa kwake ni kwamba timu yake imeshazoeleka kwa kiasi kikubwa hivyo wapinzani wameshatambua namna ya kuwazuia.

Hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kumfanya Vardy asiipate huduma ya kutosha kutoka kwa wenzake kama zamani.

Licha ya changamoto hiyo na pia kutokuwa na umachachari wa kupasua mnyororo wa wachezaji wa timu pinzani hadi kutengeneza nafasi ya kupiga shuti na kufunga mabao kama Lionel ‘Leo’ Messi, lakini angalau kuna kitu anafanana naye.

Bila shaka unafahamu kuwa Messi ni mchezaji hatari kwa timu zote. Kiufupi Messi ni hatari kwa dunia.

Takribani timu zote alizokutana nazo La Liga ameshazifunga mabao. Timu zote kubwa za ligi hiyo zimekutana na balaa lake.

Ana uadui mkubwa sana na timu za Sevilla, Atletico Madrid, Real Madrid na Valencia. Hadi sasa, Messi ameshazifunga timu hizo nne zaidi ya mabao 100 katika mechi zaidi ya 120.

Kwa kuongezea tu, timu nyingine kubwa zinazomtambua vyema Messi ni Man City, Man Utd na Chelsea. Bila kuisahau Arsenal ambao ndio wahanga wakubwa wa mabao ya Messi.

Arsenal peke yao wamefungwa mabao sita, sawa na jumla ya mabao waliyofungwa City, United na Chelsea.

Hapo ndipo mfanano wa Vardy na Messi unapoanzia. Kila mmoja anaifunga timu yoyote anayokutana nayo, iwe ndogo au kubwa, hawachagui adui wa kumuua.

Yeyote mwenye mawazo ya kuwashinda na kuwazuia wao wasishinde, huyo ndiye mhanga wao wa kwanza kabisa. Na huwa hawachelewi kummaliza mapema.

Vardy ni mchezaji hatari si tu kwa West Brom au Bournemouth, hata vigogo wa Ligi Kuu England wameshaonjeshwa shubiri yake. Wanayatambua vyema makali yake asogeapo langoni.

Mpaka kufikia Februari mwaka huu, Leicester City iliposafiri kuifuata Man City, mechi hiyo ilikuwa ni ya 43 kwa Vardy dhidi ya vigogo sita wa ligi hiyo, Man United, Tottenham, Chelsea, Liverpool na Arsenal na City.

Siku hiyo walipigwa bao 5-1, lakini ushindi huo wa City wala haukuwa habari kubwa sana zaidi ya bao pekee la Leicester lililofungwa na Vardy.

Lilikuwa ni bao la 23 dhidi ya City na vigogo wenzao watano. Kumbuka, lilikuwa ni bao la 23 katika mechi ya 43!

Bao alilowafunga City lilikuwa ni la nne katika mechi ya nane. Ameshaifunga Liverpool mabao saba katika mechi nane, Arsenal ambayo anatarajiwa kukutana nayo leo, ameshaifunga mara tano katika mechi sita.

Zilizobakia amezifunga mabao saba katika jumla ya mechi 21.

Leicester inaweza isifurukute kabisa leo mbele ya Arsenal ambayo haijapoteza mchezo wowote tangu Agosti mwaka huu, lakini kuwa na Vardy anayezipenda mechi kubwa kwao ni ahueni.

Licha ya kwamba ana kasi ndogo ya kufunga mabao msimu huu, lakini suala la kupanda kwa wastani wake wa kupiga mashuti 3.69 kwa dakika 90 anazocheza kutoka 1.96 ni moja ya sababu ya Leicester kutokuwa na wasiwasi.

Hili linachangiwa kidogo na mabadiliko ya kikosi cha Leicester, kumbuka Vardy wa moto katika msimu waliochukua taji la Ligi Kuu alikuwa akipenyezewa pasi tamu na akina Riyad Mahrez na Danny Drinkwater, katika timu tishio ya Claudio Ranieri.

Hii ya msimu wa 2018/19 ina kocha mpya, Claude Puel, sambamba na wachezaji wapya akiwemo James Maddison ambaye amechangia mabao mengi zaidi kwa upande wao (mabao mawili, asisti tatu).

Maddison alitua Leicester akitokea Norwich, ni kijana machachari kweli. Anacheza kiungo mshambuliaji na winga ya kushoto kwa ufasaha.

Ubora wake mkubwa ni kutengeneza nafasi hasa kwa kutumia mipira iliyokufa na krosi. Katika mechi zote za Ligi Kuu alizocheza, ameonesha jinsi gani alivyo hatari katika maeneo hayo.

Ana wastani wa kutengeneza nafasi mbili za kufunga mabao kwa dakika 90 anazocheza.

Na mechi bora zaidi kwake ilikuwa ni dhidi ya Newcastle ambayo Leicester walishinda 2-0, alipiga pasi tano za mwisho ambazo kama washambuliaji wangetulia wangefunga zaidi ya mabao hayo.

Kwamba Maddison ndiye mchezaji anayeichezesha vyema Leicester mpya ya Puel na pia ni mchezaji ambaye uwezo wake unataka kumbadilisha Vardy kutoka kuwa kobe hatari, hadi sungura mjanja asiyeshikika.

Je, tutaendelea kuyaona makali ya Vardy dhidi ya Arsenal leo pale Emirates. Tusubiri.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -